Biashara ya kutengeneza na kuuza "Askrimu" (Ice Lollies)

Biashara ya kutengeneza na kuuza "Askrimu" (Ice Lollies)

Vifungashio ni vya Aina gani,, na unatengeneza ice cream zile zinazouzwa in form of cone au ni zipi hizo zako
 
Pia unafanyia biashara mkoa gani na namna ya uuzaji wako ni unazungusha mitaani ama unauza vipi.
 
Gharama unazotaaja ni sahihi kabisa ila faida unayosema si kweli maana biashara ina up and down kwahiyo hapo soma nzuri zaidi ni namna ya kuulinda huo mtaji Mdogo wa iceream.
 
Gharama unazotaaja ni sahihi kabisa ila faida unayosema si kweli maana biashara ina up and down kwahiyo hapo soma nzuri zaidi ni namna ya kuulinda huo mtaji Mdogo wa iceream.
My friend, ndo maana nikasema inatemegea na ubunifu wako. Icecream hizo hizo kwa gharama hiyo hiyo ya raw materials mwingine atauza 100 mwingine 200/300. Pia usafi na jinsi gani unatanua soko lako. Kikubwa biashara itoke kwa wakati. Hata biashara ya genge mwingine ataona anayeuza genge hapati faida ila mwingine anasomesha kwasababu ya genge hilohilo. Kikubwa ni kuamua na kua focused. Mimi nawatia moyo mmnaohisi mnaweza kufanya hii kitu inalipa ukiichukulia silias.
 
Vifungashio ni vya Aina gani,, na unatengeneza ice cream zile zinazouzwa in form of cone au ni zipi hizo zako
Mie nipo Dar - Tabata. Vifungashio natumia vya vifuko na vya aina ya vijikombe nanunua k/koo soko dogo kuna maduka ndani yanauza bidhaa zote za icecream, lakini mtu anaweza tumia vifungashio vinavyompa urahisi wa upatikanaji swala tu wateja wako wavielewe si lazima utumie kama navyotumia mie.
 
Pia unafanyia biashara mkoa gani na namna ya uuzaji wako ni unazungusha mitaani ama unauza vipi
Kwasababu nimefanyakazi kubwa kutangaza bidhaa yangu ipo baadhi ya mikutano ikiwa inafanyika naitwa nipeleke na hii ndio hunipa faida haswa maana nawapelekea kwa 300. Kuna wateja wangu spesho wanaweka oda kua wanahitaj kiasi gani,pia nimetafuta masoko maeneo tofaut tofaut napeleka madukani and nina kijana anapeleka shule moja ya sekondari ..hakikisha unatafuta soko eneo ambalo linamkusanyiko wa watu pia ichukulie silias. Usiichukulie kama ni biashara ambayo wateja wako watakua watoto tu tena kwa mia mia, big no!
 
Hello friends,
Naomba nijibu maswali yenu hapa. Kama nilivosema mwanzo kuna aina nyingi za icecream ila pendwa sana ni za maziwa ..mie hutengeneza za maziwa na za ubuyu. nianze na za maziwa.

MAHITAJI
1. Maziwa ya unga
2. Sukari
3. Maji
4. Ladha (vanila)
5. Rangi ya chakula ( mie hutumia yellow)
6. Kilainishi(optional)
7. Vifungashio
sasa hapa unakua na vipimo vyako mwenyewe mfano kwa mahitaji ya icecream 70 za maziwa

1. Maji lita tano( yalochemshwa au weka water guard kurahisisha)
2. Maziwa ya unga robo kilo (tsh 3250)
3. Sukari robo kilo (tsh 650)
4. Ladha ya vanila (tsh1,000) hii utatumia vifuniko viwili tu au vitatu vya kichupa.
5 Kilainishi(tsh 500) kijiko kimoja cha chakula changanya material yako hayo namba moja hadi nne. Kisha weka rangi yako (tsh 100 tu) kidogo tu. Baada ya hapo kilainishi unakiweka kwenye blenda unachanganya maji nusu kikombe ule uji wake weka kwenye mchanganyiko wako. Congratulations bidhaa yako ipo tayari funga ktk vifungashio (tsh 500) vyako kisha weka kwa fridge yako tayari kupokea pesa.
Mahitaji 3250+1000+650+500+500+100 =600

Mapato 70@200 =14,000
14,000-6,000= 8,000
Net profit 6,000
Mahitaji kama ladha ,rangi,vifungashio na kilainishi utatumia hadi mara 5 bila kununua tena
imagn unaweza kuuza icecream 100 tu kwa siku 100 x200=20,000 kwa siku mara siku 30 sawa na 600,000 kwa mwezi toa gharama za uendeshaji unacheza kwenye laki nne. Fikiria sasa kutanuà soko lako ...ni zaidi ya mshahara wa degree holder. Ubuyu ndo cheaper zaidi ...oh i love this biz nakushawishi ufikirie. Mkihitaji ya ubuyu nitaelekeza pia
Hapo kwenye ladha huwezi weka ladha tofauti na vanilla?
 
unaweza ..mimi hupendelea tu hiyo vanila
Mkuu kama hautojali elezea kuhusu hii ya Ubuyu,na pia umeonesha ingredients zinazotumika but nimeangalia YouTube naona wanatumia Sana Sana vitu vinaitwa" pure cream na condensed milk" naomba unielekeze ni vitu gani na je ndizo unatumia pia na wewe Katika utengenezaji wako wa ice cream, na vipi kuhusu upatikanaji wake madukani na bei zake.
 
Habari, naomba kujua mchanganuo wa biashara ya Ice cream za Azam ikoje. Ambaye anajua bei ya kununulia kiwandani kwa jumla na bei ya kuuza rejareja, sana sana zile za ukwaju.
 
Yaan askirim zangu zina ubora kila anaezila anasifia! Natengeneza za maziwa zenye ladha mbalimbali km vanilla, strawbery, banana na chocolate pia.. Ni tamu mno!
Naomba kujua please, unatumia maziwa freshi au ya unga?
 
Back
Top Bottom