Naomba nielimishwe kidogo kuhusu biashara ya kununua mpunga kutoka kwa wakulima na kuuza kwa wafanyabiashra, napenda kujua biashara hii inafanyikaje nikiwa na maana ni wapi naweza nunua mpunga kutoka kwa wakulima, bei ya gunia moja,uhifadhi wake na masoko yake.
Ninataka kuingia kwenye biashara ya mazao hasa nafaka Kama mahindi na mpunga, naomba ushauri wa source zenye low price lakini ubora wa juu wa mazao hayo humu nchini.
Lakini Pia naomba kujua masoko mazuri ya mazao hayo na jinsi ya kusafirisha kwa bei nafuu zaidi.
Mtaji wangu mdogo lakini ni bora kuanza kidogo kuliko kupotezea fursa.
Nakumbuka niliwahi kufanya CBA ya mpunga nikilimia Mahenge ambapo faida ya kulima ekari moja ya mpunga unaotegemea mvua ilikuwa laki nne na nusu (450,000) na mtaji wake ukijumlisha na kukodi shamba ilikuwa 250,000
Turiani, mvomero, kilosa, bei ya shamba roba debe 9 linakwenda 45 hadi 50 kwa kipindi cha mavuno mwezi 6,7, ukifika mwezi nov, dec, January, feb, Mach, roba Lina fika 90,110,hadi 120 hio kwa bei ya stock, ila ushauri nunua kipndi cha mvuno weka gharani baada ya muda unauza kwa bei ya juu faida ni pasu kwa pasu.
Lau ningekua ninaujua uwezo wa mtaji wako Kuwa kiasi chako kimefika 15. M ningekushauri ujiingize ktk biashara ya kufuata nafaka mikoani na kuleta hapo Dar ktk soko kama tandika wapo madalali wazuli huwa Wana pokea mali na baada ya siku 3 au 5 unakabiziwa pesa unaendelea na kufanya hiyo baada ya muda mfupi Utaona faida ya hili
Hali ya sasa kiuchumi inahitaji biashara muhimu tu ili kuweza kuilinda pesa.Mahitaji ya chakula yanazidi kuongezeka siku hadi siku,na upatikanaji wake baadhi ya maeneo umekuwa mgumu kutokana na sababu kadha wa kadha. Leo nimeona tupeane mawazo mazuri kwenye biashara ya mazao ya nafaka kama vile mpunga, ngano, dengu, maharage, kunde, njugumawe n.k ikiwa ni vyakula maarufu nchini.
Kwa mweye ujuzi wa namna biashara hii inavyoendeshwa maeneo mbalimbali nchini atujuze. Kadhalika na njia bora za masoko pamoja na changamoto zake.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.