Biashara ya Madini ya Dhahabu: Fahamu Uwekezaji Wake, Changamoto na Faida

Biashara ya Madini ya Dhahabu: Fahamu Uwekezaji Wake, Changamoto na Faida

🎤🎤🎤JAMANI MALINYI MISEGESE KUMEHILA,(KUMELIPUKA DHAHABU)
wale wenye kusimika Gest mpooo...
Wenye mpesa..
Kuweka plant..
Makota
Mama lishe. ! Huu ndo wakati wa kutengeneza pesa wakati mgodi wa motomoto...😋😋! Mie soon nafika huko ntawapa mrejesho...lols!
Asante sana kwa hii taarifa Mkuu, hayo maeneo yapo katika Wilaya gani huko?
 
Hii biashara inakuhitaji sana mwenyewe uwepo eneo la tukio na uwe na akili nzuri kidogo ili kurun show na kutoboa.
Ni biashara nzuri kama kichwa chako ni kizuri na kweli una kiu ya mafanikio.

Kuna namna tofauti tofauti ya kujihusisha na hii biashara kwa mzoefu na kwa ambaye sio mzoefu.

Unaweza kufuata huu mtiririko kadili uonavyoona inafaa.

  • Jipe muda kwa kuzungukia maeneo kadhaa ya uchimbaji ukiangalia nini kinachofanyika na namna gani watu wanaishi.
  • Kwenye mzunguko wako jipe muda sana kwenye machimbo mapya ya dhahabu.
  • Jaribu kuunda urafiki na watu wawili watatu watatu wanaofanya vitu vifuatavyo, mchimbaji, muuzaji, msagaji, mama ntilie, wenye mabaa na grocery ( tembelea hayo maeneo ujifunze kitu.)
  • Kwa wewe unayeanza sio jambo jema kuanza kununua na kuuza dhahabu kabla hujajua abcd za dhahabu - NI HATARI.
  • Ukiwa kwenye harakati za kusoma mazingira jiridhishe na biashara zote zisizo za dhahabu zinazofanyika na ambazo unaweza kuzifanya ili ukaishi mazingira hayo wakati unajifunza game.( kukodisha pump, blower, kuuza miti, mama ntilie, kuuza maji, grocery nk.
  • Ukipata kauzoefu kidogo Tafuta karasha la kusaga mawe used lenye hali nzuri kwa 5mil (jipya size ya kati ni 8.5 - 9 Mil).
  • Ukiwa na karasha fungua sehemu ya kusagia na kuosha (Mwalo) unapaswa kuwa na Karasha, mercury, mizani, magunia, maturubai ( roughly uwe na kama 10mil kibisha unaweza kuanza na 3mil nyingine iwe pembeni na total ni 13mil).
  • Wakati wa kusagisha na kuosha huwa unatarget vitu viwili ( Kuwa na rundo la mchanga hakikisha unasaga mawe yanayosoma vizuri na ununuzi wa dhahabu).
  • Hapo sasa ukiwa na mwalo na watu wanaoshea kwako unaweza kununua dhahabu kulingana na mzunguko lakini ukikomaa per day unaweza kulaza faida ya 100K +.
  • Ndani ya miezi sita mpaka mwaka kulingana na speed na usomaji wa rundo(kifusi) unaweza kuuza hela nyingi sana na ukatengeneza faida ambayo sasa ndio itakupa kiburi na kukubatiza kuwa miner sasa.
  • Mtaji ukikua sasa na bila shaka utakuwa unaijua network na dhahabu unaijua unaweza kuamua mwenyewe wakati unaendelea na karasha what is the next round..( Uanze uchimbaji [hii ni kamari na inahitaji ujasiri, hela na uwe mshirikina}, Ujenge plant kama mtaji umekua vizuri.
  • Binafsi sishauri sana kuingia kwenye uchimbaji unless uwe na muscles uchimbe kisasa kwa maana ya exploration na drilling ya kisasa otherwise hapo kuna mitihani sana na uamue kuikabili ( I know it and I'm doing this is reality, African magic is highly working here asikudanye mtu).
  • Kama uko vizuri na una muscles unaweza kujenga plant au ukanunua macompressor ukaanza kufanya drilling and blast kwa kukodisha.
  • Plant unaweza kuozesha mzigo wako mwenyewe unaosaga ukifikia kifusi cha kutosha na kukodisha pia wakati mwingine.
  • Unaweza usifanye shughuli yeyote ukamiliki plant ukawa unakodisha watu wanaozesha (usijiingize kwenye dhambi hapa kwa kuwapiga watu dhahabu plant kiujanja si jambo zuri kwa mpambanaji)
  • Gharama ya plant na kila kitu roughly 40mil to 50 mil.
  • Narudia tena, usifanye biashara ya dhahabu kabla hujaijua dhahabu NI HATARI, Usiwe na tamaa utatamanishwa utaingia king watu watakupiga, Usiwe na haraka jiwekee focus yako mdogomdogo utatoboa.

