Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

AHSANTE KWA FURSA HII. NAHITAJI WADAU WA MAZAO YAFUATAYO

1. KOROSHO ZILIZOBANGULIWA
2. SOYA YA NJANO FUPI
3. SOYA YA ZAMBARAU
4. UFUTA
5. MAHARAGWE MEUPE
 
Bhbm,
Kwa mimi nakushauri kama huko vizuri ni heri ukajiingiza kwenye kilimo cha maharage,naongea hivyo sababu nina experience nayo japo kidogo,ni bidhaa inayowekeka lakini kwa kiasi kidogo unaweza pata pesa nyingi na haiumizi sana kichwa ukizijua basics,mimi ndio namalizia kupiga (kuchambua) niliyopanda mwezi wa nne ntaleta mrejesho hapa kiasi nilichopata kwa heka,unaweza kujifunza zaidi hapa,thanks.
 
Wanajamvi hope wote mu wazima wa afya njema.

Nataka kufànya biashara ya mazao hasa mahindi na nafaka zingine; lakini kwa kuanzia nataka nianze na mahindi kwanza halafu mtaji ukikua nitaongeza wigo wa mazao mengine.

Ninaomba mnisaidie namna ya kupata mazao huko mikoani ni njia gani zinazotumika ili kuweza kufanikisha kupata mzigo ndani ya muda mfupi na kuuleta Dar?

Pia naomba mnijuze mikoa au wilaya ambazo naweza pata mahindi mengi kwa bei nzuri na ambapo kuna mazao au mahindi ya kutosha ili ukusanyaji uwe wa haraka.

Kuhusu soko kwa hapa Dsm hakuna tatizo kwani nimepata mteja ambaye atachukua. ni mteja wa uhakika kwa hivyo kwa upande wa soko sina tatizo.

Tatizo ni huko mikoani ndio sijui nianzie wapi nimalizie kwa suala zima la ukusanyaji na upatikanaji wa mahindi.

Mtaji wa kuanzia ni 10m nataka kuanza mara moja biashara hii kwa anayejua naomba anisaidie kunielekeza sehemu au mikoa ambayo naweza pata mahindi na pia mbinu za ukusanyaji sbb mi ndio naanza na sio mwenyeji wa biashara hii nahitaji kupata uzoefu kwa wanaofanya au waliokwishakufanya au wanaofahamu.

Thanks in advance
Ulifikia wapi mkuu
 
Usisumbuke kwenda mpanda nenda mbeya wilaya mpya ya momba kuna shamba zuri la umwagiliaji utapata shamba kwa 100000-150000 (kukodi) ni umwagiliaji 100% ila hakikisha unapata shamba kwenye umwagiliaji
Lina ukubwa gani momba sehemu gani?
 
Habari wadau,

Kwa sasa niko Mbeya mjini hivyo nimeona kuna fursa naweza ifanya nataka ninunue mchele Mbeya mjini then niutume Dar kwa ajili ya kwenda kuuzwa.

Hivyo wadau wenye uzoezi na biashara hii wanisaidie kunijuza yafuatayo:

1. Ni wapi naweza pata mchele kwa bei nafuu kwa hapa Mbeya mjini(nimeajiriwa hivyo kwenda nje ya hapa mjini itakuwa vigumu).

2. Njia ya usafiri (nafuu) nitakayotumia kuusafirisha kwenda Dar.

Ni hayo tu.
Tumia treni mkuu TAZARA
Kama ulishindwa kuyauza mwezi january hadi april umeumia..sasa hivi mahindi dar es salaam ni tsh 780/=
 
Mimi ni mlimaji wa mahindi na pia ninategemea kuwa mzalishaji wa kati wa bidhaa za mahindi. Niko Dodoma na nnazifahamu ABC za biashara ya mahindi hapa.Tuwasiliane
Weka no sasa mkuu
Mkuu biashara ya mpunga ni nzuri ukiifanyia timing!
Mimi nina nunua mpunga napiga stoo!
Halafu mwezi dec - March unaukoboa unauza mchele faida x150%!

kama unaipenda, fanya. hakuna chuo cha uzoefu bali unakuja kutokana na kufanya kazi. kujifunza ni muhimu kwa kila hatua. tafuta taarifa za masoko mara kwa mara/kila siku. kujikwaa na kuanguka kupo but taarifa sahihi zitakuokoa
 
Unaweza ukanunua mpunga.then ukakobolesha mwenyewe.katika machine za Ku grade alafu ukawa unasafirisha na kuuza Michele...iyo ndo inalipa...pana gunia la mpunga utanunua sh 60,000 kukoboa gunia 3,500. Kwa mpunga mkubwa litatoa kilo 70-72.hivyo kama una mtaji Wa laki sita utapata gunia 10,ambazo ukikoboa..utapata kilo 700-720...kwa kilo utauza sh 2000,,hivyo utakuwa na income ya sh.1,400,000..karbu morogoro.
Upo mjini ama Ifakara?
 
Habari zenu wakuu

Mimi nina mahindi kilo 441 nauza. Kilo moja shilingi 1000/=. Nipo Kimara Dar. Mimi nayatoa Songea. Ila sihitaji udalali. Njoo na cash tufanye biashara.
Mkuu nqmaindi Songea nauza kilo 800 kama ukihitaji nalima mwenyewe
 
Ila ukiweka stock mazao inalipa zaidi kama mahindi,dengu n.k

Mkuu 5m inatosha sana kwa kuanzia asa wakati wa mavuno ambako mazao hupatikana kwa wing I na bei nafuu kwa wakulima. Kwa mfano mahindi wakati wa mavuno huo ni mtaji wa fuso

Mkuu kuna msemo unasema "think big by starting small" kwa hiyo hakuna pesa isiyotosha.
you killed it big up
 
Back
Top Bottom