Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Siyo kweli kabisa tuache negative attitude against women; issue hapa siyo Mani aliyefanikiwa awe mwanamke au mwanaume issue ni aina ya Biashara na mahitaji take kwa maana ya soko na jinsi MTU anavyojituma; wanaume waliofanikiwa wanatoa nini? Au wanawake walioshindwa hawakuwa na chakutoa?
Maana yangu ilikuwa ni 1 tu, afanye utafti wa kutosha.hicho unachokifikiria kuwa huwa kinawabeba is added advantage to her, lakini wewe me hiyo huna, hiyo sket inaweza kumbeba japo siyakutegemea sana.mwonekano wako unaweza kukubeba ukapata kazi flan flan kakin kutegemea mwonekano tu ni kosa kubwa.
 
Hivi kwa biashara Hii ya mchele soko lake arusha likoje? Bei ya mchele arusha ikoje?
 
Biashara ya mchele ipo hivi ndg yangu kwa sisi tuliopo huku mikoani esp km hapa mkoa mpya wa Songwe ktk wilaya ya Momba kuna vijiji wao wanalima mpunga kwa sana vijiji km Kamsamba na Chitete mpunga una mbegu zaidi ya mbili tunachokifanya huku km kipindi hiki cha mavuno tunaenda vijijin tunanunua mpunga kwa wakulima kwa debe elfu3 mpk4 kwa gunia linaingia debe10 tunakuja kuuifadhi tukija kuukoboa tunauza debe1 kuanzia elfu25mpk30 hatuleti mjini bali nyie wa mjini mnakuja kununua huku kwetu
Hilo gunia la debe kumi ni la wapi.? wacha kumuongopea mwenzio bana, izo gunia serikali imezipiga marufuku, na kwenye mizani lazima upigwe faini ukikutwa nazo, gunia halali ni debe 6. tena wamepiga marufuku kupimia zile ndoo kubwa za mozambique, sikuizi tunapimia ndoo za cola,(za rangi za kupakia nyumba) ambazo zinatoa kilo 54-58.
 
Kipi bora,kununua mchele ama mpunga?sababu utajuaje mpunga unaonunua utatoa mchele mzuri unaotaka kwa ajili ya biashara..kipi bora kwa ajilimya biashara mpunga au mchele?
Unatakiwa ujue mbegu za biashara, mfano holo5,hindia,karamata hizi ni nzuri sana kwa kuuza,na kuujua utalazimika uupukuchue ktk mikono, ukiona unavunjika mikononi jua apo sio penyewe, ni chenga izo zitakusumbua sana.
 
Idea nzuri mkuu Maana mazao ya chakula/nafaka ni basic need ya mwanadamu, so kwa biashara hii wateja watakutafuta wenyewe, tupo pamoja mm wenyewe nimemaliza udom mwezi uliopita na ndio namalizia mapumziko ya Wiki moja then nianze utafiti wa hii biashara ya nafaka. Keep it up bro
 
Mkuu,
Kabla sijatoa ushauri wangu kwako kwanza nianze kwa kukupongeza kwa WAZO ulilolipata.
Lakini pia kwa maswali ulioainisha hapo juu, kwa mtu aliyemakini tayari una majibu kwa maswali yote maana umesema tayari una jamaa zako wa karibu wanaofanya biashara hiyo na tayari wameonyesha nia ya kukubeba yaani wapo tayari kukuonyesha njia. Nitashangaa sana kwa mtu ambaye tayari anafanya biashara hiyo then hawezi kukupa majibu ya maswali uliyouliza hapo juu.

USHAURI: Mtaji ulonao ni Pesa sawa lakini kwa biashara ya mazao hiyo haitoshi na kwakuwa unayo hiyo tu nikisema nikutajie kiasi ambacho unaweza kuanza nacho na ukajisikia inafanya kazi nitakuwa kama nakukatisha tamaa hivi.

Sasa basi huo mtaji ulonao (1mil) itakulazimu ujiunge na mmoja wa hao jamaa zako ulowataja ili akubebe tu hapa nina maana kwamba mwende naye huko vijijini ambapo yeye anapata mzigo mnunue kwa maana kwamba atajulikana kwa wauzaji kuwa anayenunua ni yeye (mwenyeji wao) kumbe ndani ya mzigo kuna vigunia vyako 4-5, mkija kwenye masoko anapouza huyo jamaa yako mwachie auze yeye na baadaye anakutolea pesa yako, hapo utaona mtaji na faida yako.
Ninakupa wazo hili kutokana na ufinyu wa mtaji wako.

Kwa kufanya hivyo, utakuwa unatunisha mtaji wako, lakini pia utakuwa unapata uzoefu ktk Kazi hiyo.
Baada ya muda mtaji wako utakuwa umeongezeka, lakini pia utakuwa mzoefu ili baadaye uweze kupeperuka kwa mbawa zako.
Mtaj wa million moja mbna n mkubwa kwa mazao tu n yy kujipanga na kua na nidham na pesa.
 
Wanajamvi,habari zenu.

