Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Hii ni biashara nzuri na inalipa sbb inakupunguzia risk ya kulima kwa kutegemea mvua. Pia kama biashara nyingne yoyote inayo changamoto zake. Lakini ni biashara yenye faida ukiifanya kwa makini. Labda uwe specific unataka kipi?
 
Msimu uliopita wakati wa mavuno tumenunua mahindi kwa bei kubwa lakini sasa tunayauza kwa bei ndogo ukilinganisha na bei tuliyonunulia wakati wa mavuno
 
Hii biashara ina changamoto sana mkuu tena kama ndio mwanzo unaweza kata tamaa.
 
Hii biashara ina changamoto sana mkuu tena kama ndio mwanzo unaweza kata tamaa
Hili ndio tatizo letu kubwa Watanzania. Ungeziweka bayana hizo changamoto husika.

Kuna ndugu zangu wanafanya hizi biashara na changamoto ni chache sana ukilinganisha na faida. Haswa ukiingia mwenyewe site/front kuliko kutuma watu wakufanyie kazi.

GeorgeGab hii ni biashara nzuri, ila inatakiwa uifanye mwenyewe na kuwa makini. Unapenda kufanya biashara ya mazao gani? Labda ukiainisha hapa unaweza kupata ushauri zaidi.
 
Hili ndio tatizo letu kubwa Watanzania. Ungeziweka bayana hizo changamoto husika.
Kuna ndugu zangu wanafanya hizi biashara na changamoto ni chache sana ukilinganisha na faida. Haswa ukiingia mwenyewe site/front kuliko kutuma watu wakufanyie kazi.

GeorgeGab hii ni biashara nzuri,Ila inatakiwa uifanye mwenyewe na kuwa makini. Unapenda kufanya biashara ya mazao gani? Labda ukiainisha hapa unaweza kupata ushauri zaidi.
Na hili pia ni tatizo letu kubwa jingine Watanzania tunapenda kuwapa moyo wenzetu bila kuwaelezea changamoto za biashara husika..

Ngoja nipate muda nirudi kuelezea vizur
 
Na hili pia ni tatizo letu kubwa jingine Watanzania tunapenda kuwapa moyo wenzetu bila kuwaelezea changamoto za biashara husika..

Ngoja nipate muda nirudi kuelezea vizur
Siku zote kinachotuangusha na kutukwamisha Watanzania ni nafsi zetu/yako mwenyewe. Tunagangamala na kulia lia sana kwenye changamoto badala ya kuona Fursa ndani ya hizo changamoto. Nasubiri upate huo muda wa kuzianisha hizo changamoto ambazo zinakatisha tamaa katika biashara ya mazao.
 
Ndugu na Jamaa zangu, naomba ushauri nataka kufungua biashara ya nafaka Dodoma mfano mchele ,unga wa sembe na maharage ,je mazingira yapoje uko naweza kufanikiwa wazo langu.
 
moja ya changamoto uwe tayari wakati wote kuuza kwa bei ya kupangwa na serikali kwani serikali inaiingiliaga bei za mazao hasahas vyakula ili kuwalinda walaji(wananchi) waweza wewe uwe umenunua kwa bei kubwa ukaambiwa uza kwa bei ya kupangwa na serikali uwe makini sana kwa mazao yanayoweza haribika kabla ya kuwa sokoni nakutakia biashara njema.
Hilo ndiyo tatizo maana hapo unaweza ukakuta mtaji wako wote umeishia hasara.
 
Nina mdogo wangu kahitimu masomo yake mwaka jana, sasa nimeona anakaa tu nyumbani hana kazi amelima lakini ameuza kwa hasara.

Sasa nimempa mtaji wa million 1 na nimemshauri afanye biashara ya nafaka (mchele, maharage, karanga) atakuwa anaagiza mzigo halafu anasambaza kwa mamantilie, maduka, vibanda na hata majumbani, nimempa pikipiki kwa ajili ya kuzunguka kuchukua order na kusambaza.

Biashara hii itamlipa? Ushauri zaidi unahitajika, target yake ni kupata Tsh laki 2 kama faida kwa mwezi.
 
Akiwa na nidham ya kazi, na kama anajitambua atafanikiwa. Kama ungemwongezea kidogo ingependeza zaidi, japo kiasi ulichompa si haba.
 
Wazo zuri na maamuzi mazuri pia, lkn je kabla ya kumpa hiyo ela/mtaji mmejaribu kukaa chini angalau hata kidgo mkaelimishana kuhsu hiyo biashara.

Jinsi ya kuiendesha, wateja wake, changamoto, mahesabu ya kupata faida na kila kitu?
Maana kumpa tu mtaji aanze ikiwa hana ujuzi au uzoefu na biashara inaweza kuwa changamoto kwake akashindwa kuifanya kwa ufasaha.

But all in all ni biashara nzuri sana na inafaida nzuri.
 
Kama ajielewa na ana moyo wa kufanya hiyo kazi, atafanikiwa. Endelea kumtia moyo hiyo kazi ina changamoto nyingi. Umefanya vema.
 
akiwa na nidham ya kazi, na kama anajitambua atafanikiwa.
kama ungemwongezea kidogo ingependeza zaidi, japo kiasi ulichompa si haba.
Ndio anaanza nikiona ana mwelekeo mzuri nitamuongeza, naogopa kumpa nyingi maana biashara yenyewe ni ngeni kwake.
 
Wazo zuri na maamuzi mazuri pia, lkn je kabla ya kumpa hiyo ela/mtaji mmejaribu kukaa chini angalau hata kidgo mkaelimishana kuhsu hiyo biashara.

Jinsi ya kuiendesha, wateja wake, changamoto, mahesabu ya kupata faida na kila kitu?
Maana kumpa tu mtaji aanze ikiwa hana ujuzi au uzoefu na biashara inaweza kuwa changamoto kwake akashindwa kuifanya kwa ufasaha.

But all in all ni biashara nzuri sana na inafaida nzuri.
Wazo zuri na maamuzi mazuri pia, lkn je kabla ya kumpa hiyo ela/mtaji mmejaribu kukaa chini angalau hata kidgo mkaelimishana kuhsu hiyo biashara.

Jinsi ya kuiendesha, wateja wake, changamoto, mahesabu ya kupata faida na kila kitu?
Maana kumpa tu mtaji aanze ikiwa hana ujuzi au uzoefu na biashara inaweza kuwa changamoto kwake akashindwa kuifanya kwa ufasaha.

But all in all ni biashara nzuri sana na inafaida nzuri.
Nimempa kila aina ya muongozo nimemuunganisha mpaka na watu wa kumtumia mzigo, mengine elimu yake itamuongoza.
 
Back
Top Bottom