Biashara ya kununua korosho Kanda ya Kusini (Lindi & Mtwara)

Clark boots

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2017
Posts
6,770
Reaction score
6,202
Habari za majukumu wakuu!

Nadhani humu kuna watu wanaojihusisha na hii biashara ya kununua korosho(Almaarufu "Kangomba") kule mikoa ya Lindi & Mtwara.

Naomba kwa wale wazoefu basi watoe uzoefu wao kuhusu hii business.

•Wakati sahihi wa kuanza kununua mzigo.

•Maeneo(vijiji) haswa yanayopatikana korosho kwa wingi na bei nafuu.

•Bei ya kuanzia kununulia(?Tsh@1Kg) ambayo ina-tagert faida nzuri baada ya kuuza ghalani.

Nina kahela kangu kadogo hapa nataka niwekeze kwenye hii business.

1619067794943.png

Muda wa kununua korosho mzuri ni kuanzia mwezi wa tisa mwanzoni kwa wilaya za Masasi hususani vijiji vilivyo tarafa ya Mchauru au wilaya ya Newala vijiji vinavyopakana na mto Ruvuma. Kipindi hicho bei ya kangomba(bakuli moja = 1kg) huwa inauzwa shilingi 1,000/= kwa kangomba moja.

Nimetaja wilaya hizo mbili kwa kuanzia maana korosho za eneo hilo huwa zinawahi kukomaa kabla ya korosho zinazopatikana maeneo mengine kama Ruangwa, Nachingwea n.k.

Kwa mfano gharama za kununua kangomba 100 ( Almost 100kgs) ni tshs 100,000/=, jumlisha tshs 1,000/= ya kununua gunia la kuhifadhia, pia ongeza shilingi 10,000/= kama umempa kazi mtu mwingine akununulie mzigo huo.

Usisahau gharama za kusafirisha mzigo huo kwenda ghalani tuseme tshs 1,000/= kwa kiasi hicho cha kangomba 100.
Hivyo jumla kuu kwa gharama ya kununua kangomba 100 ni;
a) Tsh 102,000/= kama unanunua mwenyewe
b) Tshs 112,000/= kama umempa kazi mtu mwingine akununulie.
N.B Bei huwa inapanda ya kangomba kadiri muda unavyosogea mbele au endapo bei ya mnada wa kwanza imekuwa kubwa.
Tuchukulie unataka kununua tani 10, hapo andaa tshs 12,000,000/= pamoja na tahadhari ikiwemo.

Bei ya kuuzia korosho huwa inaamuliwa na soko baada ya mzigo kuuzwa na chama cha ushirika kwenye mnadana. Mfano tuchukulie kila kilo imeuzwa tshs 2,400/=, hapo toa kama tshs 200/= ya ushuru na mengineyo kwa kila kilo hivyo wewe utabakiwa na tshs 2,200/= hiyo ndiyo utakayolipwa.

Bei pia ya soko mnadani huwa ina tabia ya kupanda au kushuka kwa kila mnada unaofanyika.
Ngoja niishie hapo kwa leo.
 
Muda wa kununua korosho mzuri ni kuanzia mwezi wa tisa mwanzoni kwa wilaya za Masasi hususani vijiji vilivyo tarafa ya Mchauru au wilaya ya Newala vijiji vinavyopakana na mto Ruvuma. Kipindi hicho bei ya kangomba(bakuli moja = 1kg) huwa inauzwa shilingi 1,000/= kwa kangomba moja.
Nimetaja wilaya hizo mbili kwa kuanzia maana korosho za eneo hilo huwa zinawahi kukomaa kabla ya korosho zinazopatikana maeneo mengine kama Ruangwa, Nachingwea n.k.

Kwa mfano gharama za kununua kangomba 100 ( Almost 100kgs) ni tshs 100,000/=, jumlisha tshs 1,000/= ya kununua gunia la kuhifadhia, pia ongeza shilingi 10,000/= kama umempa kazi mtu mwingine akununulie mzigo huo. Usisahau gharama za kusafirisha mzigo huo kwenda ghalani tuseme tshs 1,000/= kwa kiasi hicho cha kangomba 100.
Hivyo jumla kuu kwa gharama ya kununua kangomba 100 ni;
a) Tsh 102,000/= kama unanunua mwenyewe
b) Tshs 112,000/= kama umempa kazi mtu mwingine akununulie.
N.B Bei huwa inapanda ya kangomba kadiri muda unavyosogea mbele au endapo bei ya mnada wa kwanza imekuwa kubwa.
Tuchukulie unataka kununua tani 10, hapo andaa tshs 12,000,000/= pamoja na tahadhari ikiwemo.

