Biashara ya Kusafirisha Mazao Nje ya Nchi: Jifunze Utaratibu wa Kufuata, Changamoto, Faida na Uzoefu wa Wengine

Kaka mchele at a Kenya unazingua?
 
Hvi ni wpi naweza kupata kama nafaka zifuatazo zinaruhusiwa kuingia kenya. 1 mchele 2 alizeti ambayo haijakamuliwa.
 
Mwanzoni mwa safari ya Ujasirimali ndo hivyo ilivyo.

Safari inapoa anza majukumu yote ni ya mtu mmoja.
  • Dereva yeye
  • store keeper yeye
  • Meneja yeye
  • Sales manager yeye
  • Marketing Manager yeye
  • Security officer yeye
  • Director yeye
  • Oparational.manager yeye

Hizi zote mwanzo wa safari hufanywa na mtu mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu, nimesoma hizi posts kwa furaha sana nikijua kuwa nitakapofikia post ya mwisho kutakuwa na suluhisho la kuendelea. Lakini post zimeishia na malalamiko tuu. Hatujasogea mbele. Hatujasaidia watoto wetu ambao watakuwa taifa la kesho.

Hii ni dhambi. Hatujafanikiwa kutoa mwafaka; je tufanyeje?. Whatsapp group ingeundwa, tukutane siku moja sehemu na tujadili the way forward pamoja na kualika raisi wetu au viongozi watusikilize na kutekeleza way forward.

Thereafter tusaidiane mawazo na kusafirisha mazao nchi gani nasisi tujikwamue huu umasikini. Ssurely masoko yapo na tukipata baraka kutoka juu hata mabenki watatufata tuuu. Let's be a Tanzania without malalamiko but looking for next way forward.
 
Hivi walishindwa kujua kwamba ungepeleka hayo mazao nchi ingepata fedha ya kigheni na uchumi ungekuwa.Wakati mwingine wafanyakazi sio wote wa serikali wanachukulia mambo kirahisi rahisi tu.''Awana business mindset'' sijui kwanini mitazamo ya baadhi ya wafanyakazi wa umma ni tofauti kabisa na mitazamo ya mfanyakazi wa sekta binafsi au mjasiriamalli, wao kupata mshahara na marupuru na mda wa kuingia na kutoka ndio wanauthamini,kuona umuhimu wa kusaidia jambo lisonge mbele awana kabisa baadhi yao.
 
Natamani kweli baadi ya wafanyakazi wa serikali wabadili mitazamo yao, mfanya biashara anapofanya biashara iwe ndani au nje ya nchi,nchi inapata kodi na fedha za kigeni,urasimu na ukwamishaji avisaidi,yapaswa wajue pia wafanyabiashara na wajasiriamali wanalipa kodi na wao wanapata mishahara na huduma nyingine,bila sekta binafsi au sekta binafsi ikifa wao awatapata wa kuwahudumia,na sekta binafsi ndio zimenyanyua uchumi wa nchi nyingi.Tubadilike tufanye kazi kila mtu katika nafasi yake kama nchi za kipato cha kati na kipato cha juu,tuache kufanya kama bado ndio tumepata uhuru tunahitaji kusaidiwa.
 
Huu uzi ulikuwa mzuri sana lakini hakuna hitimisho lililofanyika kurahisisha usafirishaji wa mazao nje ya nchi. Kama kuna mtu alifanikiwa tafadhali atueleze ni hatua zipi alipitia.
 
Tanzania hawajui Export inachochea ukuaji wa Uchumi kwa haraka sana mimi huwa naponunua baadhi ya bidhaa SA naenda kufata kibali Pretoria, Sunnyside pale jamaa hawana complication zozote utaudumiwa mpaka utafurahi unaweza ukadhani kuna malipo kumbe ni buree kabisa na kama kuna kitu hauna wao ndio wanawasiliana na hao jamaa walete hizo documents ili wao wakikupa ahadi yao ya siku tatu ni asubuhi kwenda kuchukua kibali hakuna maelezo tena.
 
Huwa natamani wizara husika zikawa na majibu haya kwenye mitandao. Halafu wapo wapo tu

Post #9 kamaliza yote na sisi ndio nchi pekee ambayo haijui kula na watu

Kuna wakati unakuta matunda yetu ulaya halafu nembo ya South Africa au Kenya na hayo yanapita kwa magumashi mpaka nchi jirani halafu wana pack vizuri na kubandika nembo zao.

Hivi hatujui kwamba tunapoteza mapato mengi na pia kukosa hela za kigeni?

Kahawa yetu na avocados na vitu vingi vinapitishwa kila kukicha kwenda jirani na unaona kwenye masoko ya Ulaya na Uarabuni.

Nimenyanyua mikono kwa mijadala isiyokuwa na majibu kwa kweli.

Na wabunge wapo lakini akili imezima kabisa wanasikiliza muungurumo wa shangingi tu na kusubiri posho

Wake up guys and smell the coffee

Sent from my SM using Tapatalk
 
Kusafirisha chakula au matunda ni rahisi kama ABC kwa wenzetu na hata ulaya bidhaa nyingi hazina ushuru kabisa yaani 0%
Sasa machungwa yanaozea barabarani wakati tuna kila kitu.

Sent from my SM using Tapatalk.
 

Yaani katika suala la export ya chakula ni pasua kichwa. Mimi nimepata deal ya kusafirisha nyama ya mbuzi. Kuna vibali lukuki, vingine vinapatikana Dodoma na vingine Dsm ingawa vingiweza kupatikana sehemu moja ni pasua kichwa kweli kweli. Ukienda pale wizarani kuna wazee wapo wapo na wanakatisha tamaa kabisa, manake nao wamejichokea tu. Sasa naelekea kukwama huku naona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…