Hizo ndio lugha zao ili akuvutie maji madogo akukamate kirahisi.
1. Makatibu wengi wanatumika na watu wengi hata baadhi ya wakubwa ambao wanashiriki kwa Siri biashara hii pia huwatumia makatibu.
Mara nyingi ukiwapa pesa nao pia wanatoa ajira kwa watu waliochini hapa utaona mnyororo wa wadau unavyoongezeka.
2. Baadhi ya makatibu pia ni wezi, kwa ambae biashara ya kangomba huijui wanakupiga ktk ujazo, hapa wanaiba hivi, Kama bei ya kangomba ni buku atakukabidhi gunia lililojaa vzr tu kwa hoja kuwa hizo ni kilo 100, ambazo sawa na kangomba 100. Ukweli ni kuwa kangomba 100 zinatoa kilo 120, hapo akili kichwani mwako.
3. Makatibu wengi huwa wanaushirikiano na wezi, hapa Kuna sinema za kuvamiwa, na sinema za kuvunja nyumba ili mradi mzigo uibwe!
Kwa uchache tafakuri hizo, nikitulia nitaahuka zaidi, Ila nakusisitizia ndg yangu naamini ni mtanzania mwenzangu ambae unapambana kwa ajili ya familia, makatibu achana nao.