Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Wakuu habari za mihangaiko ya kujipatia mkate? Wakuu ninakuja kwenu kuomba ushauri juu ya ufunguaji na uendeshaji wa duka la nafaka Dar es salaam. Nina mpango wa kufungua duka la kuuza nafaka maeneo ya tandika, Mtaji wangu ni shilingi Milioni 5. Ninaomba mwenye ufahamu wa biashara hii ya duka la nafaka anisaidie kunijuza walau mambo kadhaa juu ya biashara hii.

1) Katika kufungua biashara ya aina hii vibali vinavyotakiwa ni vipi?Kwa maana napaswa kuwa na lesseni ya TRA?inachukua mchakato upi kuipata?Vipi napaswa kuwa na kibali cha TFDA?

2) Vipi kuhusu habari ya upatikani wa bidhaa?Ninawezaje kupata suppliers wa kuwa wananiletea mzigo kutoka katika mikoa nafaka husika zinakopatikana?mfano mchele,maharagwe nk?

3) Mambo mengine muhimu ya kuzingatia juu ya biashara hii ni yapi?
 
Majuzi nikywa Ndungu, Same, kuna kilimi cha mcheke, huko na bei ni nzuri, mbona sijaona wadau wakiongelea humu, au mchele wa huko sio deal?
 
Ndugu zangu wanajamii,

Mimi nilikuwa nataka ushauri wa biashara ya duka la nafaka na mazao ya muhimu ambayo ni chakula kwa binadamu; yenye mzunguko mzuri kwa biashara.
 
mkuu nafaka zinalipa kinachotakiwa ukisha nunua kwa wakulima subiri kidogo kama mwezi 1 unakuta bei imepanda unaanza kuuza maana unakuta kuna faida
 
Wadau naomba ujuzi weno kwenye hi biashara, Je nikianza na shilingi milioni 5 itanitoa? Je kuna changamoto zipi nitarajie kukutana nazo.Binafsi napenda sana kujiajiri.Robert Kayosaki anasema kwenye kitabu chake cha poor dady & Rich dady ya kwmba a highly paid slave is still a slave.WanaJF naomba kuwakilisha Hoja.
Ila ukiweka stock mazao inalipa zaidi kama mahindi,dengu n.k
Mkuu 5m inatosha sana kwa kuanzia asa wakati wa mavuno ambako mazao hupatikana kwa wing I na bei nafuu kwa wakulima
Kwa mfano mahindi wakati wa mavuno huo ni mtaji wa fuso
Mkuu kuna msemo unasema "think big by starting small" kwa hiyo hakuna pesa isiyotosha.
 
mkuu hiyo biashara ya mpunga, si rahisi kama hivyo, mi nimeifanya sana hapo mpanda, huko kote mnyamasi, mpimbwe nimezunguka, bora hata ya mchele hesabu yake ni rahisi kidogo, lakini mpunga siku shauri kabisa.
Kiongozi kama ni mwenyeji mpanda naomba unipe directions ya maeneo nayoweza kulima zao la mpunga kwa urahisi, maeneo mazuri nayoweza kukodi heka 30 hadi 50 na kuwe na uwezekano wa kufanya irrigation incase mvua iikikata. Ntafurahi kama utanisaidia taarifa nipate pakuanzia
 
Usisumbuke kwenda mpanda nenda mbeya wilaya mpya ya momba kuna shamba zuri la umwagiliaji utapata shamba kwa 100000-150000 (kukodi) ni umwagiliaji 100% ila hakikisha unapata shamba kwenye umwagiliaji
 
Unaweza ukanunua mpunga.then ukakobolesha mwenyewe.katika machine za Ku grade alafu ukawa unasafirisha na kuuza Michele. Hiyo ndo inalipa pana gunia la mpunga utanunua sh 60,000 kukoboa gunia 3,500. Kwa mpunga mkubwa litatoa kilo 70-72.hivyo kama una mtaji Wa laki sita utapata gunia 10,ambazo ukikoboa..utapata kilo 700-720 kwa kilo utauza sh 2000, hivyo utakuwa na income ya sh.1,400,000. Karbu Morogoro.
 
Unaweza ukanunua mpunga.then ukakobolesha mwenyewe.katika machine za Ku grade alafu ukawa unasafirisha na kuuza Michele...iyo ndo inalipa...pana gunia la mpunga utanunua sh 60,000 kukoboa gunia 3,500. Kwa mpunga mkubwa litatoa kilo 70-72.hivyo kama una mtaji Wa laki sita utapata gunia 10,ambazo ukikoboa..utapata kilo 700-720...kwa kilo utauza sh 2000,,hivyo utakuwa na income ya sh.1,400,000..karbu morogoro.
Nakuja man nipe namba yako MP
 
Back
Top Bottom