Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Ukiwa na muda, naomba unieleweshe hicho kisa kutaifisha sukari.

Binafsi huwa naona biashara nzuri ni kununua mazao kwa bei ya chini, kipindi cha mavuno na kuyahifadhi ili kusubiri bei ipande ndipo uuze.

Sent using Jamii Forums mobile app
CTM
Hilo tukio lilitokea 2016kama sikosei...ilikua patashika.wahindi walikonda
 
Haya mambo upepo ukiwa wako unapiga hela watu wamepiga hela sana msimu huu tuliotoka..kwa sasa mahindi mapya kwa maeneo wengi yameanza kutumika kabla ya hapo mahindi gunia yalikua laki20 sasa maeneo mengi mahindi ni elf40 hadi elf60 na mikoa mingi mahindi bado yapo shambani.

Kuna uwezekano mahindi yakashuka zaidi ya hapo miezi michache kuanzia sasa lakini pia kuna uwezekano mkubwa mwishoni kwa mwaka huu mahindi yakarudi tulikotoka gunia 120k

Mwaka huu mvua ni nyingi in terms of quantity but not productive... Mazao wengi yanaharibika/ yataharibika kwa wengi wa mvua

NB..Beti kistaarabu
#tukutane kiangazi mjini
 
Umetiki by 100% mkuu!
Yeah gunia la debe 6 limefika hadi 120K kwa mikoa kama Shinyanga!

Shida ya biashara ya mahindi kwa miaka ya nyuma bei ikichangamka serikali inaachia maghala yake ku-neutralize bei.

Ila sasa kwa kuwa mwenyewe kadai hatompangia mkulima bei mambo yatakuwa vizuri.
 
Mwaka huu Mahindi yatakuwa ya shida zaidi kutokana na mvua kuharibu hasa waliolima October na November 2019.

Mwenye mtaji afanye hima bei ikishuka hiyo March/April kwa maeneo watakayopata vizuri!

Ila mpunga hata 36,000 kwa gunia utafika msimu huu.
 

Hahaha jamaa angu uandishi wako unaonekana kabisa ni muajiriwa unatamani kuanza biashara lakini mwoga , biashara sio mtaji tu kama unavyosisitiza wewe kuwa uwe na 100+m kutoboa , unaweza ukawa na hiyo hela na usitoboe vile vile na mwenye ten m akawa na strategy nzuri na akatoboa vile vile , mshahara wa m1 ni kitu sasa pango , ule , uvae, ... tusiwe waoga kufanya vitu pale mioyo yetu inapitutuma kuhofia kufail wala tusiwavunje wengine mioyo . Mrekebishe kwa kumwelekeza sio kumvunja moyo watu wanatoka kwa mitaji midogo hiyo hiyo ukisema mpaka usibiri ukipata 100 ndipo ufanye businesses utasubiri mpaka ustafu na hela zako utalia pombe tu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atleast kabla haujaamua kufanya uyajue haya


1. Kununua magunia (empty) 1000*100=100,000
2.Gharama ya ukusanyaji
3.Gharama ya malazi (kama si mwenyeji)
4.Gharama ya ushonaji
5.Upakiaji
6.Usafirishaji
7.Ushuru
8.Ushushaji
9.Gharama za utunzaji /Storage fee
10.Ziada/ dharura
5.9 mil,
5.4 mahindi
500,000/ usafiri.
Kupakia na kushusha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boss apo serikali haijaweka mkono wake wa vibali mara sijui ushuru... vitu kibao kidogo serikali kila gunia wanaweza kumeza 3000 au 4000 bado kupakia na kushusha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio vikwazo mkuu..
Apo tunakanusha kwa hesabu alizopiga sio sahihi... japo faida ipo ni matter ya kua na mtaji tu... lakini kwa mtaji huo na faida hiyo viko tofaut tumepinga apo tu... but mazao yana faida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bro apa unamzungumzia mtanzania wa namna gan... au unazungumzia wabunge[emoji28][emoji28]
Tuzungumzie mtanzania wa kipato cha kawaida... ata mtumishi wa umma mfano mwalim,askari n.k aliestaaf sizan kama anaweza kuwekeza 100+m

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni muhimu kulisoma soko vema ,la sivyo unaweza kulia!
 
Mwaka huu Mahindi yatakuwa ya shida zaidi kutokana na mvua kuharibu hasa waliolima October na November 2019.

Mwenye mtaji afanye hima bei ikishuka hiyo March/April kwa maeneo watakayopata vizuri!

Ila mpunga hata 36,000 kwa gunia utafika msimu huu.
Wapi panatarajiwa kuwa na mavuno mengi ya Mpunga?
 
 
Kwa mkoa wa rukwa, hasa ukanda wote kuanzia, nkasi, namanyere, laela, huwa kuna mahindi mengi sana, kuanzia mwezi wa tano, ndio huvuna gunia huanzia 25,000!!! Ni mengi sana, hadi katavi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…