Biashara ya kununua korosho Kanda ya Kusini (Lindi & Mtwara)

Biashara ya kununua korosho Kanda ya Kusini (Lindi & Mtwara)

Mimi nipo hapa newala vijijini sehemu moja wanapaita tawala na hii ndio kazi yangu kubwa na korosho za huku ni nene sana
mkuu tupe ripoti za huko...mishe zinakwendaje? Mzigo unapatikana wa kutosha..?
 
Mm Nina shamba na pia Nina Senti nataka kuitia kwenye kangomba Niko Dar naondoka 15/9 Kama Kuna anatamani aingie huko nicheki inbox tupange Kama unataka kuja mwenyewe utafikia home
Mkuu vipi uliwahi kuondoka? Na upepo unasemaje huko? Mzigo ushaanza kununuliwa? Upatikanaji wake ukoje na bei zake vp
 
Sasa Hv bei ya korosho imeshafika 2000/=mtaani na jinsi inavyoonekana mwaka huu zitakuwa na bei mzuri sana huko mnadani
 
Sasa Hv bei ya korosho imeshafika 2000/=mtaani na jinsi inavyoonekana mwaka huu zitakuwa na bei mzuri sana huko mnadani
Daah kilichotokea sasa kwenye bei ya mnadani, nadhani ni biashara ya kubeti tu aisee, Bei ya korosho ya juu Sana minadani kwa mwaka huu ni 2400, nasikia Kuna Senti kadhaa inachukuliwa katika kila kilo moja,
 
Nimeamua huku kusini mwaka huu, nimejaribu hii biashara, Kangomba watu walinunua elfu mbili, na mimi nikanunua kwa Bei hiyo, mnadani zimenunuliwa kwa Bei ya 2400, wakikata hapo huo ushuru, hakuna biashara isiyo na changamoto aisee, ndio kujifunza, mwakani nikijaliwa uzima naacha kwanza mpaka nijue Bei,
 
aise, unaweza kujikuta unatengeneza faida ya shilingi mia hamsini kwa kila kilo moja badala ya buku uliyokuwa umeiplan...si mchezo😅 hapa ndo nnapoamini hakuna pesa rahisi rahisi hapa duniani
 
Sio biashara ya kukurupukia..watu wanakata mtaji sio poa..kuna wahuni waliingia front kununu kwa 2500..bei ya mnadani ni 2400..noma sana...ila mkulima hana hasara

#MaendeleoHayanaChama
 
Sasa Hv bei ya korosho imeshafika 2000/=mtaani na jinsi inavyoonekana mwaka huu zitakuwa na bei mzuri sana huko mnadani
Mara hii kangomba wamepigwa bao haswaa.

Mtu ananunua korosho 2000 kangomba alafu mnada unatangazwa kilo 2350 ukitoa ushuru inabaki 100 ndio faida

hapo kwenye 100 ukitoa wanunuzi,ukitoa muda uliotupa N.k kinachobaki ndio faidaa
 
Back
Top Bottom