Bei ya kuuzia korosho huwa inaamliwa na soko baada ya mzigo kuuzwa na chama cha ushirika kwenye mnadana. Mfano tuchukulie kila kilo imeuzwa tshs 2,400/=, hapo toa kama tshs 200/= ya ushuru na mengineyo kwa kila kilo hivyo wewe utabakiwa na tshs 2,200/= hiyo ndiyo utakayolipwa.

Bei pia ya soko mnadani huwa ina tabia ya kupanda au kushuka kwa kila mnada unaofanyika.
Ngoja niishie hapo kwa leo.
Asante sana mkuu kwa hizi nondo zako, bila shaka utakuwa ushawahi Fanya hii kitu au uko kanda hizo za wakulima wa korosho?
 
Habari za majukumu wakuu..!!

Nadhani humu kuna watu wanaojihusisha na hii biashara ya kununua korosho(Almaarufu "Kangomba") kule mikoa ya Lindi & mtwara.

Naomba kwa wale wazoefu basi watoe uzoefu wao kuhusu hii business.
•Wakati sahihi wa kuanza kununua mzigo.

•Maeneo(vijiji) haswa yanayopatikana korosho kwa wingi na bei nafuu.
•Bei ya kuanzia kununulia(?Tsh@1Kg) ambayo ina-tagert faida nzuri baada ya kuuza ghalani.

Nina kahela kangu kadogo hapa nataka niwekeze kwenye hii business.
Pata mtu unayemuamini.

Kuanzia mwezi wa tisa katikati mpaka mwishoni.

Kumbuka kuwa risk kubwa ni mtu anayekununulia.

Mara pesa ya usafiri, mara pesa za viroba, mara hivi mara vile.

Ukijifanya unaenda mwenyewe hutopata mtu, ama gharama itazidi, utafute sehemu ukae, ule uvae n.k

Solution tafuta mtu muaminifu umkabidhi pesa.

Biashara ilikuwa mwaka juzi bwana unanunua 1500 unauza kwa 3800 kudadeki.

Miaka hii usitegemee kuuza kwa 1000, jipange na 1500 wakulima nao wameshtuka 10k hawauzi wengi wao.

Ili uwavute nunua kwa zaidi ya hapo.

Neno langu sio sheria ila tu kuna risk ya kupanda na kushuka kwa bei.

Kwa ufupi kuwa Risk taker.

Risk zenyewe

.kukamatwa
.mtu muaminifu
KUpanda na kushika kwa bei mara paap umenunua kwa 1000 bei ya mnada 1250.
 
Pata mtu unayemuamini.

Kuanzia mwezi wa tisa katikati mpaka mwishoni.

Kumbuka kuwa risk kubwa ni mtu anayekununulia.

Mara pesa ya usafiri,mara pesa za viroba,mara hivi mara vile.

Ukijifanya unaenda mwenyewe hutopata mtu,ama gharama itazidi,utafute sehemu ukae,ule uvae n.k

Solution tafuta mtu muaminifu umkabidhi pesaa.

Biashara ilikuwa mwaka juzi bwana unanunua 1500 unauza kwa 3800 kudadeki.

Miaka hii usitegemee kuuza kwa 1000,jipange na 1500 wakulima nao wameshtuka 10k hawauzi wengi wao.

Ili uwavute nunua kwa zaidi ya hapo.

Neno langu sio sheria,ila tu kuna risk ya kupanda na kushuka kwa bei.

Kwa ufupi kuwa Risk taker.

Risk zenyewe

.kukamatwa
.mtu muaminifu
KUpanda na kushika kwa bei mara paap umenunua kwa 1000 bei ya mnada 1250.
Umenena points kabisa, hasa kama me nataka nimtumie mtu aninunulie japo nami nitajichanganya maeneo mengine kimtindo So an honest person ni muhimu sana ili mambo yaende sawa.
 
Muda wa kununua korosho mzuri ni kuanzia mwezi wa tisa mwanzoni kwa wilaya za Masasi hususani vijiji vilivyo tarafa ya Mchauru au wilaya ya Newala vijiji vinavyopakana na mto Ruvuma. Kipindi hicho bei ya kangomba(bakuli moja = 1kg) huwa inauzwa shilingi 1,000/= kwa kangomba moja.

Nimetaja wilaya hizo mbili kwa kuanzia maana korosho za eneo hilo huwa zinawahi kukomaa kabla ya korosho zinazopatikana maeneo mengine kama Ruangwa, Nachingwea n.k.

Kwa mfano gharama za kununua kangomba 100 ( Almost 100kgs) ni tshs 100,000/=, jumlisha tshs 1,000/= ya kununua gunia la kuhifadhia, pia ongeza shilingi 10,000/= kama umempa kazi mtu mwingine akununulie mzigo huo.

