Biashara ya Kutoa Mikopo (Microfinance): Hatua, Taratibu za Kufuata na Ushauri wa Uendeshaji

Biashara ya Kutoa Mikopo (Microfinance): Hatua, Taratibu za Kufuata na Ushauri wa Uendeshaji

Vibali vinatolewa na Benk kuu ya Tanzania baada ya wewe kusajili kampuni Brela. Tuwasiliane juu ya mchakato wa Benk kuu (maana kuna docs za kuasilisha) kama bado upo interested.
 
Vibali vinatolewa na Benk kuu ya Tanzania baada ya wewe kusajili kampuni Brela.Tuwasiliane juu ya mchakato wa Benk kuu( maana kuna docs za kuasilisha) kama bado upo interested
Huyu anataka kuanzisha Microcredit siyo Micro Finance so hakuna haja ya benk kuu hapo.Wizara ya viwanda na biashara inatosha.

- Anyway mkuu nikuulize, Unaweza kunisaidia kuandika MEMARTS kwa gharama kiasi gani na Je, ninaweza kusajili kampuni mbili kwa mpigo kama Mkaruka group of companies Limited?
 
Huyu anataka kuanzisha Microcredit siyo Micro Finance so hakuna haja ya benk kuu hapo.Wizara ya viwanda na biashara inatosha.

- Anyway mkuu nikuulize, Unaweza kunisaidia kuandika MEMARTS kwa gharama kiasi gani na Je, ninaweza kusajili kampuni mbili kwa mpigo kama Mkaruka group of companies Limited ?
Kuna tofauti gani kati ya microcredit na microfinance?
 
Kuna tofauti gani kati ya microcredit na microfinance?
MicroCredits wanatoa Mikopo tu kwa wateja wao kwahiyo ukiwa na kiasi chochote kinachowezekana unaanza Eg PLATINUM, lakini Micro Finance inahusika kutoa MIKOPO na pia inachukua pesa za watu kama AKIBA - AMANA- DEPOSITS, Hivyo ni lazima upate Kibali cha Bank kuu na hata mtaji wake ni kuanzia Bilioni eg FINCA.
 
AsantenFi wakuu nadhani M.I.T ndo wanahusika hii n kwa mjibu wa juhudi nilizofanya kwa kuzingatia maoni ya wengi lkuyttfffft.
 
Mngejadili kwa wazi hapa ingekuwa bora zaidi
 
Kuanzisha microcredit kiwago cha mtaji kisipungue 700mil, ili kupata kibal cha kufanya kazi unabidi uwena 500mil tena ni minimun capital alafv 200 ndo hapo saa kufungua branch na HQ wafanya kaz, ukiwa na 700ml utaweza kua NA kampuni ya microcredit kama TUNAKOPESHA ltd.
 
Habari wana Jf,
Heshima kwenu wote na hongereni kwa michango na mawazo mazur ambayo mmekua mkitoa juu ya mada mbali mbali,
Mm nikijana nimemaliza degree ya biashara katiaka fedha (BCOM-FINANCE)

Nimekua na ndoto ya kuwa na micro finance institution toka nipo mwaka wa kwanza chuo, hvyo nikajipanga nimetafuta mtaji nimepata (japo sio mkubwa). Kinacho nisumbua kwa sasa ni uzoefu juu ya uendeshaji wa biashara hii, kwan elimu niliyo nayo ni ya natharia (theoretical).
Nimetafuta sehem ya kufanya kazi japo kujitolea kwenye microfinance institution ili nipate uzoefu ila sijafanikisha.
Naomben msaada wenu, kwa mtu mwenye uzoefu juu ya hii biashara anisaidie kujibu maswar yafuatayo:
1. Usajiri
2. Riba na ulipaji wake (kwa mwezi, mwaka au wiki)
3. Maswala ya kisheria (defaulters)
4. Makundi ya wateja wasumbufu na wasio wasumbufu wakat wa ulipaji
5. Software ambayo inatumika kuhfadhi hizi transaction.
6. Kipengere chochote cha muhim nilichokisahau!
Maana nataka nianze bila uzoefu wowote, nimechoka kutembea na bahasha kutafuta sehemnya kujitolea.
Asanten, naomba kuwasilisha.
Mrejesho mkuu
 
