Biashara ya Madini ya Dhahabu: Fahamu Uwekezaji Wake, Changamoto na Faida

Biashara ya Madini ya Dhahabu: Fahamu Uwekezaji Wake, Changamoto na Faida

Kuna vimigodi vidogo vidogo lakini changamoto yake unapata mzigo mchache..kwa mfano kwa siku ukikusanya 4gm-10! Ni hasara.. Huko geita mie machocho niliyopita atleast Kanegele hakukua na msongamano sana na purity kule iko juu..plus ntambalale .

Ukweli kama unataka kutoka wekeza kwenye
1.Plant( hapa kama unaaminiana na mtu ingia naye share .) weka mkemia mzuri na mzoefu..hapa utapata kipato cha maana..hakikisha na wewe unakuwepo..sio unakaa Dar plant iko Mwambomba utapigwa had ushangae!
2. Nunua Crusher fukuzia kifusi kuza kifusi uza au peleka plant
3! Kuwa na sonara yako .means uwe na jiko lako la kuchomea dhahabu
4.Nunua vifusi.(sasa hapa itakubid kuwa na urafiki na mwenye plant naye unamgea %..ukinunua vifusi vizuri una hakika wakuwa na faida ya 5-7m every month ukikatika sana ni 3-5m( sasa ukiwa na plant yako nxt yr tutakuita don bila wewe kupenda)

All in all itakupasa kukaa migodini kusoma Michezo kwanza...! Kujua magumashi yanatokeaje!

La mwisho haya mamigodi yana uccm sana..walotoka sana kifedha lazima ccm iwahusu ..!la sivyo utasumbuliwa sana na tra...polisi...! Weka urafiki na polisi wa migodini..usijioneshe mpinzani in any means!

Kifupi sina hakika kama kuna hela tamu kama ya dhahabu😄😄! Ukiingia ukapata hutoki! So ni kuwa smart uje utafute mtaji!
Wewe bado upo huko au umehamia Chadema ha ha
 
MAENEO UNAYOWEZA KUWEKEZA KULINGANA NA MTAJI WAKO

Hii kazi ya madini in sekta nyingi ndani yake zinazotegemeana

Labda nizitaje na zinategemeana kimitaji

  • Uchimbaji(kutengeneza kifusi/marudio)
  • Kununua mawe
  • Kununua vifusi /marudio
  • Kununua dhahabu halisi
  • Kukodisha plant kwa ajili ya kuozesha marudio
-Kusimamia /mzabuni wa mgodi(gold Rush)
  • Kuuza vilipuzi/blasting materials
  • Kukodisha compressor kwa ajili ya uchorongaji mwamba
  • Mmiliki was duara kuuza hisa au kuuza working shift
  • Etc
 
Kuna vimigodi vidogo vidogo lakini changamoto yake unapata mzigo mchache..kwa mfano kwa siku ukikusanya 4gm-10! Ni hasara.. Huko geita mie machocho niliyopita atleast Kanegele hakukua na msongamano sana na purity kule iko juu..plus ntambalale .

Ukweli kama unataka kutoka wekeza kwenye
1.Plant( hapa kama unaaminiana na mtu ingia naye share .) weka mkemia mzuri na mzoefu..hapa utapata kipato cha maana..hakikisha na wewe unakuwepo..sio unakaa Dar plant iko Mwambomba utapigwa had ushangae!
2. Nunua Crusher fukuzia kifusi kuza kifusi uza au peleka plant
3! Kuwa na sonara yako .means uwe na jiko lako la kuchomea dhahabu
4.Nunua vifusi.(sasa hapa itakubid kuwa na urafiki na mwenye plant naye unamgea %..ukinunua vifusi vizuri una hakika wakuwa na faida ya 5-7m every month ukikatika sana ni 3-5m( sasa ukiwa na plant yako nxt yr tutakuita don bila wewe kupenda)

All in all itakupasa kukaa migodini kusoma Michezo kwanza...! Kujua magumashi yanatokeaje!

