Biashara ya Kusaga na Kukoboa: Uzoefu wangu wa miezi 15

1. Uhaba/ukosefu wa mahindi kutokana na ukame

2. Kukatika kwa umeme mara kwa mara
Hatujapishana. Changamoto kubwa kwangu ni ukosefu wa mahindi kutokana na ukame. Napambana nipate mahindi ya kutosha mwaka huu kuondoa hiyo changamoto.

Nimefunga na mashine ya kusaga ya diesel kupambana na shida ya umeme. Kama upo vizuri mfukoni, funga na ya diesel ya kusaga, italipa in a long run
 
Hizo ndiyo mada nzuri kwa vijana kuchangia na kupata mawazo Chanya, sio Kila muda kuwaza ngono tu.

Kuna mwenye uzoefu na mashine za Dizeli kuhusu faida? Kwa changamoto hii ya Umeme iliyopo nafikiria kufunga mashine ya kutumia Mafuta/Dizeli
Funga hiyo mashine ina faida nzuri sana.
-Zingatia service ya oil
-Uwe na fundi mmoja wa kurekebisha ikiharibika
-ukubwa wa kinu uendane na wingi wa wateja
-Kuwa karibu na mashine ili uweze kupata kujua kwa lita ina uwezo wa kusaga kiasi gani na inaweza kuingiza sh ngapi
-Manunuzi ya mafuta fanya mwenyewe. Usikubali mfanyakazi wako anaehudumia wateja, huyohuyo akanunue mafuta yakiisha. UTAIBIWA
-Usikubali mafuta yaishe kabisa ndo ukanunue. Utawapa nafasi ya wateja kuanza kuongea ongea. Weka stoke ya kutosha ya mafuta. Itapunguza gharama za usafiri za kwenda kununua mafuta kila wakati.
 
Asante
 
Shukrani Mkuu, nitafanyia kazi
 
643x12,500=8,037,500.
Hii ni faida kabla ya kutoa gharama nyengine.
Kuna
1. Kodi ya frame
2. Leseni
3. Mfanyakazi
4. Kodi ya mapato
5. Etc
 
Umeme ndio unaua biashara za watu na kuongeza umaskini kwenye jamii, watu wanajituma lakini serikali yenye monopoly ya umeme ndio shida zote zinaanzia hapo,hii serikali is a big let down na ndio chanzo cha umaskini nchini, pumbaf sana
Umeongea point ya msingi sana, serikali inapaswa kujua umeme ni miongoni mwa mahitaji ya msingi kwa watu. Hizo pesa inazoweka kkwenye halmashauri eti kukopesha watu kwa makundi ambazo ki msingi zinaliwa tu basi ingehakikisha inasambaza umeme kwenye kila kitongoji na kila mtaa, ingehakikisha kila mtazania anapata umeme, jambo hili lingeweza kuinua watu wengi sana ki uchumi kuliko serikali inavyo fikiria. Niliwahi kutaka kufanya biashara hii sehemu lakini TANESCO sitaacha kuwalaani kwa kuninyima umeme.
 
Naomba unitafute unipe uzoefu!!
0626063600
 
Hii project ntakuja kuifanya ukiwa na mashine ya kusanga na kukoboa mahindi na mpunga ,ukawa na project ya kufuga nguruwe ili utumie pumba za mahindi na mpunga kutoka mashineni kwako lazima utoboe kimaisha
 
0626063600 naomba unitafute bosi
 
Nimeishajenga jengo Ila bado sakafu kwa chini
Nimenunua mota 25 HP
Kinu kusaga no 75
Bado Cha kukoboa
Bado tanesco wanataka 1200000
Naomba unitafute 0626063600
 
Inaitaji service nyingi sana
Service nyingi inategemea na matunzo yako kiongozi. Ila baada ya miaka minne au mitano kutokana na matumizi yake, itahitaji major service.

Ukiachana na kubadili oil. Lazima uzingatie maji ya kupoozea engine, diesel safi, filter ya diesel iwe inasafishwa, filter ya oil iwe inasafishwa, pump ya oil iwe inakaguliwa walau mara moja kwa mwaka
 
Hii project ntakuja kuifanya ukiwa na mashine ya kusanga na kukoboa mahindi na mpunga ,ukawa na project ya kufuga nguruwe ili utumie pumba za mahindi na mpunga kutoka mashineni kwako lazima utoboe kimaisha
Kabisaaa[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…