Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Habari members,

Naomba nielimishwe kidogo kuhusu biashara ya kununua mpunga kutoka kwa wakulima na kuuza kwa wafanyabiashra, napenda kujua biashara hii inafanyikaje nikiwa na maana ni wapi naweza nunua mpunga kutoka kwa wakulima, bei ya gunia moja,uhifadhi wake na masoko yake.

Asante
 
Habari wana JF,Ningependa kujua faida na hasara ya biashara ya kuuza magunia ya mpunga kutoka mkoani kuja Dar.
 
Ninataka kuingia kwenye biashara ya mazao hasa nafaka Kama mahindi na mpunga, naomba ushauri wa source zenye low price lakini ubora wa juu wa mazao hayo humu nchini.

Lakini Pia naomba kujua masoko mazuri ya mazao hayo na jinsi ya kusafirisha kwa bei nafuu zaidi.
Mtaji wangu mdogo lakini ni bora kuanza kidogo kuliko kupotezea fursa.
 
Nenda field, hapa ataishia kupata taarifa ambazo haziakisi Soko halisi
 
Jamani wana JF naombe makadirio ya matumizi yani gharama na mavuno ya ekari moja ya mpunga. Reference mkoa Wa Morogoro
 
Nakumbuka niliwahi kufanya CBA ya mpunga nikilimia Mahenge ambapo faida ya kulima ekari moja ya mpunga unaotegemea mvua ilikuwa laki nne na nusu (450,000) na mtaji wake ukijumlisha na kukodi shamba ilikuwa 250,000
 
Turiani, mvomero, kilosa, bei ya shamba roba debe 9 linakwenda 45 hadi 50 kwa kipindi cha mavuno mwezi 6,7, ukifika mwezi nov, dec, January, feb, Mach, roba Lina fika 90,110,hadi 120 hio kwa bei ya stock, ila ushauri nunua kipndi cha mvuno weka gharani baada ya muda unauza kwa bei ya juu faida ni pasu kwa pasu.
 
Habari wanajamii habari za humu ndani mimi ni kijana nataka kuingia kwenye biasahara ya kununua mpunga mashambani kisha kuleta mjini kwa
 
Lau ningekua ninaujua uwezo wa mtaji wako Kuwa kiasi chako kimefika 15. M ningekushauri ujiingize ktk biashara ya kufuata nafaka mikoani na kuleta hapo Dar ktk soko kama tandika wapo madalali wazuli huwa Wana pokea mali na baada ya siku 3 au 5 unakabiziwa pesa unaendelea na kufanya hiyo baada ya muda mfupi Utaona faida ya hili
 
Habari wanajamvi.

Hali ya sasa kiuchumi inahitaji biashara muhimu tu ili kuweza kuilinda pesa.Mahitaji ya chakula yanazidi kuongezeka siku hadi siku,na upatikanaji wake baadhi ya maeneo umekuwa mgumu kutokana na sababu kadha wa kadha. Leo nimeona tupeane mawazo mazuri kwenye biashara ya mazao ya nafaka kama vile mpunga, ngano, dengu, maharage, kunde, njugumawe n.k ikiwa ni vyakula maarufu nchini.

Kwa mweye ujuzi wa namna biashara hii inavyoendeshwa maeneo mbalimbali nchini atujuze. Kadhalika na njia bora za masoko pamoja na changamoto zake.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom