Wanajamvi,habari zenu.
Naomba mwenye ujuzi kuhusu biashara ya mazao anijuze vitu kadhaa,by the way nataka nipate uelewa kidogo kuhusu biashara ya mazao hususan NAFAKA
Mimi ni mmoja kati ya wanaosubiri ajira toka serikalini baada ya kuhitimu chuo.Mpaka sasa nimeshakaa muda mrefu bila ajira ukiacha dili ndogondogo za hapa na pale,nimechoka kukaa bila kuwa na kitu maalum cha kufanya.
Nimepata wazo,na mimi nianze biashara ya mazao yaani niwe nasafiri kwenda vijijini kuchukua/kununua mazao(NAFAKA) Mfano;Ufuta,mahindi,karanga,alizeti na mpunga.
Tatizo ni kwamba sijawahi kufanya biashara yoyote ile,hivi karibuni nilizungumza na rafiki yangu mmoja ambaye yupo kijijini(DODOMA),Yeye anafanya biashara ya mpunga/mchele.ananunua huko kijijini na kuleta mjini.na kuna mjomba wangu yupo hapa mjini,yeye ana store ya mazao hususan Ufuta kwa sasa(maana ndo msimu wake),ananunua na kuuza.
Mjomba yupo tayari kuniunganisha na mtu anayeenda vijijini kununua ufuta anayemfahamu/anayemuamini niende nae vijijini akanifundishe kazi,na rafiki yangu yupo tayari niungane naye kwenye biashara ya mpunga,Wote wawili niliwauliza maswali kadhaa ambayo ningependa na nyinyi wanajamvi mchangie.(mengine sikuyauliza kabisa japo yapo hapo chini)
1,mtaji wa kuanzia wa mpunga/ufuta minimum inaweza kuwa kiasi gani?
2,Bei ya kununua mpunga/ufuta vijijini
3,gharama za usafirishaji wa mpunga/ufuta
4,vifaa vya muhimu vya kwenda navyo vijijini mfano;vifaa vya kuhifadhia/packaging kama magunia nk. na gharama zake.
5,inachukua muda gani kujaza mzigo wa pesa kama 1,000,000/= kwa mpunga/ufuta
6,faida kwa kila gunia la ufuta/mpunga
7,upatikanaji wa soko(DODOMA)
8,Bei ya kuuza kwa kila gunia la ufuta/mchele namaanisha kwa kilogram.
9,challenges/risks za biashara hii ya ufuta/mpunga
10,matakwa ya kisheria na kodi (mfano VAT) Ipoje?
11,mengineyo,ambayo sijayaorodhesha hapo juu,tafadhali
NB: Wote wawili walikuwa na uelewa juu ya debe maarufu kama "mozambique" .hili debe lipoje?,kwa nini litumike?,bei ya hlo debe ni kiasi gani? lina tofauti gani na debe la kawaida?
Natanguliza,shukurani.