La mwisho haya mamigodi yana uccm sana..walotoka sana kifedha lazima ccm iwahusu ..!la sivyo utasumbuliwa sana na tra...polisi...! Weka urafiki na polisi wa migodini..usijioneshe mpinzani in any means!

Kifupi sina hakika kama kuna hela tamu kama ya dhahabu😄😄! Ukiingia ukapata hutoki! So ni kuwa smart uje utafute mtaji!

Plants zinahitaji mtaji kiasi gani kuanzisha?
 
Hii kazi ya madini in sekta nyingi ndani yake zinazotegemeana
Labda nizitaje na zinategemeana kimitaji
-uchimbaji(kutengeneza kifusi/marudio)
-kununua mawe
-kununua vifusi /marudio
-kununua dhahabu halisi
-kukodisha plant kwa ajili ya kuozesha marudio
-kusimamia /mzabuni wa mgodi(gold Rush)
-kuuza vilipuzi/blasting materials
-kukodisha compressor kwa ajili ya uchorongaji mwamba
-mmiliki was duara kuuza hisa au kuuza working shift
-etc

Mimi nataka kujua zaidi kuhusu hiyo ya kuuza vilipuzi, compressors na madawa. Mtaji, changamoto na faida zake.

Na hiyo ya umiliki wa elution plant.
 
Hii biashara inakuhitaji sana mwenyewe uwepo eneo la tukio na uwe na akili nzuri kidogo ili kurun show na kutoboa.
Ni biashara nzuri kama kichwa chako ni kizuri na kweli una kiu ya mafanikio.

Kuna namna tofauti tofauti ya kujihusisha na hii biashara kwa mzoefu na kwa ambaye sio mzoefu.

Unaweza kufuata huu mtiririko kadili uonavyoona inafaa.

  • Jipe muda kwa kuzungukia maeneo kadhaa ya uchimbaji ukiangalia nini kinachofanyika na namna gani watu wanaishi.
  • Kwenye mzunguko wako jipe muda sana kwenye machimbo mapya ya dhahabu.
  • Jaribu kuunda urafiki na watu wawili watatu watatu wanaofanya vitu vifuatavyo, mchimbaji, muuzaji, msagaji, mama ntilie, wenye mabaa na grocery ( tembelea hayo maeneo ujifunze kitu.)
  • Kwa wewe unayeanza sio jambo jema kuanza kununua na kuuza dhahabu kabla hujajua abcd za dhahabu - NI HATARI.
  • Ukiwa kwenye harakati za kusoma mazingira jiridhishe na biashara zote zisizo za dhahabu zinazofanyika na ambazo unaweza kuzifanya ili ukaishi mazingira hayo wakati unajifunza game.( kukodisha pump, blower, kuuza miti, mama ntilie, kuuza maji, grocery nk.
  • Ukipata kauzoefu kidogo Tafuta karasha la kusaga mawe used lenye hali nzuri kwa 5mil (jipya size ya kati ni 8.5 - 9 Mil).
  • Ukiwa na karasha fungua sehemu ya kusagia na kuosha (Mwalo) unapaswa kuwa na Karasha, mercury, mizani, magunia, maturubai ( roughly uwe na kama 10mil kibisha unaweza kuanza na 3mil nyingine iwe pembeni na total ni 13mil).
  • Wakati wa kusagisha na kuosha huwa unatarget vitu viwili ( Kuwa na rundo la mchanga hakikisha unasaga mawe yanayosoma vizuri na ununuzi wa dhahabu).
  • Hapo sasa ukiwa na mwalo na watu wanaoshea kwako unaweza kununua dhahabu kulingana na mzunguko lakini ukikomaa per day unaweza kulaza faida ya 100K +.
  • Ndani ya miezi sita mpaka mwaka kulingana na speed na usomaji wa rundo(kifusi) unaweza kuuza hela nyingi sana na ukatengeneza faida ambayo sasa ndio itakupa kiburi na kukubatiza kuwa miner sasa.
  • Mtaji ukikua sasa na bila shaka utakuwa unaijua network na dhahabu unaijua unaweza kuamua mwenyewe wakati unaendelea na karasha what is the next round..( Uanze uchimbaji [hii ni kamari na inahitaji ujasiri, hela na uwe mshirikina}, Ujenge plant kama mtaji umekua vizuri.
  • Binafsi sishauri sana kuingia kwenye uchimbaji unless uwe na muscles uchimbe kisasa kwa maana ya exploration na drilling ya kisasa otherwise hapo kuna mitihani sana na uamue kuikabili ( I know it and I'm doing this is reality, African magic is highly working here asikudanye mtu).
  • Kama uko vizuri na una muscles unaweza kujenga plant au ukanunua macompressor ukaanza kufanya drilling and blast kwa kukodisha.
  • Plant unaweza kuozesha mzigo wako mwenyewe unaosaga ukifikia kifusi cha kutosha na kukodisha pia wakati mwingine.
  • Unaweza usifanye shughuli yeyote ukamiliki plant ukawa unakodisha watu wanaozesha (usijiingize kwenye dhambi hapa kwa kuwapiga watu dhahabu plant kiujanja si jambo zuri kwa mpambanaji)
  • Gharama ya plant na kila kitu roughly 40mil to 50 mil.
  • Narudia tena, usifanye biashara ya dhahabu kabla hujaijua dhahabu NI HATARI, Usiwe na tamaa utatamanishwa utaingia king watu watakupiga, Usiwe na haraka jiwekee focus yako mdogomdogo utatoboa.

