Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Ujanja wa kuhifadhi mazao ili usubiri Bei ipande umepitwa na wakati. Kinacholeta faida kubwa ni kadi ya mzunguko wa mtaji na si kusubiri uuze kwa bei kubwa Mara moja baada ya kuhifadhi kwa miezi mingi.

Mfano umenunua Michele Tani 10 kwa sh 1000/= kwa kilo. Bei ya kuuza kwa jumla kwa Sasa ni sh 1300/= kwa kilo. Lakini ukisubiri kwa miezi mitano ijayo bei itakuwa sh 1,800/= kwa kilo.

Ukiuza Sasa utapata faida ya sh. 300/= x 10,000 = unapata 3,000,000/=. Halafu ndani ya mwezi mmoja unaweza kuzungusha mtaji Mara mbili hivyo kupata faida ya sh 6,000,000/= kwa mwezi. Kwa miezi minne unapata faida ya sh 24,000,000/=.

Ukiuza baada ya miezi mitano utapata faida ya sh 800/= x 10,000 hapo unapata faida ya sh 8,000,000/=.

Sasa aliyekuwa anazungusha mtaji muda wote Ana 24,000,000/= wakati aliyesubiri Bei ipande atapata 8,000,000/=. Hapo nani mjanja? Zaidi ya hayo ukifika mwezi wa tano aliyekuwa anazungusha mtaji wake unakuwa mkubwa na anaweza kuongeza mtaji kwa sh milioni kumi ili aongeze kiwango Cha manunuzi Bei ya kununulia itakapopanda. Hivyo huo mwezi wa tano bado atafanya biashara kubwa tu!

Wajanja walishaachana na ushamba wa kuweka stock kwa biashara ya nafaka!
 
Itakuwa vizuri kama hayo mazao utayaongezea thaman mfano kusaga unga wa mahindi na kuupaki hasa kwa miji nyenye uhitaji mama Dodoma.
 
Sasa hebu tupe faida wote hapa jukwaani. Bei ya mashine ya kukoboa na kusaga unga kwa mfano yenye uwezo wa kusaga Kama Tani moja kwa siku ni sh ngapi?
 
Ujanja wa kuhifadhi mazao ili usubiri Bei ipande umepitwa na wakati.
Umeongea vyema sana. Wanaotunza mazao wanakuwa na biashara zao za kuendesha maisha ya kila leo. Umiweka mazao utalipa vipi bills?.

Fanya biashara ambayo kwanza itakupa kazi/occupation pia ikuhakikishie kodi ya meza kwa mkeo kila siku. Sasa mazao na wewe umesema unataka kuacha kazi utaishi vipi ukiyaweka hiyo miezi unayosubiri bei ipande?
 
Thanks mkuu
 
Jamani Mimi ninaplani ya kufanya biashara ya mchele kwa wale was Dodoma,Arusha na moshi mchele unabei gani na ili niweze kuuza hata tani moja kwa siku mbili nianzieje!??
 
Jumla mtaji wako ilikua kama kiasi gani mkuu
 
Hizi mashine zina bei gani mkuu
 
Uko wap tuungane mkuu Mimi mwenyewe kuna uzi wangu humu nilikuwa naomba ushauri kwa wadau labda kwenu soko liko juu
 
Wap huko wananunua kilo ya mchele sh1300 mkuu
 
Bei ya ufuta ikoje kwa Sasa mjini Dar? Nna ton 3 hapa na lazma niziuze
 
B Naomba kujua bei ya kusafirisha mzigo
Kwa gunia moja la mchele kutoka mbeya hadi dar ni sh.ngapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…