Naomba mwenye ujuzi kuhusu biashara ya mazao anijuze vitu kadhaa,by the way nataka nipate uelewa kidogo kuhusu biashara ya mazao hususan NAFAKA

Mimi ni mmoja kati ya wanaosubiri ajira toka serikalini baada ya kuhitimu chuo.Mpaka sasa nimeshakaa muda mrefu bila ajira ukiacha dili ndogondogo za hapa na pale,nimechoka kukaa bila kuwa na kitu maalum cha kufanya.

Nimepata wazo,na mimi nianze biashara ya mazao yaani niwe nasafiri kwenda vijijini kuchukua/kununua mazao(NAFAKA) Mfano;Ufuta,mahindi,karanga,alizeti na mpunga.

Tatizo ni kwamba sijawahi kufanya biashara yoyote ile,hivi karibuni nilizungumza na rafiki yangu mmoja ambaye yupo kijijini(DODOMA),Yeye anafanya biashara ya mpunga/mchele.ananunua huko kijijini na kuleta mjini.na kuna mjomba wangu yupo hapa mjini,yeye ana store ya mazao hususan Ufuta kwa sasa(maana ndo msimu wake),ananunua na kuuza.

Mjomba yupo tayari kuniunganisha na mtu anayeenda vijijini kununua ufuta anayemfahamu/anayemuamini niende nae vijijini akanifundishe kazi,na rafiki yangu yupo tayari niungane naye kwenye biashara ya mpunga,Wote wawili niliwauliza maswali kadhaa ambayo ningependa na nyinyi wanajamvi mchangie.(mengine sikuyauliza kabisa japo yapo hapo chini)

1,mtaji wa kuanzia wa mpunga/ufuta minimum inaweza kuwa kiasi gani?

2,Bei ya kununua mpunga/ufuta vijijini

3,gharama za usafirishaji wa mpunga/ufuta

4,vifaa vya muhimu vya kwenda navyo vijijini mfano;vifaa vya kuhifadhia/packaging kama magunia nk. na gharama zake.

5,inachukua muda gani kujaza mzigo wa pesa kama 1,000,000/= kwa mpunga/ufuta

6,faida kwa kila gunia la ufuta/mpunga

7,upatikanaji wa soko(DODOMA)

8,Bei ya kuuza kwa kila gunia la ufuta/mchele namaanisha kwa kilogram.

9,challenges/risks za biashara hii ya ufuta/mpunga

10,matakwa ya kisheria na kodi (mfano VAT) Ipoje?

11,mengineyo,ambayo sijayaorodhesha hapo juu,tafadhali

NB: Wote wawili walikuwa na uelewa juu ya debe maarufu kama "mozambique" .hili debe lipoje?,kwa nini litumike?,bei ya hlo debe ni kiasi gani? lina tofauti gani na debe la kawaida?

Natanguliza,shukurani.
Ingekua mahindi ningeungana naww kijijini kwetu mahindi bei rahisi sana !! Ila n njombe sasa njombe had dar mtaji itaishia kwenye nauli but sjajua wanaonunuaga wanapelekaga dar au WAP?
 
Wadau kwa msaada zaidi

Biashara yoyote ile inahitaji ubunifu ili kukimbizana na soko kwangu mie nilienda mbali zaid na kufungua kampuni na kufanya packaging mwenyewe ya ujazo tofauti 2kg, 5kg, 10kg kulingana na soko hivyo kuweza kusupply mpaka kwenye supermarket zetu za mjin apa.
 
Ingekua mahindi ningeungana naww kijijini kwetu mahindi bei rahisi sana !! Ila n njombe sasa njombe had dar mtaji itaishia kwenye nauli but sjajua wanaonunuaga wanapelekaga dar au WAP?
Biashara kama hizi lazima upate mtu aliye na uzoefu nazo,atakupa picha yote ipoje then utaangalia unaweza au la.
 
Ingekua mahindi ningeungana naww kijijini kwetu mahindi bei rahisi sana !! Ila n njombe sasa njombe had dar mtaji itaishia kwenye nauli but sjajua wanaonunuaga wanapelekaga dar au WAP?
Bei gani huko njombe? Kilogram Moja sh? Au debe/ndoo Moja sh? Na gunia je? Msaada Wa taarifa tafadhali. Natanguliza shukrani.
 
mtaji ninaoweza kupata hauzidi 1,000,000/=,by the way nnachotaka ni kujua hii biashara inaendeshwa vp angalau kwa muhtasar.
Huku Turiani mwezi wa saba mpaka nane waweza Pata gunia la mpunga kwa elfu 60-70, gunia ya debe nane. Kwa hiyo pesa yako bora ununue hizo gunia utakazo pata kwa mtaji wako na kukoboa mpunga. Gunia moja kama utasimamia likajazwa vizuri waweza Pata 65 - 75 kgs. Mchele ukiwa mzuri bei 1200 - 1300
 
Wadau kwa msaada zaidi

Biashara yoyote ile inahitaji ubunifu ili kukimbizana na soko kwangu mie nilienda mbali zaid na kufungua kampuni na kufanya packaging mwenyewe ya ujazo tofauti 2kg,5kg,10kg kulingana na soko hivyo kuweza kusupply mpaka kwenye supermarket zetu za mjin apa..
Tunaomba mwanga mkuu, nlikua nnawazo kama lako, unaanzia wapi?
 
