Biashara ya Madini ya Dhahabu: Fahamu Uwekezaji Wake, Changamoto na Faida


Uko sahihi
 
MImi leo yangu ni maswali tu ELUTION PLANT NI NINI? Inafanya kazi gani? Ni sehemu ya PALNT NZIMA au ni kifaa/mashine inayojitegemea?
Ukishasaga mawe yako ukaosha..like tope kikiwa kubwa ndo tunapeleka plant ..lakini kabla ya kupelekwa plant unapima kujua kifusinchako kitatoa dhahabu kias gan...huko Sasa ndo zinaanza process za kuchomoa

Dhahabu .process haizid 2-4wks..! Kule Kuna chemicals wanachanganya na kifusi kuchomoa dhahabu. .ah nenda ukajionee
 
Risks za kupoteza mtaji kama umeamua kufanya biashara ya kota ni nn? Chakuzingatia ni nn?

Sent using Jamii Forums mobile app
Risk ni kubwa unanunua saa11 jion dhahabu kwa 80000/- kesho ukipeleka jikoni imedrop maybe kwa 3000/-bado Kuna vipoint huwa vinapungua unapochoma na Kama ndo mgeni Kuna vipoint hapo lazima wanakuibia so gram moja unaweza katika hata 7000/!

Chakuzingatia ni wewe kuwa MWIZI!

na wakishajua Kota fulani anaibia wateja utakesha kusubiria mzigo!na habari zinasambaa fast. Watu wanakuwa wanakupita tu utakoleza mkaa had usinzie hakuna anayekuuzia!
 
Sawa ahsante. Kwahyo ili uweze kulinda mtaji usipotee mpaka ntakapokua mzoefu nianzie wapi ambapo risk ni limited? Kwa kununua karasha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa ahsante. Kwahyo ili uweze kulinda mtaji usipotee mpaka ntakapokua mzoefu nianzie wapi ambapo risk ni limited? Kwa kununua karasha?

Sent using Jamii Forums mobile app

Kiuhalisia Bora ununue kalasha na uhakikishe unanunua mawe mazuri, uvumilivu zaidi, maana unaweza panga ufanye kazi kwa 3mths ikafika had 6mths. Natural disasters, mvua, ukosekanaji wa mawe, duara kujaa maji etc etc!
 
Vingi ulivyoongea sio vya kweli na tabia ya wizi wizi ama utapeli kwa kota/digala hiyo ni tabia ya mtu na si kila kota/digala wala haikutaki uwe hivyo ili ufanikiwe ktk dhahabu.

Dhahabu ya machimbo purity iwe asilimia 77% khaa! hiyo sijapata kuiona labda ktk dhahabu za vyombo. Hapa tanga asilimia ya chini ni 97.3% ila ya kawaida ni 98.4% na biashara hii haitaji uwe na jiko ndo ufanikiwe maana hapa kwa kila gram unabaki na gap la 25k kama faida,,, kinachotakiwa hasa ni kuomba Mungu mgodi utoe madini hapo hela utaziona yakiwa machache usanii unakuwa mwingi.
 
Sawa mkuu
 
Tanga sehemu gani uliko?
 
Sawa ahsante. Kwahyo ili uweze kulinda mtaji usipotee mpaka ntakapokua mzoefu nianzie wapi ambapo risk ni limited? Kwa kununua karasha?


ILI KULINDA MTAJI USIPOTEE WAKATI WA KUTAFUTA UZOEFU WA BIASHARA

Kk kama una mtaji tafuta eneo ambapo dhahabu inatoka kwa wingi nenda jenga kakibanda tega scale yako lipa bei nzuri wachimbaji watakuletea dhahabu bila kuhangaika na hela yako haitakata hata nukta.

