Biashara ya kununua mashamba na kukata viwanja kisha kuuza

Ghost.js

Senior Member
Joined
Jul 1, 2015
Posts
188
Reaction score
347
Habari. Hii ni biashara nzuri sana hasi ukiwa na mtaji. Mtaji wake unapaswa uwe na pesa ya kununua kuanzia heka 1.

Mfano ukinunua heka 1 kwa shilingi million 22, eneo hilo(Kibaha) viwanja vinauzwa kuanzia million 3.5 vya mbele na vya nyuma ni million 3.3, kwenye heka 1 unaweza toa viwanja 10, kama una dalali mzuri na matangazo ndani ya mwezi na nusu umemaliza heka. Piga hesabu utapata faida kiasi gani.

Kama unaitaji hii biashara basi karibu, mimi ni dalali nipo Kibaha nitakuongoza kila hatua.
Kama pia kuna mwenye kuweza tukakaa chini na kukubaliana kwa mikataba basi karibu tufanye kazi.
Mawasiliano yangu ni

0744757738/0784376888
 
Mkuu, unahitaji mtu aweke sh 22m ili wewe uiuze kwa sh 35m sio? Ukifanikiwa kuuza sh 100m, 65m inakuwa ya...?

Madalali na pepo, ni pepo na jehanamu!
Hauwezi nunua shamba la million 22 ukapata hiyo pesa unasema, sababu mazingira halisi yanaonesha bei ya hivyo viwanja, na kwenye mauzo, ni makubaliano, kwamba mwenye mtaji anachukua asilimia fulani toka kwenye faida ya kila kiwanja na dalali anapata asilimia fulani, ila mwenye mtaji atakuwa juu kwenye faida inaweza kuwa asilimia 80% kwa 20% ni kutokana na makubaliano ya kazi
 
Kwenye heka moja unapata viwanja 8 venye 500sqm, viwanja 10 vyenye 400sqm. Kama sijakosea, unapata 35mil. Kama uliwekeza 22mil. sasa faida ya kuuza vyote viwanja 10 ni 13mil....
 
wauzaji wote wa viwanja kibaha, viwanja vyao havifiki ukubwa wa 400sqm. Kama wanavyo tangaza
wote wanauza viwanja vya ukubwa wa 225sqm, na hapa ndipo watu wanapo pigwa. unaambiwa kiwanja cha 20 kwa 20 bei milion mbili na unalipa kwa awamu!

Kuna wenyeji wanauza viwanja vya 20 kwa 20 =400sqm kwa Tshs 1,400,000 tu.
Nenda maeneo ya Mikongeni, viziwa ziwa, Mnemela, Mkalmbati. Kuna wenyeji wanauza hivyo viwanja
 
Asante kwa hili mkuu.
 
Nipo hapa mkuu natamani hii biashara kwa moyo wote wote.....sema mtaji wangu bado mdogo mdogo maana huwez ukawa na milioni 22 alafu zote uwekeze ubaki sifuri.
Unaweza lipa nusu, mkaandikiana mkataba baada ya muda unamaliza deni
 
wauzaji wote wa viwanja kibaha, viwanja vyao havifiki ukubwa wa 400sqm. Kama wanavyo tangaza
wote wanauza viwanja vya ukubwa wa 225sqm, na hapa ndipo watu wanapo pigwa. unaambiwa kiwanja cha 20 kwa 20 bei milion mbili na unalipa kwa awamu!

Kuna wenyeji wanauza viwanja vya 20 kwa 20 =400sqm kwa Tshs 1,400,000 tu.
Nenda maeneo ya Mikongeni, viziwa ziwa, Mnemela, Mkalmbati. Kuna wenyeji wanauza hivyo viwanja
Nipeleke kwenye hizi bei boss
 
Mkuu ni biashara nzuri ila usizidishe chumvi, kusema mwezi ni kuzidisha michumvi na kutoa false hope, uhalisia ni unaweza kaa na kiwanja miezi hata 6 mpaka mwaka hakijanunuliwa kikaisha.

Kama kweli ni mwezi, Kwanini hamuongei na mwenye kiwanja mkakata mkauza moja kwa moja ndani ya mwezi kwa 35m?

Kwanini mtu anunue chote yeye ndo akate? Au hamtaki pesa? Sema ni biashara nzuri sababu ni salama na kiwanja hakiozi, utauza tu.

Back
Top Bottom