Ndio maana utoaji leseni unaendana na kiwango cha mtaji wako ulionao. Mfano mimi mtaji wangu ni elfu ishirini nitaenda kuchukua leseni manispaa kwa sababu biashara yangu ni ndogo...wenye mitaji mikubwa hiyo milioni 500+ ndio wanaenda huko wizarani kuchukua leseni. Consultant nyie ndio kikwazo kikubwa cha watu kusajili kampuni, mkiombwa ushauri jinsi ya kufungua kampuni mnaorodhesha vitu vingi mara sijui Memorandum....mara Tax Clearance, Mara Board of Directors mpaka watu wanakata tamaaa. Ina maana mimi na mke wangu tumeishia darasa la saba wote hatuwezi kufungua kampuni?