Biashara ya Kusafirisha Mazao Nje ya Nchi: Jifunze Utaratibu wa Kufuata, Changamoto, Faida na Uzoefu wa Wengine

Eti Nchi ya Viwanda!

Board of External Trade kazi Yao ni kuleta Vipeperushi na kuvisambaza Sabasaba nothing more.

Utaratibu wa ku Export ni urasimu kuliko wa Ku Import wakati Exports ndio huchochea ukuaji wa Uchumi kuliko Import!
Umesema kweli kabisa! Export inachochea ukuaji wa uchumi haraka.

Inaleta pesa za kigeni. Lakini, mamlaka husika wala hicho sio kipaumbele chao.

Sijui ni nini..! Labda tunalaana au tuliisha ikosea mizimu ya mababu!
 
Yaani huu ndo urasimu, kiasi (tani) vipi kama nini sema ntakuwa na export ufuta tani 2 ila soko likakuwa nikapata mteja mwngine inamaana natakiwa nianze kufatilia tena kibali badala ya kukusanya mzigo serekali ijiangalia kwa hili.
Urasimu huu ndo unatufanya kuonekana mazoba hata katika soko la Afrika Mashariki.

Biashara ni ushindani, wewe unapeleka barua Dodoma kwa katibu mkuu. Huyo mteja atasubiri kweli ufanye maigizo yako yupo tu! Ujinga ulopitiliza.
 
Watu wenye mitaji mikinwa mikubwa wanafanya sana hii biashara. I think hata MO anafanya hizi biashara, so tukiwapata waliofanya kwa muda mrefu wanaweza kutuonesha njia kwa sababu comments karibu zote zinaziongelea changamoto.

Ila biashara hii ni nzuri kwa sababu nje kuna uhitaji wa mazao ya kilimo.
 
UZOEFU WANGU: ADUI MKUBWA WA MKULIMA TANZANIA NI SERIKALI

Wakati ule wa kauli mbiu ya Kilimo Kwanza nilidhani sasa Tanzania "itapasua" Lakini duuu, ikawa ni mtindo wa kuuwa kilimo kabisa: pembejeo fake, mbolea fake, mbegu fake, vipawa tila (sisi huku kwetu tunaviita vipapatilo) fake, mapanga na majembe fake, mabomba ya kupuliza dawa fake, dawa za ngombe fake, dawa za kuku fake, mkulima akifika sokoni Dar es salaam au Arusha au Mwanza anakutana na dalali fake. Kila kitu, kila kitu, fake. Hivyo basi tukamua kuita yale ma vx v8 kilimo kwanza maana Serikali kweli ilituangusha sisi wapenda kilimo.

Lakini kila zao tunalolima lina soko la uhakika hapa hapa nchini. Kwa soko la nje huna haja ya kuanza kwenda sijui Saudi Arabi, Comoro au hata Ulaya au Marekani. Kwa kuanza Kenya tu hapo ni soko tosha. Lakini ukitaka kuuza mazo Kenya ujizatiti kweli kweli. Sijui unaweka machungwa yako kwenye "Fuso tandam" halafu unakwenda kutafuta soko Nairobi utarudi na kilio. Hivyo kwa kuanza hatuna haja ya kwenda huko wenyewe kuuza mazoo yetu kwani kuna matapeli kweli kweli. Wao wanakuja hapa wananunua kila kitu na kwa bei yeyote. Huku kwetu Handeni Wakenya wakivamia soko la mnada wa mbuzi ni balaa. Wananunua kwa bei ya kufa mtu. Hivyo hatuna haja ya kwenda Vingunguti tunawasubiri Wakenya, wakija tunawapiga kweli kweli.

Lakini adui mkubwa wa mkulima Tanzania ni Serikali. In this country there is no "proper" well established regulatory mechanism kwa mazao yote, hata yale ya pamba na Kahawa (angalia sheria ya sasa ya Bodi ya Kahawa na ile ya Bodi ya Pamba ndo utajua nasema kitu gani), vituo vya utafiti wa kilimo vimekufa, kila kitu katika kilimo ni holela (wanasema let market forces play). Ukilima mungu akajalia neema ukapata mpunga mwingi Serikali inatoa vibali kwa wafanyibiashara kuingiza mchele wa plastiki ambao unauzwa kwa bei ya kutupwa. Kufanya biashara ya kuuza mazao nje ya nchi ni sawa kutaka kusafirisha cocaine nje ya nchi. Ni kazi kweli kweli.