Usisahau gharama za kusafirisha mzigo huo kwenda ghalani tuseme tshs 1,000/= kwa kiasi hicho cha kangomba 100.
Hivyo jumla kuu kwa gharama ya kununua kangomba 100 ni;
a) Tsh 102,000/= kama unanunua mwenyewe
b) Tshs 112,000/= kama umempa kazi mtu mwingine akununulie.
N.B Bei huwa inapanda ya kangomba kadiri muda unavyosogea mbele au endapo bei ya mnada wa kwanza imekuwa kubwa.
Tuchukulie unataka kununua tani 10, hapo andaa tshs 12,000,000/= pamoja na tahadhari ikiwemo.

Bei ya kuuzia korosho huwa inaamliwa na soko baada ya mzigo kuuzwa na chama cha ushirika kwenye mnadana. Mfano tuchukulie kila kilo imeuzwa tshs 2,400/=, hapo toa kama tshs 200/= ya ushuru na mengineyo kwa kila kilo hivyo wewe utabakiwa na tshs 2,200/= hiyo ndiyo utakayolipwa.

Bei pia ya soko mnadani huwa ina tabia ya kupanda au kushuka kwa kila mnada unaofanyika.
Ngoja niishie hapo kwa leo.

Mkuu inaonekana unaielewa vyema hii biashara...naomba unijuze zaidi maana kuna mtu mmoja wa karibu niliongea nae kuhusu issue kama hii ila yeye aliniambia unaweza kuwatumia watu wanaoitwa makatibu, hao unawapa pesa ya kununulia kilo, kisha unawapa na cha juu kidogo i.e Tsh. 200 ili wakakununulie na malipo mengine, kisha wanakuuzia halafu pesa yako itatumwa moja kwa moja kwenye akaunti yako... Hii mkuu imekaaje usalama wa pesa zangu upo kweli kwa mtindo huu?
 
  • Thanks
Reactions: apk
mkuu inaonekana unaielewa vyema hii biashara...naomba unijuze zaidi mana kuna mtu mmoja wa karibu niliongea nae kuhusu issue kama hii ila yeye aliniambia unaweza kuwatumia watu wanaoitwa makatibu, hao unawapa pesa ya kununulia kilo, kisha unawapa na cha juu kdg i.e tsh. 200 ili wakakununulie na malipo mengine, kisha wanakuuzia hlf pesa yako itatumwa moja kwa moja kwenye akaunti yako...hii mkuu imekaaje usalama wa pesa zangu upo kweli kwa mtindo huu?
Duh.. kweli ina hitaji kujifunga macho kweli sasa ukidhulumiwa inakuwaje?

Na mtaji wa kuanzia ni kuanzia shilingi ngap?
 
Mtaji inategemea na nguvu yako tu mkuu, hata kama una milioni 100 watu wanaingia mzigoni, na mwisho wa siku wanakuletea tani zako kadhaa...jamaa aliniambia hata milioni moja na laki 2 sio mbaya kuanza nayo huku ukiusoma upepo...ambapo milioni moja itatumika kununulia korosho kutoka kwa hao wakulima ambapo kwa pesa hiyo utapata tone 1 = 1000 kilo...hizo laki 2 za juu ni za hao uliowapa kazi kwa maana ktk kila kilo wamechukua tsh.200.

Sasa hapo faida au hasara yako itategemea na soko likoje kwa muda husika. Japo aliniambia mara nyingi mnadani bei zinaangukia tsh 2200 - 2500 kwa kilo moja.
 
mkuu inaonekana unaielewa vyema hii biashara...naomba unijuze zaidi mana kuna mtu mmoja wa karibu niliongea nae kuhusu issue kama hii ila yeye aliniambia unaweza kuwatumia watu wanaoitwa makatibu, hao unawapa pesa ya kununulia kilo, kisha unawapa na cha juu kdg i.e tsh. 200 ili wakakununulie na malipo mengine, kisha wanakuuzia hlf pesa yako itatumwa moja kwa moja kwenye akaunti yako...hii mkuu imekaaje usalama wa pesa zangu upo kweli kwa mtindo huu?
Dah mimi hiyo risk siiwezi kwakweli
 
Hilo lipo, kikubwa tafuta mtu unayemuamini awe katibu au mwingine tu atakufanyia kazi hiyo. Kisha mkabidhi hela kidogo kidogo. Ninarudia mpe hela kidogo kidogo. Mfano una tsh milioni moja, unampa laki moja ikiisha anakukabidhi mzigo unapima ghalani (kwenye kituo cha chama cha ushirika), ukiona mwelekeo unaridhisha unampa tena laki moja nyingine na utaratibu ni uleule kama nilioutaja hapo juu.

N.B. Suala la fedha usalama ni 50/50 endapo haushiriki mwenyewe kwenye kuhakiki mzigo unaonunuliwa na kuandikisha taarifa zako sahihi wakati wa kupima mzigo ghalani.

