Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Uzi mzuri sana, Niko Sumbawanga gunia LA mahindi ni 50000 kwa sasa na yanazid kupanda bei , upatikanaji wake pia ni mgumu
 
Uzi mzuri sana, Niko Sumbawanga gunia LA mahindi ni 50000 kwa sasa na yanazid kupanda bei , upatikanaji wake pia ni mgumu
Mkuu uko swax mitaa ipi? Naomba niinbox namba yako...
 
Biashara ya mpunga inalipaje ? kwa wale wazoefu na wafanya biashara ya mpunga tupeane muongozo hapo
 
Habari wanajukwaa. Mwenye ufahamu na biashara ya kusafirisha mchele kutoka Ubaruku (WIlaya ya Mbarali Mkoani Mbeya) kwenda Dodoma naomba anieleweshe hapa, kuhusu gharama na namna ya kupata malori yanayobeba mzigo.
Asanteni.
 
Habari wanajukwaa. Mwenye ufahamu na biashara ya kusafirisha mchele kutoka Ubaruku kwenda Dodoma naomba anieleweshe hapa, kuhusu gharama na namna ya kupata malori yanayobeba mzigo.
Asanteni.
Ubaruku ipo Wilaya na Mkoa gani??
 
Magari ni mengi sana toka ubaruku unasafilisha tank ngapi labda tuanzie hapo
 
Wewe upon wapi Dodoma ubaruku sio sehem ya kiwaza usafili mkuu upo mwingi chaguo lako tu kama unasafilisha tan za kutosha
 
Mpaka hapo usha mteka kwenye upande wa machine na vifungashio ili akutumie wewe kuvipata ila ukizidi 100k Mimi najua wanapo uza machine kwabei rahisi na vifungashio
 
Habari wana Jamii Forum,

Natumaini mu wazima wa afya nyote na mnaendelea na shughuli za kila siku.

Nimeleta mada hapa jukwaani tujadili kidogo kuhusiana na BIASHARA YA NAFAKA KAMA MCHELE, KARANGA, MAHARAGWE, MAHINDI kwa jumla na rejareja.

Biashara hii ipo sana akilini mwangu kwa sasa. Nahitaji msaada wenu wa mawazo jinsi ya kuanza na kuiendesha hii biashara.

Napatikana Arusha
Namba: +255767944367
 
Biashara hii nzur sana kwa kuvusha mpakani kama uko arusha ukichukua nafaka uvushe nairobi kuna faida kubwa sana. Binafsi nilijaribu kufanya kidogo vitunguu kutoa mangola na kupeleka marikiti nairobi kwakwel profit ipo ukiwa na mtaji. Sijajua target yako lakini nafaka inalipa kwa nchi za jirani maana wanategemea sana chakula kwetu
 

Nime target kufanya biashara hapahapa ndani na nje ya arusha
 
Wazo zuri biashara iko poa sana jarbu kununua maharage hasa ya njano mazuri hapo karatu au manyara maeneo kama simanjiro au mbulu au kateshi ,babati kipindi cha msimu utoe vijijini ukauzie mjini soko ni kubwa cha msingi uwe na store ila kwa mchele nadhani fanya package afu uuze kwa mama ntiliye reja reja kwa kuwafikishia kazini kwao au hotelini
 
Kwa mahindi fanya kununua kipindi cha mavuno bei ikiwa chini afu uyauze bei ikipanda maana kwa kawaida maindi hayana faida sana ila maharage ni nomah kama una mtaji afu ukayotoa bush hasa ukapeleka dar utatoboa sana cha msingi yawe manene na mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…