Biashara ya Kusafirisha Mazao Nje ya Nchi: Jifunze Utaratibu wa Kufuata, Changamoto, Faida na Uzoefu wa Wengine

Biashara ya Kusafirisha Mazao Nje ya Nchi: Jifunze Utaratibu wa Kufuata, Changamoto, Faida na Uzoefu wa Wengine

Mchele peleka zanzibar una bei ya afadhali,ku export mchele kaka utapata kifaduro.kuna mchele wa pakistan umenyooka! Bei yake inaweza hata kufika nusu ya mchele wa kwetu katika soko la dunia,tatizo wenzetu wanapewa ruzuku na serikali ndio maana bei zao ni za chini sana sokoni kulinganisha na za kwetu
Kaka mchele at a Kenya unazingua?
 
Hvi ni wpi naweza kupata kama nafaka zifuatazo zinaruhusiwa kuingia kenya. 1 mchele 2 alizeti ambayo haijakamuliwa.
 
Halafu niwafundishe jambo. Vijana mnaoingia katika shughuli za kilimo kinachowaghalimu kufanikiwa katika kilimo ni tabia ya kuplay roles zaidi ya moja mtu moja huyo huyo. Wewe ni mkulima kazi yako ni kulima mazao ya standard inayotakiwa basi.

Sasa unakuta mtu mkulima yeye, msafirishaji yeye, mtu wa masoko yeye, bwana shamba yeye, dalali yeye, manager yeye, store keeper yy sasa mwisho wa siku akipiga mavuno mara moja tu kurudia tena hataki hata kusikia anaaacha. Tunakuwa tunafanya kilimo cha kujaribu.
Mwanzoni mwa safari ya Ujasirimali ndo hivyo ilivyo.

Safari inapoa anza majukumu yote ni ya mtu mmoja.
  • Dereva yeye
  • store keeper yeye
  • Meneja yeye
  • Sales manager yeye
  • Marketing Manager yeye
  • Security officer yeye
  • Director yeye
  • Oparational.manager yeye

Hizi zote mwanzo wa safari hufanywa na mtu mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu, nimesoma hizi posts kwa furaha sana nikijua kuwa nitakapofikia post ya mwisho kutakuwa na suluhisho la kuendelea. Lakini post zimeishia na malalamiko tuu. Hatujasogea mbele. Hatujasaidia watoto wetu ambao watakuwa taifa la kesho.

Hii ni dhambi. Hatujafanikiwa kutoa mwafaka; je tufanyeje?. Whatsapp group ingeundwa, tukutane siku moja sehemu na tujadili the way forward pamoja na kualika raisi wetu au viongozi watusikilize na kutekeleza way forward.

Thereafter tusaidiane mawazo na kusafirisha mazao nchi gani nasisi tujikwamue huu umasikini. Ssurely masoko yapo na tukipata baraka kutoka juu hata mabenki watatufata tuuu. Let's be a Tanzania without malalamiko but looking for next way forward.
 
Changamoto yake kubwa ni urasimu wa Serikali
Nilipata Dili flani la kupeleka Mzigo Mwingi tu Commoro nikakusanya Nguvu za Jamaa zangu Kama wawili tukakusanya Mtaji wetu mdogo tu Kama 20 Million.

Tukashauriwa Tufuate Vibali halali

Tu kaanza kuelekezwa tuanze board of external Trade, huko ikapigwa Danadana twende Chamber of Commerce kule wakatueleza kazi yao ni kutoa Vibali tu tukitaka kujua kitu gani kinaruhusiwa kipi hakiruhusiwi twende Wizara ya Mifugo au Kilimo ndio wenye orodha ya Mazao yanayoruhusiwa kusafirishwa Nje ya Nchi!

Niliwauliza wale Watu wa Chamber of commerce pale Kwny Barabara ya Morogoro na Samora ( PPF House) kwanini hiyo orodha ya vitu vinavyoruhusiwa kwanini wasikae nayo pale kupunguza Urasimu Jibu wanatoa huo ndio utaratibu 'Mzee usilete Ujuaji fuata taratibu'

Tulipofika Wizara ya Kilimo ndio balaaa Urasimu mpaka tukaamue tusafirishe kienyeji
Hivi walishindwa kujua kwamba ungepeleka hayo mazao nchi ingepata fedha ya kigheni na uchumi ungekuwa.Wakati mwingine wafanyakazi sio wote wa serikali wanachukulia mambo kirahisi rahisi tu.''Awana business mindset'' sijui kwanini mitazamo ya baadhi ya wafanyakazi wa umma ni tofauti kabisa na mitazamo ya mfanyakazi wa sekta binafsi au mjasiriamalli, wao kupata mshahara na marupuru na mda wa kuingia na kutoka ndio wanauthamini,kuona umuhimu wa kusaidia jambo lisonge mbele awana kabisa baadhi yao.
 
