Hii inatufanya watanzania hatuendi mbele kwa haraka.,
Kama unamtaji wa kununua au kulima ukapata gunia 2000, unashindwaje kuongezea dhamani hayo mahindi?
Kiroba cha kilo 25 ya unga uwe dona au sembe ni 22000 kwa Dar, ukisaga kunia moja unaweza kupata vitoba 3 kwa sembe au 4 kwa dona achilia mbali Pumba . Sasa kwann tunauza chakula ghafi!!??. Ni ajabu sana kwa mikoa ya mpakani na Kenya kama Kilimanjaro na Arusha, watanzania wanapeleka mahindi ghafi Kenya wenzetu wanayaongezea dhamani na kurudisha tena Tanzania kuuza kwa bei kubwa.
Ni vyema mkaungana kama mitaji haipo kubadili mambo.