Okay, kama utakuwa poa biashara iko poa sana tena sana hususan kama utakuwa na uwezo wa kufuata au agiza mzigo mkubwa toka Shinyanga, Mbeya au Morogoro au Dodoma. Pia kama uko vizuri zaidi unaweza chukulia hapa mjini (Dar) na kuuza popote unapoona inafaa hata nje ya nchi kama kibali kinaruhusu.
Biashara hii iko poa huwezi jutia japokuwa mwaka huu kidogo kodi zinasumbua kwa mfano Shinyanga vijijini kodi imekuwa kubwa sana (imepanda toka 500 hadi 2000) ndani ya wiki hii halimashauri ilipochukua jukumu la kukusanya kodi yenyewe badala ya mudhabuni kitu ambacho kitapandisha bei ya mchele maradufu na kama itapanda zaidi itapunguza faida kwa mfanyabiashara ya mchele hususani yule mwenye kununua na kuuza mchele badala ya mpunga toka kwa mzalishaji.