Natamani kweli baadi ya wafanyakazi wa serikali wabadili mitazamo yao, mfanya biashara anapofanya biashara iwe ndani au nje ya nchi,nchi inapata kodi na fedha za kigeni,urasimu na ukwamishaji avisaidi,yapaswa wajue pia wafanyabiashara na wajasiriamali wanalipa kodi na wao wanapata mishahara na huduma nyingine,bila sekta binafsi au sekta binafsi ikifa wao awatapata wa kuwahudumia,na sekta binafsi ndio zimenyanyua uchumi wa nchi nyingi.Tubadilike tufanye kazi kila mtu katika nafasi yake kama nchi za kipato cha kati na kipato cha juu,tuache kufanya kama bado ndio tumepata uhuru tunahitaji kusaidiwa.
 
Huu uzi ulikuwa mzuri sana lakini hakuna hitimisho lililofanyika kurahisisha usafirishaji wa mazao nje ya nchi. Kama kuna mtu alifanikiwa tafadhali atueleze ni hatua zipi alipitia.
 
Tanzania hawajui Export inachochea ukuaji wa Uchumi kwa haraka sana mimi huwa naponunua baadhi ya bidhaa SA naenda kufata kibali Pretoria, Sunnyside pale jamaa hawana complication zozote utaudumiwa mpaka utafurahi unaweza ukadhani kuna malipo kumbe ni buree kabisa na kama kuna kitu hauna wao ndio wanawasiliana na hao jamaa walete hizo documents ili wao wakikupa ahadi yao ya siku tatu ni asubuhi kwenda kuchukua kibali hakuna maelezo tena.
 
Huwa natamani wizara husika zikawa na majibu haya kwenye mitandao. Halafu wapo wapo tu

Post #9 kamaliza yote na sisi ndio nchi pekee ambayo haijui kula na watu

Kuna wakati unakuta matunda yetu ulaya halafu nembo ya South Africa au Kenya na hayo yanapita kwa magumashi mpaka nchi jirani halafu wana pack vizuri na kubandika nembo zao.

Hivi hatujui kwamba tunapoteza mapato mengi na pia kukosa hela za kigeni?

Kahawa yetu na avocados na vitu vingi vinapitishwa kila kukicha kwenda jirani na unaona kwenye masoko ya Ulaya na Uarabuni.

Nimenyanyua mikono kwa mijadala isiyokuwa na majibu kwa kweli.

Na wabunge wapo lakini akili imezima kabisa wanasikiliza muungurumo wa shangingi tu na kusubiri posho

Wake up guys and smell the coffee

Sent from my SM using Tapatalk
 
Uzi mzuri sana huu. Big up mleta mada kwa kuanzisha mjadala huu. Ku-export mazao, nchi hii ni urasimu tu ndicho kinachowakwamisha wengi. Ubabaishaji mwingi kwenye office za Serikali. Maofisa hawajuwi hata majukumu yao kama mdau alivyochangia hapo juu.

Nadhani kuna haja ya kulipigia kelele suala hili, kwamba kuwe na taasisi MOJA tu ambayo ihusike na utoaji wa vibali na clearance zote kwa mtu anayetaka kuexport bidhaa nje ya nchi.

Mie natafuta mzoefu wa biashara hii ya mazao awe 'mentor' wangu... anipe A to Z jinsi ya kufanya & kuexcel kwenye biashara ya nafaka/mazao kwa soko la hapa hapa nchini.

-Kaveli-
Kusafirisha chakula au matunda ni rahisi kama ABC kwa wenzetu na hata ulaya bidhaa nyingi hazina ushuru kabisa yaani 0%
Sasa machungwa yanaozea barabarani wakati tuna kila kitu.

Sent from my SM using Tapatalk.
 
Changamoto yake kubwa ni urasimu wa Serikali
Nilipata Dili flani la kupeleka Mzigo Mwingi tu Commoro nikakusanya Nguvu za Jamaa zangu Kama wawili tukakusanya Mtaji wetu mdogo tu Kama 20 Million.

Tukashauriwa Tufuate Vibali halali

Tu kaanza kuelekezwa tuanze board of external Trade, huko ikapigwa Danadana twende Chamber of Commerce kule wakatueleza kazi yao ni kutoa Vibali tu tukitaka kujua kitu gani kinaruhusiwa kipi hakiruhusiwi twende Wizara ya Mifugo au Kilimo ndio wenye orodha ya Mazao yanayoruhusiwa kusafirishwa Nje ya Nchi!

Niliwauliza wale Watu wa Chamber of commerce pale Kwny Barabara ya Morogoro na Samora ( PPF House) kwanini hiyo orodha ya vitu vinavyoruhusiwa kwanini wasikae nayo pale kupunguza Urasimu Jibu wanatoa huo ndio utaratibu 'Mzee usilete Ujuaji fuata taratibu'

Tulipofika Wizara ya Kilimo ndio balaaa Urasimu mpaka tukaamue tusafirishe kienyeji

Yaani katika suala la export ya chakula ni pasua kichwa. Mimi nimepata deal ya kusafirisha nyama ya mbuzi. Kuna vibali lukuki, vingine vinapatikana Dodoma na vingine Dsm ingawa vingiweza kupatikana sehemu moja ni pasua kichwa kweli kweli. Ukienda pale wizarani kuna wazee wapo wapo na wanakatisha tamaa kabisa, manake nao wamejichokea tu. Sasa naelekea kukwama huku naona.
 
Back
Top Bottom