Mimi sijui tufanye nini? Kazi mijini hakuna. Vijana wana shahada zao mwaka wa nne sasa wanatafuta kazi. Hakuna kazi. Kwa mazingira tuliyo nayo kilimo hakimvutii msomi hata kidogo. Wapo wachache wanaojaribu, lakini wanakutana na mazingira magumu kweli. Lakini tuna ardhi kubwa sana na tunajisifu 25% ya ardhi yetu ni "protected areas" tumewaachia tembo, fisi na nyoka waishi humo na bado ardhi kubwa imebaki. Ule mto Ruvu, Mto Rufiji, mto Wami, Mto Pangani mvua ikinyeesha maji yote yanakwenda baharini. Ulaya na Marekani wameendelea kwa kuishi kando kando ya mito. Sisi mabonde ya mito tunayakimbia.

Kweli kuna potential kubwa, tena kubwa sana katika kuuza mazao nje ya nchi. Serikali jamani muione hii na muifanyie kazi. Hivyo viwanda vitapata wapi malighafi? Au mnataka assembiling factories kwa vile Tanzania kuna cheap labor?
 
Watu wenye mitaji mikinwa mikubwa wanafanya sana hii biashara. I think hata MO anafanya hizi biashara, so tukiwapata waliofanya kwa muda mrefu wanaweza kutuonesha njia kwa sababu comments karibu zote zinaziongelea changamoto.
Ila biashara hii ni nzuri kwa sababu nje kuna uhitaji wa mazao ya kilimo
Mo ana bahati ya kupata monopoly channel
 
Changamoto yake kubwa ni urasimu wa Serikali
Nilipata Dili flani la kupeleka Mzigo Mwingi tu Commoro nikakusanya Nguvu za Jamaa zangu Kama wawili tukakusanya Mtaji wetu mdogo tu Kama 20 Million.

Tukashauriwa Tufuate Vibali halali

Tu kaanza kuelekezwa tuanze board of external Trade, huko ikapigwa Danadana twende Chamber of Commerce kule wakatueleza kazi yao ni kutoa Vibali tu tukitaka kujua kitu gani kinaruhusiwa kipi hakiruhusiwi twende Wizara ya Mifugo au Kilimo ndio wenye orodha ya Mazao yanayoruhusiwa kusafirishwa Nje ya Nchi!

Niliwauliza wale Watu wa Chamber of commerce pale Kwny Barabara ya Morogoro na Samora ( PPF House) kwanini hiyo orodha ya vitu vinavyoruhusiwa kwanini wasikae nayo pale kupunguza Urasimu Jibu wanatoa huo ndio utaratibu 'Mzee usilete Ujuaji fuata taratibu'

Tulipofika Wizara ya Kilimo ndio balaaa Urasimu mpaka tukaamue tusafirishe kienyeji
Urasimu Wa serikali ndio chanzo cha njia za panya.hongeleni nchi ya viwanda
 
Wakati ule wa kauli mbiu ya Kilimo Kwanza nilidhani sasa Tanzania "itapasua" Lakini duuu, ikawa ni mtindo wa kuuwa kilimo kabisa: pembejeo fake, mbolea fake, mbegu fake, vipawa tila (sisi huku kwetu tunaviita vipapatilo) fake, mapanga na majembe fake, mabomba ya kupuliza dawa fake, dawa za ngombe fake, dawa za kuku fake, mkulima akifika sokoni Dar es salaam au Arusha au Mwanza anakutana na dalali fake. Kila kitu, kila kitu, fake. Hivyo basi tukamua kuita yale ma vx v8 kilimo kwanza maana Serikali kweli ilituangusha sisi wapenda kilimo.