Habarini wakuu, naombeni msaada kwa mwenye uzoefu, nataka nianze hii biashara ila sina baadhi ya taarifa hope wapo wenye uzoefu watanijuza, kama mlivoelezea juu hapo kuwa miezi ya mwanzo wa mwaka bei ya mahindi huwa inapanda kidogo, Taarifa kubwa ninayotaka kujua ni muda wa mavuno sababu mara nyingi bei ndio huwa inashuka, Naombeni mnijuze misimu ya mavuno au upatikanaji wa mahindi kulingana na mikoa kwa mfano kama sasa nikitaka mahindi nikachukue mkoa gani? maana nimejaribu kufuatilia bei wilaya kama ya sumbawanga naona wao mahindi yapo juu kidogo nadhani waliwahi kuvuna, nisaidieni kwenye hili jamani wenye uzoefu kwenye biashara hii. Yani kwa kifupi nataka nijue kwa kuanzia kama sahivi mkoa gani mahindi yanapatikana kwa wingi na mnijuze kila mkoa na miezi yake ya mavuno. Nitashukuru nikipata majibu ya hayo maswali yangu kwa haraka.

Natanguliza shukrani, Ahsanteni.
 
Ingekua mahindi ningeungana naww kijijini kwetu mahindi bei rahisi sana !! Ila n njombe sasa njombe had dar mtaji itaishia kwenye nauli but sjajua wanaonunuaga wanapelekaga dar au WAP?
Naomba bei ya mahindi kijijini kwenu
 
Huku Turiani mwezi wa saba mpaka nane waweza Pata gunia la mpunga kwa elfu 60-70, gunia ya debe nane. Kwa hiyo pesa yako bora ununue hizo gunia utakazo pata kwa mtaji wako na kukoboa mpunga. Gunia moja kama utasimamia likajazwa vizuri waweza Pata 65 - 75 kgs. Mchele ukiwa mzuri bei 1200 - 1300
Nice idea mkuu ila hizi biashara nimegundua ukitaka kufanya ni muhimu uwe na mtu unayefahamiana naye eneo la ununuzi hasa ukiwa mgeni katika biashara.huko inaonesha inalipa vzuri lakini kwa capital ya 1m haitoshi maana kuna gharama nyingi.
 
nice idea mkuu ila hizi biashara nimegundua ukitaka kufanya ni muhimu uwe na mtu unayefahamiana naye eneo la ununuzi hasa ukiwa mgeni katika biashara.huko inaonesha inalipa vzuri lakini kwa capital ya 1m haitoshi maana kuna gharama nyingi.
Mwaka jana nilikuwa huko kikazi, nikanunua gunia 30 @ 50,000 - 55000. Usafiri mpaka ilipo mashine nzuri ya kutoboa 3000 @ gunia. Plus also costs za unayempa kazi ya kukununulia (hapa uwe muangalifu sana kupata mtu reliable ili upate variety nzuri ya mpunga - super-, na pia ujazo usipungue debe 8). Pia mashine kuna gharama kidogo za kuanika kama haujakauka vizuri. Kila gunia nilipata between 65 - 70 kg na ulikuwa mchele mzuri sana nikauza 1300 kwa kilo.
 
Mwaka jana nilikuwa huko kikazi, nikanunua gunia 30 @ 50,000 - 55000. Usafiri mpaka ilipo mashine nzuri ya kutoboa 3000 @ gunia. Plus also costs za unayempa kazi ya kukununulia (hapa uwe muangalifu sana kupata mtu reliable ili upate variety nzuri ya mpunga - super-, na pia ujazo usipungue debe 8). Pia mashine kuna gharama kidogo za kuanika kama haujakauka vizuri. Kila gunia nilipata between 65 - 70 kg na ulikuwa mchele mzuri sana nikauza 1300 kwa kilo.
Kweli huko kuna bei nzuri sana,mimi nilienda bush moja huku dom mwez wa saba,debe lilikuwa 8,000. Nilifanikiwa kununua gunia 14 zenye ujazo wa debe saba na gunia moja lililopelea kidogo.gharama:usafiri 3500/=@gunia, ushuru 2000/=@gunia, kupakia na kushusha 800/=.bado gharama za pale mashineni;kukoboa 30/=@kilo ya mpunga(mpunga ulikuwa approximately 1500 kilograms).na gharama za kujaza mchele kwenye gunia na movement za mashineni 400/=@gunia la mchele.mchele nilikoboa zilitoka gunia 9 za kilo miamia na nusu gunia lenye kilo 45; jumla kilo 945 lakini bahati mbaya haukutoka mzuri ulitoka na chenga kosa tulilofanya ni kutoanika mpunga.niliuza mchele wangu kwa bei ya 1200/=@kilo.nilipata profit kiasi,though nilitegemea niuze 1300/= ili nipate faida niliyolenga.
 
Back
Top Bottom