Biashara ya madini ni kichaa. Kaka yangu kapoteza milioni 120 mwezi huu nimemkuta ameshaanza kudata

Biashara ya madini ni kichaa. Kaka yangu kapoteza milioni 120 mwezi huu nimemkuta ameshaanza kudata

Aisee naandika huu Uzi nikiwa nimekuja kumtembelea kaka yangu hospital hapa Mbeya, aisee hii biashara sio ya kuingilia kichwa kichwa.

Huwezi amini nipo hospitali maana broo kama akili zishaanza kuwehuka, vitu anavyoongea havieleweki aisee, haamini kama kafukia milioni 120.

Nawashauri ndugu zangu wana jamiiforums hii sio biashara ya kufanya, ni kama inauchawi fulani hivi!
Mbona kapoteza pesa kidogo sana. Wenzake wanapoteza 500M-1B na hawarudishi silaha ghalani. Hapo ndio anakomaa inatakiwa arudi tena. Hii kanuni nafikiri hakuizingatia "The higher the return the higher the risk. Ukipigwa umepigwa na ukipiga umepiga. Asifikiri wakina Mdimi na mdogoake Misgwa mpaka wanapata jiwe la over 24B walipoteza 10M.

Akiamka afute vumbi asonge na safari asibaki alipoangukia au kuahirisha safari
 
Yataka moyo na Kifua kuyashinda haya!
 
Wachimbaji wadogo wengi wanafanya kwa kubahatisha, hawafanyi utafiti.

Madini siyo maharage ambayo unapanda sehemu na kuyaona yanavyokua. Kwenye madini, unatafuta kitu ambacho hukuweka wewe wala rafiki yako. Hivyo hatua ya kwanza ni kufanya utafiti, siyo kuchimba. Unachimba baada ya kufanya utafiti, na kujua yako wapi,, kwa kiwango gani.
Nakuambia unaweza fanya tafiti na ukapigwa vilevile. Kwenye madini kuna matapeli wa hatari sana. Kipindi hiki cha masika sample za dhahabu zinapandwa Kwenye vitalu visivyo na hazina. Ukija na kipimo cha kiangazi unakuta pori kila ukipenyeza kipimo kinasoma. Unakuja kuanza uchimbaji unaambulia 25M wakati kitalu umenunua 200M. Nakuambia unaweza kufa.

Uchimbaji wa madini unahitaji uwekezaji mkubwa ili kuifikia hazina iliyo mita 100 chini ya ardhi ndio utafurahia
 
Bro wako sio mvumilivu kwenye haya maisha. Nilishawahi poteza 270m, ni kweli iliniuma sana. Nilitulia kiume nikaendelea na maisha.

Nilishasahau na kutengeneza zaidi ya hiyo
Wewe ni mwamba ila pia inategemea na umri. Kama ni over 50 years of age kuhimili inakuwa ngumu. Sukari na pressure vinakumaliza
 
Wachimbaji wadogo wengi wanafanya kwa kubahatisha, hawafanyi utafiti.

Madini siyo maharage ambayo unapanda sehemu na kuyaona yanavyokua. Kwenye madini, unatafuta kitu ambacho hukuweka wewe wala rafiki yako. Hivyo hatua ya kwanza ni kufanya utafiti, siyo kuchimba. Unachimba baada ya kufanya utafiti, na kujua yako wapi,, kwa kiwango gani.
Utafiti na kutumia mambo mengi nayo ni gharama maradufu ila faida ipo sana ,
 
Hiyo hela ni ndogo sana kwenye Madini.

Tatizo mtu mtaji ni mdogo anataka kujingiza kwenye biashara kubwa ambazo zinahitaji Utumiaji mkubwa wa fedha kwa kupata watalamu na vifaa vya kisasa vya kugundua uwepo wa madini ni wapi, Na sio kufukua fukua au kuchimba chimba tuu.

Sasa 120 milioni nae atajitia mwekezaji katika uchimbaji? Mwisho wa siku unakuwa huchimbi madini ina unachimba udogo kwasababu unabakia kuwa mtu wa bahati nasibu kuwa yako hapa au pale.

Sio kwamba nadharau Hela yake ila ukiongelea ishu ya Madini hiyo hela wachimbaji wanaipoteza ndani ya wiki moja kwenye kutengeneza labda tuu njia au kwenye matumizi ya vifaa, umeme ,hewa , wafanyajakazi na chakula.

Alichokosea alijingiza kwenye Sehemu siyo level yake.

Nimeishi Mererani nimejifunza mengi kuhusu Madini.

Mnae mskia Billion Laizer kile kipindi anatangazwa kupata madini makubwa na kuwa bilionea alafu wakawa wanasema ni mchimbaji mdogo ambae alipata mabiloni , Usije ukadhan amewekeza milioni 120 labda. Ni mtu ameuwa zaidi ya bilioni za hela. Sasa jiulize mchimbaji mdogo anamaliza mabilioni ya hela jee level ya uchimbaji madini ndo unaweka milioni 120, nawe utajiesabia umewekeza kwenye madini?

Na sio kuwa madini yanaushirikina kama wengi wamavyojidanganya ila yanahitaji vifaa vyakisasa na watalamu haswa wa miamba uweze kuyapata kwa uhakika ila hela nayo inapotea ya kutosha.
 
Kweli mkuu, sawa na kazi ya mafundi,ukimchukua injinia akujengee na umchukue fundi maiko akujengee, uhakika wa nyumba Yako ni injinia!
Ndiyo maana Barrick, GGM, SHANTA, WILLIAMSON (MWADUI) hatusikii wakitoa kafara wanaelekezwa tu na technology na hawachimbi kwa hasara wale mafala wanatoa kitu chenyewe ila sisi bila kujua, mtaji mdogo tunafanya kubahatisha matokeo yake lazima udate
 
Wengi wanaingia with unrealistic expectations wanadhani wataenda leo na kuwa matajiri overnight. Never happening.

120M kwenye madini ni hela ndogo sana itakua alisikiliza wachimbaji wadogo wakamjaza matumaini hewa. Hiyo haikutoi hata kwenye level ya uchimbaji mdogo.

Angeuliza wachimbaji wakongwe hapo Chunya wanafanyaje kazi kabla ya kuingiza hela zake.

View attachment 3269195
120M sio ndogo, hiyo ni hela nyingi sema inategemeana unafanya nini kwenye dhahabu?
 
120M sio ndogo, hiyo ni hela nyingi sema inategemeana unafanya nini kwenye dhahabu?

Ni hela ndogo sana kwenye hii sekta. However I agree with you inategemea unafanya nini, kuna upande inaweza kukuvusha toka hatua moja kwenda nyingine na kuna angle hutoboi kwa hiyo hela. Kama aliingia kwenye uchimbaji moja kwa moja alienda kupoteza I could tell him that a mile away. Kama aliingia kama dealer/broker labda angeweza kutoboa ila inahitaji a lot of information na network kubwa.
 
Angeingia kwa kuozesha udongo ingemlipa ikiwa angefanya kazi na watu sahihi.

Uchimbaji wengi wanabahatisha na kutapeliwa na waganga.
 
Back
Top Bottom