Lakini kila zao tunalolima lina soko la uhakika hapa hapa nchini. Kwa soko la nje huna haja ya kuanza kwenda sijui Saudi Arabi, Comoro au hata Ulaya au Marekani. Kwa kuanza Kenya tu hapo ni soko tosha. Lakini ukitaka kuuza mazo Kenya ujizatiti kweli kweli. Sijui unaweka machungwa yako kwenye "Fuso tandam" halafu unakwenda kutafuta soko Nairobi utarudi na kilio. Hivyo kwa kuanza hatuna haja ya kwenda huko wenyewe kuuza mazoo yetu kwani kuna matapeli kweli kweli. Wao wanakuja hapa wananunua kila kitu na kwa bei yeyote. Huku kwetu Handeni Wakenya wakivamia soko la mnada wa mbuzi ni balaa. Wananunua kwa bei ya kufa mtu. Hivyo hatuna haja ya kwenda Vingunguti tunawasubiri Wakenya, wakija tunawapiga kweli kweli.

Lakini adui mkubwa wa mkulima Tanzania ni Serikali. In this country there is no "proper" well established regulatory mechanism kwa mazao yote, hata yale ya pamba na Kahawa (angalia sheria ya sasa ya Bodi ya Kahawa na ile ya Bodi ya Pamba ndo utajua nasema kitu gani), vituo vya utafiti wa kilimo vimekufa, kila kitu katika kilimo ni holela (wanasema let market forces play). Ukilima mungu akajalia neema ukapata mpunga mwingi Serikali inatoa vibali kwa wafanyibiashara kuingiza mchele wa plastiki ambao unauzwa kwa bei ya kutupwa. Kufanya biashara ya kuuza mazao nje ya nchi ni sawa kutaka kusafirisha cocaine nje ya nchi. Ni kazi kweli kweli.

Mimi sijui tufanye nini? Kazi mijini hakuna. Vijana wana shahada zao mwaka wa nne sasa wanatafuta kazi. Hakuna kazi. Kwa mazingira tuliyo nayo kilimo hakimvutii msomi hata kidogo. Wapo wachache wanaojaribu, lakini wanakutana na mazingira magumu kweli. Lakini tuna ardhi kubwa sana na tunajisifu 25% ya ardhi yetu ni "protected areas" tumewaachia tembo, fisi na nyoka waishi humo na bado ardhi kubwa imebaki. Ule mto Ruvu, Mto Rufiji, mto Wami, Mto Pangani mvua ikinyeesha maji yote yanakwenda baharini. Ulaya na Marekani wameendelea kwa kuishi kando kando ya mito. Sisi mabonde ya mito tunayakimbia.

Kweli kuna potential kubwa, tena kubwa sana katika kuuza mazao nje ya nchi. Serikali jamani muione hii na muifanyie kazi. Hivyo viwanda vitapata wapi malighafi? Au mnataka assembiling factories kwa vile Tanzania kuna cheap labor?
Mkuu kama viongozi wenyewe ambao ndio wanapanga huo urasimu wa kila kitu wanatakiwa kujua kusoma na kuandika tu unategemea nini!? Matokeo yake ndio kama haya tuko nyuma kwa kila kitu. Tutaendelea kuota Tanzania ya viwanda mpaka dunia inafika mwisho.
 
Tabu ya kazi za kupeana na kujuana mwisho wa siku mtu siyo sahihi anaweka kwenye kitengo nyeti na bange zake ndiyo hizo.
 
Changamoto yake kubwa ni urasimu wa Serikali
Nilipata Dili flani la kupeleka Mzigo Mwingi tu Commoro nikakusanya Nguvu za Jamaa zangu Kama wawili tukakusanya Mtaji wetu mdogo tu Kama 20 Million.

Tukashauriwa Tufuate Vibali halali

Tu kaanza kuelekezwa tuanze board of external Trade, huko ikapigwa Danadana twende Chamber of Commerce kule wakatueleza kazi yao ni kutoa Vibali tu tukitaka kujua kitu gani kinaruhusiwa kipi hakiruhusiwi twende Wizara ya Mifugo au Kilimo ndio wenye orodha ya Mazao yanayoruhusiwa kusafirishwa Nje ya Nchi!

