Biashara ya Kusaga na Kukoboa: Uzoefu wangu wa miezi 15

Biashara ya Kusaga na Kukoboa: Uzoefu wangu wa miezi 15

Unit 1 ya umeme inakulipa sh 1,000; yaani inaleta faida ya 1,000 - 357= 643
Swala la faida itategemeana na eneo ulilopo kwa huku nilipo unit moja ya umeme itakulipa faida ya kuanzia Tsh 1500-2000 kwa kutegemea na mzigo unao usaga, eg, ukisaga unga wa mahindi tu 1unit itatoa 1500 lla kama utasaga unga wa mhogo, 1unit Itatoa mpaka 2500
 
Hongera sana mdau, hapo segera ndio kwetu, wasalimie michungwani na kiziwa ndago.
siku nikija nitakuja kukusalimia.
 
Nataka kufanya Blanding na Packing!
Tafuta brand yako, gharama kama sikosei ni 150,000,
Then tafuta mwenye stock ya Mahindi, anaehitaji kukobolewa na kutumia brand yako,,
Utamcharge 7000,kukoboa, kusaga na kupack kwenye mifuko, kila junia moja la mahindi,,
Hapo umeme juu yako, vibarua, kila kitu,, yeye atalipa 7000 kwa kila junia la mahindi,
 
Asante sana kwa wazo zuri
 
Swala la faida itategemeana na eneo ulilopo kwa huku nilipo unit moja ya umeme itakulipa faida ya kuanzia Tsh 1500-2000 kwa kutegemea na mzigo unao usaga, eg, ukisaga unga wa mahindi tu 1unit itatoa 1500 lla kama utasaga unga wa mhogo, 1unit Itatoa mpaka 2500
Ni wapi huko kiongozi?
 
Ndugu zangu, mwaka jana July 2021 nilinunua mashine ya kusaga na kukoboa na kuifunga Tanga mwezi wa Septemba, 2021.

Mchanganuo wa Vifaa:-

1. Mashine ya Kusaga

Kinu size 75 - 1,200,000
Mortor 30hp - 1,300,000
Starter(On/Off)- 300,000
Pulleys 2 - 100,000
Mikanda 3 - 15,000

2. Kinu cha Kukoboa

Kinu rollers 3 - 1,200,000
Mortor 30hp - 1,300,000
Pulleys 2 - 100,000
Switch - 300,000
Mikanda 3 - 45,000

Vifaa vingine vya umeme:-
1. Main Switch 3Phase - 190,000
2. Socket braker 100A- 60,000
3. Wires, taa, earthrod,clamps, switches - 150,000

Vifaa vya usimikaji mashine
1. Channel/Chasis cha chini (2)- 250,000
2. Cement mifuko 2 - 29,000
3. Mchanga ndoo 30 - 15,000
4. Guta la Kokoto - 30,000
5. Usafiri Guta ( 2,3&4) - 10,000

Ufundi:-
1. Umeme - 200,000
2. Ujenzi/Mechanical - kufitisha vinu chini - 150,000

Gharama ya kufunga umeme 3 phase (jumla) - 1,200,000

Kodi ya frame - 50,000 kwa mwezi.

Ikumbukwe, umeme wa 10,000 unapata units 28.

MAPATO:
(Ukiwa huna mahindi)
Umeme wa 10,0000 = units 28= 28*1,000 = 28,000/=
(Faida 28,000-10,000=18,000)

Umeme wa 100,000, faida 180,000
etc etc.

Kwa kipindi cha miezi 15 niliyofanya kazi, nimetumia units 12,500 sawa na mapato ya sh 12,500,000/=

Hizi ni bei halisi na nimehusika fully mwenyewe kila hatua ya mradi huu mpaka sasa.

USHAURI:

Ukitaka kufungua mashine za kusaga na kukoboa, tafuta mtaji hata wa gunia 5 za kuanzia, maana wateja huenda mashine yenye mahindi, hivyo utauza MAHINDI, PUMBA na UNITS ZA UMEME kwa haraka.

Ikumbukwe, gunia 1 linatoa debe 3 za pumba, na kila debe ni 4, 000 ( bei ya sasa 2022 November)

Sina mtaji wa mahindi. Mahindi naletewa na watu/wateja, mm kwangu faida ni units za umeme zinavyopukutika.

Biashara sijaisajili, sina leseni bado.

Naombeni wazo la namna ya kuweza kukopesheka.
Thread yangu Bora ya December 2022
 
1. Uhaba/ukosefu wa mahindi kutokana na ukame

2. Kukatika kwa umeme mara kwa mara
1.Vipi kuhusu ubora wa mahindi?
2.Gunia moja la kilo 100 kwa wastani linatoa unga kilo kiasi gani?
3.Je ubora wa mahindi unaweza kuamua kiasi cha unga au pumba unachopata?
 
Unit 1 ya umeme inaingiza 1,000. Bei ya kununua unit 1 ni 357.

Maana yake unit 1 faida yake ni 643!
Nadhani wengi wanauliza hiki kipengele kwa sababu umeweka gharama za umeme pekee ilihali kiuhalisia lazima kutakuwa na gharama nyinginezo...hivyo hiyo faida ya 643 unayoisemea itakuwa chini.
 
Nataka kufanya Blanding na Packing!
Achana kabisa na mambo ya mikopo. Jikusanye mdogomdogo tu kisha utapanua mtaji wako. Kuwa mvumilivu. Mambo mazuri huchukua muda kidogo..

Najua unaweza kuwa na shauku ya kutaka sana kukopa na ukaachana na huu ushauri tunaokupa wa kutokopa, ila iwapo Roho wa Mungu atakutembelea ukakubaliana na ushauri wa kutokopa, itakuwa kheri sana kwako.
 
Umeme ndio unaua biashara za watu na kuongeza umaskini kwenye jamii, watu wanajituma lakini serikali yenye monopoly ya umeme ndio shida zote zinaanzia hapo,hii serikali is a big let down na ndio chanzo cha umaskini nchini, pumbaf sana
 
Nadhani wengi wanauliza hiki kipengele kwa sababu umeweka gharama za umeme pekee ilihali kiuhalisia lazima kutakuwa na gharama nyinginezo...hivyo hiyo faida ya 643 unayoisemea itakuwa chini.
Muongozo kama huu:
 
Back
Top Bottom