Karibu mavumbini tulicheze disco, kuwa mvumilivu changamoto hazikwepeki ni kupambana nazo kadili zinavyokuja.
Usisononeke na maisha mazuri ya wenzio, Pambana usiku mchana, jua mvua utafika hizo level.
No easy man, work hard, God will put the bless. Heshimu watu.

Mkuu nina maswali mawili:

Nataka kujua zaidi kuhusu uuzaji vilipuzi, compressors na madawa. Mtaji, changamoto na faida zake.

Na hiyo ya umiliki wa elution plant. Mtaji (ambao umesema roughly 40M-50M), changamoto na faida zake.
 
mzee niaje?
 
chief naomba nikujibu baadaye...
 
Best nakusoma vzr ,kiasi nakufananisha na best yangu mmoja hivi ,sijui alipotelea wapi ?

Nina Buyer wa Diamond ,uhakika yuko Europe , diamaa kwa bongo ikoje , ( nje ya mada kdg )

Sent using Jamii Forums mobile app

Ila mtu chake jamani unazingua balaa🤭 huyo rafiki yako namjua🤭...! Diamond labda mchek mrangi ana madili hayo!
 
Plants zinahitaji mtaji kiasi gani kuanzisha?
Ukitaka kuanzisha tembelea sehem za kahama na geita upitie walau plants 5! Upate abc ...kwanza kupima tu udongo sample ni hela...30000/-..Sasa imagine wangap wanapima samples zao kujua kiwango Cha dhahabu kilichomo...kukodisha plant 2wks 4m! Na ni foleni sio kawaida..!labd uwe unajulikan
 
Changamoto za plants hua ni nn hasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukitaka kuanzisha tembelea sehem za kahama na geita upitie walau plants 5! Upate abc ...kwanza kupima tu udongo sample ni hela...30000/-..Sasa imagine wangap wanapima samples zao kujua kiwango Cha dhahabu kilichomo...kukodisha plant 2wks 4m! Na ni foleni sio kawaida..!labd uwe unajulikan

Nilisikia ni 2M per 24hrs!
 
Asante. Vp maabara ya upimaji sample za udongo.. mtaji, faida na changamoto zake?
Ndo yale Yale tu Kama results zinapishana Sana na wenzako wanakuhama. ! Huko Sina idea kwakweli...as Sina passion nazo Sana!
 
Back
Top Bottom