Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwenye TV naona umepiga hesabu Expensive Sana.Kitambulisho muhimu nalifahamu hilo, thanks kwa kunikumbusha pia.
Kuhusu TV ndugu ntaanza na moja mbeleni ntaongeza nyingine kadiri ya mapato yatakavyo kuwa.
Asante Tena.
Mawazo mazuri mkuu, generator liwe na mafuta ya kutosha tayari kwa ajili ya dharura.Nyongeza, angalia wenzio wana vitu gani then wewe boresha uwe zaidi yao.
Jitahidi mafuta yawemo muda wote kwenye jenereta kama itatokea umeme kukatika unawasha haraka .
kabla ya mechi hakika jenereta linakuwa nje tayari ili umeme ukikatika unawasha chap kwa haraka.
usiweke viti vya plastic utakula hasara kubwa sana.
Mkuu usisahu kitambulisho cha mjasilimali kama uwekezaji wako hauzidi 4M.
NB: kwa Tv moja huwezi kufanikiwa, chukulia kwa mfano
15:00 Nyumbu vs Arsenal
15:00 Chelsea vs Spurs
utaweka ipi na utaacha ipi?
Nipo Arusha ndugu kwa sasaDSTV ni 99,000 mkuu. Mimi staff ingawa nipo ZANZIBAR.
Kisha wewe upo wapi?
Asante kwa ushauri kaka, ni wazo zuri kwa kuwa na TV Inch 65 ulinunua sehemu gani?Sijui km huko vijijini wapo wengine wanaonyesha mpira ila kiukweli ukipata inch 65 utakuwa umepiga hatua kubwa. Mi nakumbuka nilinunua inch 65 kwa Samsung kwa 1.5m.yaani hata watu wawe wengi kiasi gani na kwa ukubwa gani inchi, 65 ni kiboko
Sijui km huko vijijini wapo wengine wanaonyesha mpira ila kiukweli ukipata inch 65 utakuwa umepiga hatua kubwa. Mi nakumbuka nilinunua inch 65 kwa Samsung kwa 1.5m.yaani hata watu wawe wengi kiasi gani na kwa ukubwa gani inchi, 65 ni kiboko
Kama jana , game 2 kubwa zilikuwa muda mmoja, Simba vs Azam huku Man City Vs Tottenham.Write your reply...TV inatakiwe ziwe mbili kwa kuanzia.
Ulinunua feki
Samsung 65" kwa 1.5
Asante kwa kuzidi kunikumbusha. Umeongea mambo ya msingi mkuu.Vitu muhimu vya kuwa navyo flatscreen kuanzia inch 43 uwe nazo kuanzia mbili vinga'muzi vya Dstv unatakiwa uwe navyo viwili kimoja kinaunganishwa mfumo wa extra view vinga'muzi vya azam navyo viwe viwili kwa ajili ya mechi za ligi kuu tanzania bara na mechi za klabu bingwa afrika,mapinduzi na mechi zingine n.k pia usisahau startimes kwa ajili ya mechi za europa league upande wa banda linatakiwa liwe banda kubwa la kutosha lenye mabenchi na ikiwezekana ufunge feni chini unaweza ukawawekea turubai wateja wakakaa usisahau Generator ili kupambana na kero za umeme
Canal ndo nini mkuu? Naomba nieleweshe hapoNikuuzie canal mkuu hutojuta bei ni 130 unalipia 45 jwa mwezi, ligi 5View attachment 1184976
Hiyo bei umeongeza sana jomba nasikia sio kivile halafu mwambie ni french mpiraCanal ndo nini mkuu? Naomba nieleweshe hapo
Hii canal unalipiaje? Niliambiwa natakiwa niwe na mtu Kigoma atakayevuka kwenda Burundi ili kunilipia.Nikuuzie canal mkuu hutojuta bei ni 130 unalipia 45 jwa mwezi, ligi 5View attachment 1184976
Achana nayo itakupotezea muda unatafuta kutapeliwa nunua dstv ufanye kazi kwa uhakikaHii canal unalipiaje? Niliambiwa natakiwa niwe na mtu Kigoma atakayevuka kwenda Burundi ili kunilipia.
Biashara yakuonyesha mpira inalipa kama itakuwa karibu na maeneo haya.Fata ushauri huu.nipo kwenye game msimu wa tatu huu ila hakuna faida kubwa labda icheze simba Vs yanga kila weekend
huko vijijini EPL hakuna wadau wengi wanachagua game zao ..hicho kingilio cha 500 utakuwa unacheza tu
Kaka upo vzuri asante kwa kutupa nondo za kuongeza kipato zaidi.Biashara yakuonyesha mpira inalipa kama itakuwa karibu na maeneo haya.
1 chuo
2 shule za boarding
3 vituo vya magari hasa dalala na parking za magari makubwa.
4 Mijini sehemu yoyote yenye kusanyiko kubwa la vijana.
Vijijini watu wanafuatilia ligi ya Tanzania tu na mechi za mashindano kama AFCON EURO na World cup.
Kama anataka kuweka vijijini simshauri kupeleka supersport labda ajiridhishe hapo anapopeleka anauhakika walau wa watu hamsini kila mechi wanaweza ingia kuangalia EPL.
faida atakuwa anaipata kunapokuwa na mechi kubwa kubwa kwani zina mashabiki wengi maeneo mengi.
Siku ya simba na yanga anapandisha kiingilio kuwa 1000 watu wataingia wengi bila kujali kiingilio na atapata faida.
Kuna huduma ya cable. Unakuta mtu ana ungo anawaunganisha nyinyi ambao hamna ungo sasa mwenye ungo ana canal + mi nikataka niwe na ungo wangu mwenyewe ndiyo akanipa majibu hayo.Achana nayo itakupotezea muda unatafuta kutapeliwa nunua dstv ufanye kazi kwa uhakika