Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia

Mkuu uko wapi kwa sasa biashara ya mazao inatakiwa uende na msimu ...kwa sasa ni msimu wa maharage ya ukanda wa mbulu kwa watu wa Arusha wanaelewa ..kununua na kuweka stoo ni kamari bei inaweza kushuka kuliko hata uliyonunulia pia inafanywa na watu wenye mitaji mikubwa

Wajanja wa mazao wanaenda na msimu pia unaweza ukaweka stoke ikakutana na msimu mwingine hapo tayari umeingia cha kike.kama uko pande za Arusha tembelea mbauda kupata maelekezo zaidi
Unatusaidia na wengine mkuu mwaga Nondo hapa tufaidike sote kaka.
 
Wandugu poleni na mihangaiko ya kila siku hususani katika kipindi hiki cha janga la Corona.

Moja kwa moja nije kwenye mada, mwaka jana nilijikita sana kwenye biashara ya zao la mpunga yaani nilikuwa nalima na kununua ila biashara inakua ngumu kidogo kulingana na bei inayokuwa sokoni kwa muda huo...
Unaweza kujiunga na earmoney ambayo itakusaidia kuingiza kipato wakati huu wa karantini tembelea link ifuatayo kujiunga
Viewing payed advertising sites eenmoney.xyz - Welcome!
 
Wandugu poleni na mihangaiko ya kila siku hususani katika kipindi hiki cha janga la Corona.

Moja kwa moja nije kwenye mada, mwaka jana nilijikita sana kwenye biashara ya zao la mpunga yaani nilikuwa nalima na kununua ila biashara inakua ngumu kidogo kulingana na bei inayokuwa sokoni kwa muda huo...
Ni biashara nzuri na inaweza ikakuinua ila ni lazima utafute zao ambalo utalimudu kwa mtaji wako na network uliyo nayo.Ikiwa hutaki kuweka stock na kusubiri bei ipande basi unataka jambo la kwanza uwe na soko la uhakika (usitegemee madalali wa Dar).

Jambo la pili ni lazima uwe na team ya watu unaowaamini wa kukukusanyia mzigo (Watanzania wengi sio waaminifu hata waliopo vijijini-uwe tayari kupigwa kidogo).

Jambo la tatu ujue sheria na kanuni zinazoendana na biashara hii.Unaweza kukusanya mzigo gari ikazuiwa na Halmashauri ya kijiji.Unaweza pia kuwatembelea watou Kama Mo Dewji kwa mazao kama kunde,mbaazi na mengineyo.
 
Ni biashara nzuri na inaweza ikakuinua ila ni lazima utafute zao ambalo utalimudu kwa mtaji wako na network uliyo nayo.Ikiwa hutaki kuweka stock na kusubiri bei ipande basi unataka jambo la kwanza uwe na soko la uhakika (usitegemee madalali wa Dar)...
Brother umeongea point sana hasa hiyo ya soko. Maana unaweza nunua mzigo mwingi halafu hujui umuuzie nani? Dah imenipa kigugumizi sana hiyo.

Mimi nataka kufanya hii biashara nimepanga kutumia 20M sasa soko sijui. Wajuvi wa masoko ya biashara ya mahindi ama maharage njooni muokoe jahazi huku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wandugu poleni na mihangaiko ya kila siku hususani katika kipindi hiki cha janga la Corona.

Moja kwa moja nije kwenye mada, mwaka jana nilijikita sana kwenye biashara ya zao la mpunga yaani nilikuwa nalima na kununua ila biashara inakua ngumu kidogo kulingana na bei inayokuwa sokoni kwa muda huo...
Njoo pm mkuu tuyajenge. Ninatafuta ajira hiyo, niko kijijini. Usalama wa pesa zako ni 100%. Utaamua wewe aina ya mkataba wa kazi.
 
BIASHARA YA STOCK YA MAHINDI. nachangia katika mada hii kama mkulima ambae nimekulia shambani na niliwahi fanya kwa kuweka stock ya mahindi, niseme tu kwamba mara nyingi kwa aliye makini anaeza pata faida. japo inaweza rudisha mtaji wako, ikakupatia faida kidogo sana, au faida ikawa double au triple ya mtaji wako. mambo ya msingi:

1. Inahitaji ufuatiliaji wa karibu sana.

2. Dawa ni lazima kuweka ukitumia mifuko ya kawaida. hapa kwenye dawa unahitajika umakini mwingine mkubwa kwanzia kwenye kununua dawa na upuliziaji wake maana kuna dawa fake siku hizi.

