Biashara ya kutengeneza na kuuza, ndio itakayo timiza ndoto zako

Biashara ya kutengeneza na kuuza, ndio itakayo timiza ndoto zako

Nasoma watu wanasema ujasiriamali unahitaji mtaji mkubwa ambacho sio sahihi hata kidgo. Ili ufanikiwe inatakiwa uweke pesa ndogo sana ukiona response ya soko ni nzuri ndio unaongeza...tolea mfano labda mikate, tengeneza mkate mmoja kwaa kutumia sufiria, fanya mbwembwe zako uwe tofauti na ubora kukiko iliyopo sokoni ninda kwenye mgahawa wowote waombe uwape kama sample watakayowauzia wateja alafu utakaa upokee feedback kwa walaji, ikiwa nzuri a mingine sambaza bureo anglia feedbacks ukiona watu wanaupenda sana...anza production mtaji hata bank wanakupa ukiwa na field report nzuri...ila wewe hata uwe na bilioni ya kuwekeza ukatengeneza mikate ambayo watu hawaipendi hiyo pesa umepoteza...ujasiriamali hauitaji mtaji mkubwa mwanzoni
 
Mkuu Sasa mimtaji wangu m40 natafuta machine zakuzalisha kile kinacholingana na mtaji wangu...mfano wa paper bags,bamboo tooth stick
Kwa sasa ni vizuri kuzalisha kile ambacho kinaendana na bajeti yako kwa sasa; kwa huko baadaye mambo yakiwa mazuri unaweza kuamia kwingine
 
Biashara ya viwanda ngumi, wew tengeneza brand yako,
Fanya kama wanavyofanya kina Ailyons, Nike, na wenzake,

Miliki lab tu, kutengeneza outsource,
Tatizo kwenye 'outsource' unakuwa huna tofauti na watu wanaoagiza mzigo china na kuja kuuza hapa; ingawa utakuwa umeweka 'lable' yako.
Hapo 'core function' yako inakuwa inafanywa na wengine; hili ni tatizo. Ni bora uagize mali ghafi, uje ukamilishe mwenyewe ukiwa huku.
 
Biashara ya viwanda ngumi, wew tengeneza brand yako,
Fanya kama wanavyofanya kina Ailyons, Nike, na wenzake,

Miliki lab tu, kutengeneza outsource,
Biashara ya viwanda ukitaka kuijua ugumu wake waulize wale wa Arusha viwandani umeme ulipoanza kusumbua mwisho wa mwaka.

Una contractual obligations kupeleka order ya units kadhaa kwa mteja, kashalipa hela alafu umeme unakata kipuuzi bila taarifa.
Ukijichanganya usitimize masharti kuna kesi ya mamilioni unaweza pewa, order ya 6M ila kesi unaweza daiwa 40M, bora uingie hasara uzalishe.

Unachoma mafuta ya generator na sababu ulikuwa unajitafuta basi halina power ya kutosha, mashine zinajam, mara linachemka linaharibika linahitaji spare na matengenezo. Hapo umeme unakuja nusu saa unakata. Maji nayo mamlaka inakwambia umeme shida ndio maana hayatoki.

Anakuja OSHA anakuta masharti hujatimiza (si ndio kwanza unajaribu). Anakuja fire, anakuja TRA, anakuja mpumbavu gani mwingine kutoka serikali.

Usiende kichwakichwa. Kila kitu akili
 
Kweli nilibugi mno kurukia hiyo biashara bila kufikiria vizuri na kutafiti. Maelezo yako ni mazuri ila kwa bahati mbaya umeshindwa kabisa kuficha upumbavu wako hapo nilipo-bold.
Tukizungumzia biashara weka siasa pembeni kubali uhalisia hata kwa maumivu. Nilijua utapanick, niliishakwambia akili unazo tatizo tu huyo mtalii wako hutaki atajwe vibaya.

Mfanyabiashara mzuri ni mwanasiasa mkubwa sana, anajua kula timing na kusoma upepo na anajua kabisa huyu mwanasiasa ni mweupe kichwani hata kama atajipendekeza kwake. Hata madiwani na mameya wa majiji, wafanyabiashara wao wanawajua vizuri sana.
 
Tatizo kwenye 'outsource' unakuwa huna tofauti na watu wanaoagiza mzigo china na kuja kuuza hapa; ingawa utakuwa umeweka 'lable' yako.
Hapo 'core function' yako inakuwa inafanywa na wengine; hili ni tatizo. Ni bora uagize mali ghafi, uje ukamilishe mwenyewe ukiwa huku.
Hapana, ukiweka brand yako ni tofauti, unaweza leo tengenezea china, kesho India, unakuwa umekwepa stress nyingi sana
 
Back
Top Bottom