mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Ujanja wa kuhifadhi mazao ili usubiri Bei ipande umepitwa na wakati. Kinacholeta faida kubwa ni kadi ya mzunguko wa mtaji na si kusubiri uuze kwa bei kubwa Mara moja baada ya kuhifadhi kwa miezi mingi.
Mfano umenunua Michele Tani 10 kwa sh 1000/= kwa kilo. Bei ya kuuza kwa jumla kwa Sasa ni sh 1300/= kwa kilo. Lakini ukisubiri kwa miezi mitano ijayo bei itakuwa sh 1,800/= kwa kilo.
Ukiuza Sasa utapata faida ya sh. 300/= x 10,000 = unapata 3,000,000/=. Halafu ndani ya mwezi mmoja unaweza kuzungusha mtaji Mara mbili hivyo kupata faida ya sh 6,000,000/= kwa mwezi. Kwa miezi minne unapata faida ya sh 24,000,000/=.
Ukiuza baada ya miezi mitano utapata faida ya sh 800/= x 10,000 hapo unapata faida ya sh 8,000,000/=.
Sasa aliyekuwa anazungusha mtaji muda wote Ana 24,000,000/= wakati aliyesubiri Bei ipande atapata 8,000,000/=. Hapo nani mjanja? Zaidi ya hayo ukifika mwezi wa tano aliyekuwa anazungusha mtaji wake unakuwa mkubwa na anaweza kuongeza mtaji kwa sh milioni kumi ili aongeze kiwango Cha manunuzi Bei ya kununulia itakapopanda. Hivyo huo mwezi wa tano bado atafanya biashara kubwa tu!
Wajanja walishaachana na ushamba wa kuweka stock kwa biashara ya nafaka!