Habari wana Jf,
Heshima kwenu wote na hongereni kwa michango na mawazo mazur ambayo mmekua mkitoa juu ya mada mbali mbali,
Mm nikijana nimemaliza degree ya biashara katiaka fedha (BCOM-FINANCE)

Nimekua na ndoto ya kuwa na micro finance institution toka nipo mwaka wa kwanza chuo, hvyo nikajipanga nimetafuta mtaji nimepata (japo sio mkubwa). Kinacho nisumbua kwa sasa ni uzoefu juu ya uendeshaji wa biashara hii, kwan elimu niliyo nayo ni ya natharia (theoretical).
Nimetafuta sehem ya kufanya kazi japo kujitolea kwenye microfinance institution ili nipate uzoefu ila sijafanikisha.
Naomben msaada wenu, kwa mtu mwenye uzoefu juu ya hii biashara anisaidie kujibu maswar yafuatayo:
1. Usajiri
2. Riba na ulipaji wake (kwa mwezi, mwaka au wiki)
3. Maswala ya kisheria (defaulters)
4. Makundi ya wateja wasumbufu na wasio wasumbufu wakat wa ulipaji
5. Software ambayo inatumika kuhfadhi hizi transaction.
6. Kipengere chochote cha muhim nilichokisahau!
Maana nataka nianze bila uzoefu wowote, nimechoka kutembea na bahasha kutafuta sehemnya kujitolea.
Asanten, naomba kuwasilisha.
Samahani hebu rekebisha izo r ziwe l.
 
Wakuu na biashara ya pawn shop? Nayo Ina fall kwa categories hizo?
 
Habari wanajukwaa

........................................................................................................
Update: MABADILIKO JUU YA KUPATA LESENI YA BIASHARA YA MIKOPO
Kwa mujbu wa notisi ya Benki Kuu ya Tanzania kuna mwongozo umetolewa w namna gami kampumi au mtu binafsi anaweza kufanya biashara hii ya kutoa mikopo
1. Suala la Mtaji
2. Jina la kampuni kuwa na neno linalotambulisha shughuli ya kampuni
3. Shughuli zilizoainishwa ktk MEMARTS kuwa za mwelekeo wa masuala ya fedha tu
4. Wamiliki wa kampn kuwa na elimu tambuzi juu ya biashara hata kama wameajiri wasimamizi
5. Taratibu za kupata kibali na leseni
6. Makundi yalivyogawanywa ie Tier 1,2,3 na 4 nk
..,.....................................................................................................

Vile vile tumeandaa semina juu ya notisi hiyo ya BOT kwa wadau wanaohitaji karibuni sana
........................................................................................................

Watu wengi wamekuwa wanauliza juu ya suala hili wengine ikiwa hapa jukwaani na wengine kwa kuja PM. Naona vema kuweka wazi suala hili katika jukwaa letu maarufu la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali.

Mwongozo huu unaweka bayana juu ya kusajili kampuni ya kutoa Mikopo binafsi na upatikanaji wa leseni yake (Application conditions for Microcredit business license)

Utangulizi

Microcredit company ni kampuni inayojihusisha na kutoa MIKOPO TU kwa mtaji binafsi iliyonayo na hairuhusiwi kuweka pesa za mtu hii itambulike hivyo.
Ukitaka masuala ya kuweka na kutoa pesa huko ni Microfinance.

Leseni ya biashara hii inatolewa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ofisi za BRELA Ghorofa ya 5, jengo la ushirika, brbr ya Lumumba, Mnazi mmoja, Dar es Salaam.