3. msimu mzuri wa kununua ni kipindi mkulima anavuna. mfano saivi ukienda kwa mkulima moja kwa moja mikoa ya rukwa mkulima atakuuzia 30,000/= hadi 42,000/=. kipindi cha mwezi january =february yalikuwa yanauzwa 90,000/= hadi 108,000/=
 
Mahindi yaneza banguliwa pindi yamewekwa stock japo nasikia wanasema wadudu wanaobangua ukiwanyima hewa hawezi kuishi kabisa hvyo wataalamu wakaja na mifuko ambayo haipitishi hewa, ukitumia mifuko hiyo huna haja ya dawa
 
Bhbm,

Mkuu mimi c pingani na wewe but nataka kukushauri jambo moja,

- katika swala zima la biashara ya nafaka ni bora ukajikita katika ku ad value au kuongeza thamani ya hizo nafaka.

1. Ni bora ukawa na ofisi yako mjini na jaribu kuyaongezea thamani hayo mazo kama vile kugred na kupark kabisa. Hapo utakuwa umeongeza thamani na utauza kwa bei ya juu, na unaweza tafuta hata supermaket tano tu za kuwa sambazia...
Kampuni gani hiyo ya kenya mkuu?
 
Mkuu "Chasha Poultry Farm" nimekuwa nikifatilia comments zako nyingi kwenye threads tofauti kwa kweli una mitazamo ya tofauti, kisomi na kimapinduzi zaidi kwenye tasnia nzima ya ujasiriamili na biashara Tanzania, binafsi nimekuwa insipired sana na miongozo yako mbalimbali, Mungu akubariki.

Value addition is very important in every things we do as entrepreneur and business men, watanzania umefika wakati tutoke kwenye mbinu za ujima za kibiashara. Mkuu big up sana...
Kuwa supplier ni vizuri sana Ila wengi wamedhulumiwa mnooooo kuwa makini wengine mzigo unapeleka vizuri kwenye kulipana Sasa ndo kimbembe.

Au unapeleka mzigo wa mil5 badala upewe yote unapewa nusu au inachelewa maana biashara inatakiwa izunguke vinginevyo[emoji3525]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana jamii forurm naombeni ushauri

Mimi nimfanyakazi wa kuajiriwa kwenye moja ya makampuni ya Cement nchini Tanzania....

Kwa sasa nimechoka na kazi nataka kujiari..

Nawazo la karibu ni kufanya biashara ya kununua mazao ya nafaka kotoka mashambani na kupeleka sokoni

Mazao mfano wa ...
Mahindi ukizingatia huu ndio msimu
Mpunga
Maharagwe
Ulezi
Ngano
Nk
Je kwa mtaji wa 20m itanitoa...pia naomba kujua changamoto zake...
 
Biashara ya nafaka kwa wewe mwenye mtaji mkubwa,nibora kuwa na ghala la kuifadhi mazoa,unawalangua wakulima kupindi cha mavuno alafu unayaifadhi vuzuri unasubiri mda soko likiwa juu ndio unaanza kuuza utaona faida itakavyokuja mara 3.

Changamoto ni gharama za kuifadhi nafaka,nyingine kuyumba kwa soko la nafaka huwa unaeza kuifadhi maindi mda bei ikapanda ukichelewa ukiwa mzito kwenye maamuzi yanaeza kushuka ghafla ukapata hasara
 
Asante sana mkuu
 
Mkuu nakushauri usifanye biashara ya mazao sababu ni biashara ya msimu na wewe unahitaji kuendesha maisha.

Nakushauri kwa mtaji huo fanya biashara ya kuongeza thamani ya mazao na kupata bidhaa ya mwisho mfano maize flour packaging au mafuta ya alizeti yaliyosindikwa.

Kama upo mkoa wowote anzisha mashine ya kusaga na kusindika unga wa mahindi iwe dona au sembe. Kwa mtaji huo utapata mashine nzuri (ukihitaji nione),kifungashio na utabaki na mtaji wa kununua mahindi.

Utakoboa na kusaga mahindi vizuri kutengeneza unga mzuri wenye ubora na utauza madukani huky ukifurahia faida ya unga na pumba.
Kila la kheri boss
 
Back
Top Bottom