Hivyo ili uwe na usalama hakikisha unakuwepo kwenye eneo la tukio wakati wa kupima mzigo na malipo ya fedha yanaingizwa kwenye account number yako.

Pia endapo hauko karibu na eneo la tukio hakikisha siku ya kupima mzigo uwepo na ujaze taarifa zako.

Vinginevyo itakuwa sawa na yule aliye mjini huku akilima shamba la mpunga kijijini kwao kwa njia ya tigopesa/m-pesa bila ya yeye kushuhudia chochote huku akitegemea kwenda kuvuna tu.
 
Hiyo mbinu ilitumika zamani. Wengi walifungwa wengine walitaifishwa Mali zao kuna waliouza rasimali zao ili kulipa madeni.

Kama wewe ni riskiteka karibu tujumuike.
 
Kwamba hao waliofungwa walikula pesa za watu ambazo walipewa kwa ajili ya kununulia mzigo? Au watoa mitaji ndo waliofungwa?
 
Hilo lipo, kikubwa tafuta mtu unayemuamini awe katibu au mwingine tu atakufanyia kazi hiyo. Kisha mkabidhi hela kidogo kidogo. Ninarudia mpe hela kidogo kidogo. Mfano una tsh milioni moja, unampa laki moja ikiisha anakukabidhi mzigo unapima ghalani (kwenye kituo cha chama cha ushirika), ukiona mwelekeo unaridhisha unampa tena laki moja nyingine na utaratibu ni uleule kama nilioutaja hapo juu.

N.B. Suala la fedha usalama ni 50/50 endapo haushiriki mwenyewe kwenye kuhakiki mzigo unaonunuliwa na kuandikisha taarifa zako sahihi wakati wa kupima mzigo ghalani.
Hivyo ili uwe na usalama hakikisha unakuwepo kwenye eneo la tukio wakati wa kupima mzigo na malipo ya fedha yanaingizwa kwenye account number yako.
Pia endapo hauko karibu na eneo la tukio hakikisha siku ya kupima mzigo uwepo na ujaze taarifa zako.
Vinginevyo itakuwa sawa na yule aliye mjini huku akilima shamba la mpunga kijijini kwao kwa njia ya tigopesa/m-pesa bila ya yeye kushuhudia chochote huku akitegemea kwenda kuvuna tu.
Shukrani sana mkuu, umezidi kunifumbua macho, kwa hiyo km mambo yakienda vizuri na ukawapata watu waaminifu sio dili baya au sio!
 
Muda wa kununua korosho mzuri ni kuanzia mwezi wa tisa mwanzoni kwa wilaya za Masasi hususani vijiji vilivyo tarafa ya Mchauru au wilaya ya Newala vijiji vinavyopakana na mto Ruvuma. Kipindi hicho bei ya kangomba(bakuli moja = 1kg) huwa inauzwa shilingi 1,000/= kwa kangomba moja.

Nimetaja wilaya hizo mbili kwa kuanzia maana korosho za eneo hilo huwa zinawahi kukomaa kabla ya korosho zinazopatikana maeneo mengine kama Ruangwa, Nachingwea n.k.

Kwa mfano gharama za kununua kangomba 100 ( Almost 100kgs) ni tshs 100,000/=, jumlisha tshs 1,000/= ya kununua gunia la kuhifadhia, pia ongeza shilingi 10,000/= kama umempa kazi mtu mwingine akununulie mzigo huo.

Usisahau gharama za kusafirisha mzigo huo kwenda ghalani tuseme tshs 1,000/= kwa kiasi hicho cha kangomba 100.
Hivyo jumla kuu kwa gharama ya kununua kangomba 100 ni;
a) Tsh 102,000/= kama unanunua mwenyewe
b) Tshs 112,000/= kama umempa kazi mtu mwingine akununulie.
N.B Bei huwa inapanda ya kangomba kadiri muda unavyosogea mbele au endapo bei ya mnada wa kwanza imekuwa kubwa.
Tuchukulie unataka kununua tani 10, hapo andaa tshs 12,000,000/= pamoja na tahadhari ikiwemo.

Bei ya kuuzia korosho huwa inaamliwa na soko baada ya mzigo kuuzwa na chama cha ushirika kwenye mnadana. Mfano tuchukulie kila kilo imeuzwa tshs 2,400/=, hapo toa kama tshs 200/= ya ushuru na mengineyo kwa kila kilo hivyo wewe utabakiwa na tshs 2,200/= hiyo ndiyo utakayolipwa.

Bei pia ya soko mnadani huwa ina tabia ya kupanda au kushuka kwa kila mnada unaofanyika.
Ngoja niishie hapo kwa leo.
Helpful... Asante mkuu!!
 
Back
Top Bottom