Mambo muhimu yanayotakiwa ni

1. Usajili - BRELA
Hapa ni kusajili kampuni au partners inategemea mmejipanga vipi na hufanyika BRELA. Mtaji lazima uwe mkubwa, jitahidi uwe japo 50mil+ japo nashauri uwe mkubwa (mfano x00mil) zaidi kwani biashara hii inaweza kukua hadi ukahitaji kuanza huduma za kutoa na kuweka pesa (microfinance)
Hakikisha MEMARTS au Partnership deed yenu isiwe yenye mlengo (Objects) wa biashara yoyote isiyosimamiwa na Benki Kuu

2. TIN-TRA
Sajili TIN ya kampuni TRA, pata TAX CLEARANCE CERTIFICATE ambayo utaandika inaenda Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji

3. Sera ya ukopeshaji (lending policy and procedure Manual)
Uwe na hii sera ya ukopeshaji ambayo itatoa mwongozo wa riba, taratibu, kanuni nk

4. CV za wanahisa
Wanahisa/wakurugenzi/wahasibu wawe na CV na vyeti kuonyesha uzoefu wao ktk tasnia ya fedha

5. Taarifa za kifedha
Walau taarifa za fedha (bank statements) zao wanahisa au kampuni walau kwa miezi mitatu

6. Uthibitisho wa uraia
Kopi za vitambulisho vya Taifa vilivyothibitishwa

7. Mkataba wa Pango
Uwe umethibitishwa kisheria na vilivile umelipiwa kodi ya stempu TRA

8. Nyaraka zote zibanwe kama kitabu

Wazoefu na wajuzi zaidi wanaweza kuongezea zaidi. Karibuni kwa mjadala

Kwa huduma hizi unaweza kumtumia Consultant alie jirani yako au ukatucheki kwa email: consultafrolinktz@gmail.com na mobile/whatsapp: 0659211222/0777777766/0755411455
 
wengine wanachukua leseni halmashauri, sio lazima huko wizarani, na mtaji wa kusajili kampuni Brela unaanzia elfu ishirini.
Ni kweli kusajili kampuni kiwango cha chini cha mtaji ni sh 20,000. Lakini unaweza sajili kampuni kwa mtajo huo na usifanye biashara kikwazo kikubwa kikiwa mtaji.

Nakupa mfano
Kampuni zenye kupata vibali CRB. Mfano kama civil engineering coy mtaji walau mil 500 ndiyo utapata kibali baada ya kukamilisha taratibu zote. Hivyo kwa mtazamo wako iwapo wewe ina mtaji wa elfu 20,000 utaweza kupata leseni? Soma kipengele cha kupeleka bank statement

Suala la leseni Mkuu hebu pitia nakala ya leseni zilizo kundi A zinazotolewa wizarani na kundi B leseni ndogo hutolewa Manispaa. Fomu ya leseni kama unayo soma kipengele namba 8 ktk biashara za kundi A ambazo hutolewa na Wizara, utaonda benk na huduma za fedha zinaangukia hapa.

Kwa hao wanaofanya kwa leseni ya manispaa sina uhakika kama wapo au laah maana hata ukiangalia list ya leseni za manispaa hakuna.
 
Ni kweli kusajili kampuni kiwango cha chini cha mtaji ni sh 20,000. Lakini unaweza sajili kampuni kwa mtajo huo na usifanye biashara kikwazo kikubwa kikiwa mtaji. Nakupa mfano. Kampuni zenye kupata vibali CRB. Mfano kama civil engineering coy mtaji walau mil 500 ndiyo utapata kibali baada ya kukamilisha taratibu zote.

Hivyo kwa mtazamo wk iwapo wewe ina mtaji wa elfu 20,000 utaweza kupata leseni? Soma kipengele cha kupeleka bank statement

Suala la leseni Mkuu hebu pitia nakala ya leseni zilizo kundi A zinazotolewa wizarani na kundi B leseni ndogo hutolewa Manispaa
Ndio maana utoaji leseni unaendana na kiwango cha mtaji wako ulionao. Mfano mimi mtaji wangu ni elfu ishirini nitaenda kuchukua leseni manispaa kwa sababu biashara yangu ni ndogo...wenye mitaji mikubwa hiyo milioni 500+ ndio wanaenda huko wizarani kuchukua leseni. Consultant nyie ndio kikwazo kikubwa cha watu kusajili kampuni, mkiombwa ushauri jinsi ya kufungua kampuni mnaorodhesha vitu vingi mara sijui Memorandum. Mara Tax Clearance, Mara Board of Directors mpaka watu wanakata tamaaa...Ina maana mimi na mke wangu tumeishia darasa la saba wote hatuwezi kufungua kampuni?
 
