Biashara ya kuuza dawa za kulevya inalipa sana haitokaa iishe duniani

Biashara ya kuuza dawa za kulevya inalipa sana haitokaa iishe duniani

Nafaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
12,154
Reaction score
31,246
Leo nilikuwa ninatazama documentary mpya kabisa ya DW imetoka mwezi huu ambapo mwandishi wa habari na camera man wake walizama columbia wakiwa na jeshi la kupambana na biashara za dawa za kulevya kuchukua matukio.

Kule ndipo zao linalimwa milimani na maporini, halafu huko huko linavunwa na kupeleka mahabara ziko huko huko porini. Yani majani 200kg ndiyo yanatoa 1kg cocaine. Likishazalishwa, linasafirishwa kama unga tu wa sembe mpaka town linauzwa kwa wadau ambao nao wanalipeleka mpaka Mexico. Yani 400kg za cocaine zikifika mexico zinauzwa dollar 8 milion yani zaidi ya billion 10 za kitz.

Sasa Mexico ndiyo shida, wao wanaifungua na kuifunga upya katika nusu kilo au 1kg, kwanza inatangualia aluminium foil, halafu wanamalizia na sole tape. Wakivusha 400kg kuingia Marekani inakuwa na thamani ya zaidi ya dollar milion 70, yani zaidi ya billion 150 za kibongo.

Documentary inaonyesha toka kitu kinatoka columbia kinaenda warehouse, kinatolewa warehouse kinapelekwa kwenye boat kwa ajili ya kuelekea Marekani. Hawa ma drug lord hawana mchezo, muda wote wana askari wana ma AK47 na majambia ukijichanganya tu umekwisha. Mwandishi wa habari na crew lake waliamua kuwapa tu exclusive arekodi kila kitu lakini sura zao wamezificha.

Akiwa na askari wa columbia walivamia shamba flani wakaua ring leader na walinzi wake kadhaa. Hii vita sidhani kama wanaweza kuishinda aisee. Jamaa wanatumia kila mbinu kama jeshi kuanzia kuwasiliana kwa codes, na vifaa vya hali ya juu.
 
umoja wa mataifa utasema nini kuhusu mmea huo, bangi wamesema poa tu ilimwe kwa kutengeneza dawa,si ajabu huko mbeleni huo mmea wa cocain nao utaonekana uko freshi tu kwa kutengenezea dawa
Hakuna kitu kizuri wala kibaya bali ni perception tu. Wakati waafrika wanauzwa kama kuku wakiwa watumwa kwa waafriak wenzao nawazungu lilikuwa jambo la kawaida tu. Yani hata akikuua anasahau kama vile kachinja tu kuku na ataenda kuomba hata akiambiwa ataje dhambi alizotenda hawezi kutaja kumuua mtumwa kama ni dhambi.

Bangi sasa imeanza kuwa legalized, baada ya miaka kadhaa itakuwa jambo la kawaida tu. Sasa la kujiuliza ilikuwaje ikasemekana ni hatari na sasa huo uhatari umeisha vipi? Jibu ni kuwa labda haikuwahi kuwa hatari absi tu ilikuwa perception ya watu.

Cocaine ndo hiyo nayo, kitu cha mmea wa coca. Sijui chochote kuhusu hiki. Ila kuna jamaa aliniambia watu wengi wanaofanya mambo ya ajabu, wanatengeneza matangazo ambayo ukiona mpaka unajiuliza huyu jamaa aliwaza nini, au wana tengeneza mziki wa ajabu au movies hasa watu wa S.A na Marekani huko wengi wanapata imagination hizo wakiwa washa nusa mambo hayo.
 
Et kulegalize mtakuwa mnasinzia hovyo mitaani
 
Basi ili kutibu ukimwi ni kutotoa dawa za kupunguza makali ili atakae umwa afe. Au tuwape poison kwenye zle dawa, au tuite meli kubwa wapande tukawatelekeze katikati pale Bermuda najarbu kuwaza tu kwa sauti[emoji849][emoji849][emoji849]
Yote majibu
 
SASA kama yale makaburi ya kifahari ya wauza unga wakubwa kule mexico,ina maana serikali ya huko haiyaoni? kama inayaona inashindwa nini kuyabomoa? Makabari yamejengewa vijumba na misalaba juu,jumuiya ya kikristo inashindwaje kuwakemea wauza unga waache kuweka misalaba kwenye makaburi yao?
 
SASA kama yale makaburi ya kifahari ya wauza unga wakubwa kule mexico,ina maana serikali ya huko haiyaoni? kama inayaona inashindwa nini kuyabomoa? Makabari yamejengewa vijumba na misalaba juu,jumuiya ya kikristo inashindwaje kuwakemea wauza unga waache kuweka misalaba kwenye makaburi yao?
 
Back
Top Bottom