Karibu mavumbini tulicheze disco, kuwa mvumilivu changamoto hazikwepeki ni kupambana nazo kadili zinavyokuja.
Usisononeke na maisha mazuri ya wenzio, Pambana usiku mchana, jua mvua utafika hizo level.
No easy man, work hard, God will put the bless. Heshimu watu.
Amen!
 
Nchi hii bado ina fursa nyingi tu, kwa bahati mbaya serikali ya CCM imezihodhi fursa karibu zote.
Hapa sasa unataka kuleta siasa wakati wana JF wanapeana maujuzi on GOLD BUSINESS. Wewe lalamika tu watu wakisonga mbele!
 
Mengi mno huko geita ndo yanatengenezwa 4m..lenye mfuko mmoja..8m lenye mifuko 2! Zuri ni Hilo kubwa...unafanya kazi double fast
Kwa nadharia yangu ndogo, CRUSHER au KARASHA (kwa lugha ya migodini!) ni lile mashine la kusagia mawe, yanatengenezwa humu humu nchi na yanakuwa na goroli ndani za kusagia au ku - crush hayo mawe ya dhahabu tayari kwa kupelekwa KUOSHA kwenye MWALO. Mwalo ni kama kadimbwi unakotengeneza pale machimboni aidha kwa kuletewa maji au kwa kutumia maji yatokayo chini ya maduara kule wanakochimba dhahabu. Wenye maujuzi Zaidi tufafanulieni.
 
Ukitaka kuanzisha tembelea sehem za kahama na geita upitie walau plants 5! Upate abc ...kwanza kupima tu udongo sample ni hela...30000/-..Sasa imagine wangap wanapima samples zao kujua kiwango Cha dhahabu kilichomo...kukodisha plant 2wks 4m! Na ni foleni sio kawaida..!labd uwe unajulikan
Wangari Maathai, PLANT inakuwa na vitu gani, yaani inakuwa na nini na nini, vimtambo gani vidogo vidogo vina comprise PLANT? Asante.
 
Biashara ya elution plants ni brand Kama unavyosikia ITV, CLOUDS etc....yaani Kama huna jina hamna biashara....elewa huku ni wasukuma wakisikia zile mashine wanaweka steel wire Kwny pipe ,yaani wanakukimbia Mara moja hata uwaambie unachoma mzigo bure.....walioanza wametangulia waache wazipige...ila ni biashara yenye kula hell kirahisi sijawahi kuona...fikiria Kuna mtu Ana mashine 5 na zote zinakula mzgo Kila siku kwa wiki,each mashine ni 1.2-1.5mil
Kwa siku anaingiza 6mil kwa wiki 42mil
MImi leo yangu ni maswali tu ELUTION PLANT NI NINI? Inafanya kazi gani? Ni sehemu ya PALNT NZIMA au ni kifaa/mashine inayojitegemea?
 
Hivi sister zile mashine za kusaga mawe yawe madogo [Si makalasha yakutoa unga] huwa ni bei gani na sijaona mnazizungumzia kabisa hapa.
Hizo Mashine mkuu zinaitwa jaw crusher au kimgodi zinaitwa jogirasha, bei ndo sijui
 
[emoji441][emoji441][emoji441]JAMANI MALINYI MISEGESE KUMEHILA,(KUMELIPUKA DHAHABU)
wale wenye kusimika Gest mpooo...
Wenye mpesa..
Kuweka plant..
Makota
Mama lishe. ! Huu ndo wakati wa kutengeneza pesa wakati mgodi wa motomoto...[emoji39][emoji39]! Mie soon nafika huko ntawapa mrejesho...lols!
Dadake ebu nicheki pm tutete jambo
 
Swali: Bei ya kununulia ni shilingi ngapi na unauza kwa bei gani hizo gramu 10 hadi upate faida ya 20 - 30 elfu? Na ni wapi, Geita au Mpanda?
Bei hupanda na kushuka. Leo inaweza kupanda kesho inadrop kufuatia soko la dunia. Sasa hivi dhahabu ni kuanzia 100k so unaweza nunua mfodini kwa 85-90! Kufuatia usafi wa dhahab
 
Back
Top Bottom