Ndio maana utoaji leseni unaendana na kiwango cha mtaji wako ulionao....Mfano mimi mtaji wangu ni elfu ishirini nitaenda kuchukua leseni manispaa kwa sababu biashara yangu ni ndogo...wenye mitaji mikubwa hiyo milioni 500+ ndio wanaenda huko wizarani kuchukua leseni.....Consultant nyie ndio kikwazo kikubwa cha watu kusajili kampuni......mkiombwa ushauri jinsi ya kufungua kampuni mnaorodhesha vitu vingi mara sijui Memorandum....mara Tax Clearance, Mara Board of Directors mpaka watu wanakata tamaaa...Ina maana mimi na mke wangu tumeishia darasa la saba wote hatuwezi kufungua kampuni?... ...
Mkuu LAKI si pesa
Kwanza tambua LESENI YA BIASHARA HAITOLEWI KWA KIGEZO CHA MTAJI bali inatolewa kwa:
1. Leseni kundi A (zitoleazo wizarani)
Kwa kuangalia Sera ya Taifa, sura ya Taifa au Kimataifa ktk utekelezaji na inaongozwa na sera. (Refer biashara ya mikopo inaongozwa na sera)
2. Biashara kundi B ndogo (Manispaa)
Biashara hizi haziongozwi na sera ya Taifa na utekelezaji wake hauna mwongozo wa sera ya Kitaifa au Kimataifa. Hivyo utaona hy biashara kama ilisajiliwa hapa si sahihi.

Suala la Consultant
Kwa bahati mbaya ktk nyuzi mbalimbali umekuwa na mtazamo hasi juu ya Consultants. Tambua consultants hawafanyi kazi kwa matakwa yao balinkwa kufuata taratibu, sheria na kanuni zilizowekwa ktk kutoa mwongozo sahihi wa uendeshaji wa biashara. Consultants wana umuhimu mkubwa ktk jamii katika kutoa mwongozo sahihi wa masuala yote ya biashara kwa ujumla wake na ndiyo maana hata usajili wa Consultant firm lzm upeleke vyeti vya taaluma hii: soma hapa
Umuhimu wa kumtumia Mshauri wa kibiashara katika usajili wa kampuni na mengineyo

Elimu ya darasa la saba
Usajili wa kampuni haujaweka ukomo wa elimu ktk usajili wa kampuni. Kwa mfano. Hata wewe na mkeo mwaweza kusajili kampuni ya mikopo lkn CV zikatumika za waajiriwa wako wenye sifa za kupata leseni ya biashara ya kutoa mikopo

USHAURI JUU YAKO
Huenda unapenda kujifunza kujua masuala mengi juu ya sheria, taratibu na kanuni za biashara lkn huzifahamu (niwie radhi kama sipo sahihi) jitahidi uulize. Pili, ondoa dhana potofu juu ya Consultants! Na usiwaze ni watu wa kucomplicate mambo laah hasha. Jenga urafiki na consultants mbalimbali kama wa biashara, sheria, utawala nk. Utakuja "prove" ulikuwa "wrong" kimtazamo wako
 
Yap....Tena wengine mitaji yao hata laki tano haifiki.
Kosa halisahihishwi kwa kosa. Huenda kuna kosa mahala wakati wa kutoa leseni. Unaweza kuwafurahia hao wanaotoa mkopo kwa mtaji huo wa laki tano lkn hebu angalia riba wanayowaumiza mtaani! Je utaendelea kuumia kwa riba kubwa zisizo na udhibiti mpaka ln? Pili, sera ya mkopo nani aliipitia na kuiidhinisha hk manispaa kwa sababu biashara zinazoongozwa kqa sera husimamiwa na wizara
 
Back
Top Bottom