Mac Alpho
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 13,953
- 27,825
Hili ni wazo zuri sana, changamoto huwa inakuja kwenye ukusanyaji wa hayo mazao kutoka sehemu tofauti maana inahitaji uwe na stock ya kutosha kuhudumia kwa muda wa kipindi kirefu ndani ya mwaka.Kilimo ni kizuri kama kuna uhakika wa maji au mvua; au unaweza ukagawa sehemu, nyingine ikawa ranch ya mifugo kama mbuzi au kondoo.
Au ukaanzisha kampuni ya kununua mazao na kuyaongezea thamani; hii haiathiriwi na ukosefu wa mvua vs mkulima.
Changamoto nyingine ni namna ya kupenya sokoni maana linapokuja swala la bidhaa za mazao ya chakula (mf mchele), waTz wengi wamezoea vitu local kuliko vile ambavyo vipo kwenye vifungashio tayari.