Niliwauliza wale Watu wa Chamber of commerce pale Kwny Barabara ya Morogoro na Samora ( PPF House) kwanini hiyo orodha ya vitu vinavyoruhusiwa kwanini wasikae nayo pale kupunguza Urasimu Jibu wanatoa huo ndio utaratibu 'Mzee usilete Ujuaji fuata taratibu'

Tulipofika Wizara ya Kilimo ndio balaaa Urasimu mpaka tukaamue tusafirishe kienyeji
Sasa baada ya hapo ikawaje
 
Ndugu, ninakubaliana na wewe kwa asilimia zote. URASIMU. Mimi nilipata tenda ya kupeleka chakula cha mifugo hapa jirani tu, Kenya.

Kwa "ujinga" wangu nilitaka kurasimisha shughuli yangu kwa kufuata taratibu zote husika, wizara ya kilimo na mifugo aliyenipokea nadhani hajui hata kilichomuweka hapo, nikarushwa niende TFDA. Huko nako, wakaanza kunishangaa tu kama vile nimepotea njia. Hawajui kama wanahusika na biashara yangu. Nikarushwa niende TRA. Huko nako wakasema nipate kwanza kibali toka wizara ya kilimo na mifugo, pamoja na TFDA.

Nikaanza zoezi upya kupitia hizo office. Hakuna nilichoambulia, zaidi ya dharau kutoka kwa watumishi wa serikali.

Kwa vile mzigo ulikuwa tayari mteja ameshalipia na kutuma lori kwa ajili ya uchukuzi, tulipakia mzigo na kumwachia dereva afanye maalifa yake mzigo ufike. Hatukuwa na namna, maana mamlaka zote husika ni kama vile hawajui kwamba biashara ya nje kwa maana ya export inaleta pesa za kigeni kwa taifa.

Hapa bado kunatatizo kubwa sana! Sijui nani ataweza kutusaidia angalau kuwe na mamlaka moja inashughulika na biashara ya nje, ambapo unaweza kupata vibali na taratibu zote husika ukitaka kufanya hiyo biashara.
Halafu huko kwenye hivi viofisi vya uma kumejaa wajinga sana. Yaani nchi ina mambo mengi ya kijinga sana. Saa nyingine mtu unaona bora ukawekeze Rwanda maana kule pamoja na udikteta wa Kagame hawana ujinga ujinga kwenye biashara
 
Huu ndio urasimu tunaoongelea

Ukiangalia Sharti no. 4 na namba 8 utajua kabisa si Sharti la Kibiashara!

Inaonekana Kibali kinachotolewa sio cha biashara ni cha kuvusha Mazao wao wanaita cha Biashara!

Nitaje aina ya Zao na kiwango ninachotaka kusafirishwa Ina maana nikishapata kibali cha Machungwa nikapewa taarifa kuwa soko la Machungwa lime change lete Mananasi maana yake nikaombe kibali upya? Tunaanda sera na taratibu kijamaa kwny soko huria

Ukitaka kupeleka Mzigo Mara ya pili unaandika report then unaomba Tena kibali [emoji12][emoji12][emoji12] hii sio Biashara BAKITA watohoe jina
Hii misheria yao ya enzi za ujima bado wanayo halafu wapuuzi wa TRA wakikukamata eti unakwepa kodi!!! Ndo maana watu wanaona bora watoe rushwa tu, ujinga ujinga mwingiii. Inakera sana
 
Ukitaka kufanikiwa Biashara Basi kubali kupambana na TRA, ukitii Sheria Na Taratibu za TRA 100% jiandae Mali zako kupigwa Mnada na Bank Kama ulikopa
 
tatizo mnaolalama wengi huwa hamfanyi chochote . Utasikia malalamiko ya kuhusu ugumu wa kufanya biashara yanatolewa na mtu ambaye kaajiriwa hata biashara hajui ni kitu gani. Ndo JF hiyo.
Ungenijua wala usingenitathimini hivyo; sijawai kuaajiliwa au kufanyakazi ya kibarua toka nizaliwe njoo kwenye changamoto za biashara ili ubebe uhusika ujue ulasimi wa tahasisi za kiserekali.
 
Back
Top Bottom