Wakati ule wa kauli mbiu ya Kilimo Kwanza nilidhani sasa Tanzania "itapasua" Lakini duuu, ikawa ni mtindo wa kuuwa kilimo kabisa: pembejeo fake, mbolea fake, mbegu fake, vipawa tila (sisi huku kwetu tunaviita vipapatilo) fake, mapanga na majembe fake, mabomba ya kupuliza dawa fake, dawa za ngombe fake, dawa za kuku fake, mkulima akifika sokoni Dar es salaam au Arusha au Mwanza anakutana na dalali fake. Kila kitu, kila kitu, fake. Hivyo basi tukamua kuita yale ma vx v8 kilimo kwanza maana Serikali kweli ilituangusha sisi wapenda kilimo.
Lakini kila zao tunalolima lina soko la uhakika hapa hapa nchini. Kwa soko la nje huna haja ya kuanza kwenda sijui Saudi Arabi, Comoro au hata Ulaya au Marekani. Kwa kuanza Kenya tu hapo ni soko tosha. Lakini ukitaka kuuza mazo Kenya ujizatiti kweli kweli. Sijui unaweka machungwa yako kwenye "Fuso tandam" halafu unakwenda kutafuta soko Nairobi utarudi na kilio. Hivyo kwa kuanza hatuna haja ya kwenda huko wenyewe kuuza mazoo yetu kwani kuna matapeli kweli kweli. Wao wanakuja hapa wananunua kila kitu na kwa bei yeyote. Huku kwetu Handeni Wakenya wakivamia soko la mnada wa mbuzi ni balaa. Wananunua kwa bei ya kufa mtu. Hivyo hatuna haja ya kwenda Vingunguti tunawasubiri Wakenya, wakija tunawapiga kweli kweli.
Lakini adui mkubwa wa mkulima Tanzania ni Serikali. In this country there is no "proper" well established regulatory mechanism kwa mazao yote, hata yale ya pamba na Kahawa (angalia sheria ya sasa ya Bodi ya Kahawa na ile ya Bodi ya Pamba ndo utajua nasema kitu gani), vituo vya utafiti wa kilimo vimekufa, kila kitu katika kilimo ni holela (wanasema let market forces play). Ukilima mungu akajalia neema ukapata mpunga mwingi Serikali inatoa vibali kwa wafanyibiashara kuingiza mchele wa plastiki ambao unauzwa kwa bei ya kutupwa. Kufanya biashara ya kuuza mazao nje ya nchi ni sawa kutaka kusafirisha cocaine nje ya nchi. Ni kazi kweli kweli.
Mimi sijui tufanye nini? Kazi mijini hakuna. Vijana wana shahada zao mwaka wa nne sasa wanatafuta kazi. Hakuna kazi. Kwa mazingira tuliyo nayo kilimo hakimvutii msomi hata kidogo. Wapo wachache wanaojaribu, lakini wanakutana na mazingira magumu kweli. Lakini tuna ardhi kubwa sana na tunajisifu 25% ya ardhi yetu ni "protected areas" tumewaachia tembo, fisi na nyoka waishi humo na bado ardhi kubwa imebaki. Ule mto Ruvu, Mto Rufiji, mto Wami, Mto Pangani mvua ikinyeesha maji yote yanakwenda baharini. Ulaya na Marekani wameendelea kwa kuishi kando kando ya mito. Sisi mabonde ya mito tunayakimbia.
Kweli kuna potential kubwa, tena kubwa sana katika kuuza mazao nje ya nchi. Serikali jamani muione hii na muifanyie kazi. Hivyo viwanda vitapata wapi malighafi? Au mnataka assembiling factories kwa vile Tanzania kuna cheap labor?