Angalizo:-

A. Ulizia kwa mtu unaemwamini dhahabu ya eneo husika ni safi kiasi gani/ purity % yake, hiyo itakupa muongozo wa bei ya kununulia + bei zinazotamba mtaani

B. Usimdhamini mchimbaji kbs we mwambie unanunua dhahabu tu na uzidishe kama 1000 toka bei ya kawaida

C. Uwe na mtu atakaekusaidia kuchoma na kupuliza madini yasiyokamatishwa na mercury hadi utakapozoea

NB: Naongea kwa uzoefu wangu, 1 kuhusu return za karasha na risks zake 2, ni mnunuaji wa muda na faida yake naijua ila nakushauri kama una hela za mawazo achana na karasha uncertainty zake ni kubwa mno
 
Pia nadhani kama utakuwa unanunua toka kwa wachimbaji, ni vizuri uwe unajua hata bei ya kwenye soko lako. Si kibiashara kununua bei ya juu na kuuza bei ya chini; pia kuna suala la uzito, ukinunua na kisha kwenda kuchoma lazima uzito utapungua. Na hivyo kula kwako au siyo sasa unafanyaje katika hali hii?
 
Hahahhahah brother kumbe ndio sababu wanaotoka kanda ya ziwa huku mgodini hawaeleweki ...

Hivi mchimbaji utamuibiaje!!! Imagine mtu karisk maisha yake kwenye fonga then umletee hbr zisizoeleweka si atakupiga moko labda uwe umemdhamini hlf umzingue kwenye bei vinginevyo awe form 1 si rahisi kumuibia mchimbaji labda utumie ubabe mwingi na huo sio utu ila yeye ndio rahisi kukuibia hususani ukiwa umemdhamini..

Pia dhahabu bei haipangwi na mtu mmoja kama nyanya muanze kulumbana kuna apps kibao ambazo wenye majiko hutumia kupanga bei ya siku mfano netnadia wanatoa live update ya commodity price kila baada ya dk kadhaa pia unaweza angalia bei ya silver ama gold muda husika live online na trend ya kushuka mtu unaiona ukihofia kama una mzigo mkubwa unampigia mnunuzi wako nna labda gram 100 nakuja baada ya siku 2 ila naziuza kwa bei ya leo, hapo itategemeana na anakuamini kiasi gani mana baada ya siku 2 inaweza kupanda zaidi mfano itoke kwenye 140000 iwe 145000 ambapo ww itakubidi umuuzie kwa ile mliyofunga awali yani 140 and vise verse, hawa wanunuaji wakubwa wanapanga bei... Kuiba ni dhambi Pima kihalali kama hujadhamini biashara ya dhahabu haina hasara

Say no to #Ujanjaujanja
 
Uko sahihi Sana!
 
Samahani..hapo ulisposema uzidishe 1000 sio wizi!?..au
 
Tanga dhahabu zinapatikana kila kona ila uzalishaji wake ni mdogo na purity yake nahisi ndio inaongoza kwa tz
Yaani ww ni mbishi mjuaji bila sababu ....ukishaona mgodi dhahabu zake chache percentage za kufeli ni100/-%. Yaan kwa siku unashundia gram 7! Faida hapo si ya kula tu. Lol.tembeaga uone. Kuna machaka purity had 68%>>sema umekuja kubishana nakuangalia tu
 
Sijui nyie hii biashara mnaifanyaje, kama mnunuaji lazima kila leo uwe na update ya bei ya siku kila leo isipokuwa jumapili lazima ujue bei sokoni ikoje, na uweze kulisoma soko linaenda kupanda ama kushuka, we utanunuaje bila kujua unaenda kuuzaje???

Dhahabu kupungua uzito inategemeana mfano hizi za kukamatisha na mercury unapaswa uichome haswaa tena kwa mkaa wenye nguvu uhakikishe mercury yote imeisha ukiitoa dhahabu ikiwa njano iliyokolea ile kama inaenda kuwa red ama brown hivi hiyo imeiva vzr japo wachimbaji wanakuwa wakali ila inabidi ukomae nao mana wao wanataka ubabue ili mercury iwabebe ila ukichoma vzr hata kama ni dungu la gram 40 halitopungua zaidi ya point 5 au chini zaidi,

Zile zisizokamatishwa zinapungua kama mtu hukupuliza vzr yaan umenunua zikiwa na uchafu mwingi hivyo zikichomwa ule uchafu ukitoka ndio zinapungua kulingana na uchafu uliokuwepo au kuzidi hapo ila ukizipuliza vzr huwa hazipungui sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…