Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 1,117
- 3,153
Napita Kinyerezi watu na ndoo kichwani. Nauliza vipi naambiwa mara ya mwisho maji yalitoka January hadi Leo tar 5 March 2023 hayajatoka.
Maboza yanakimbizana njiani kupelekea watu maji majumbani kwao, nimeuliza wanauza maji shilingi ngapi? Naambiwa wanaanzia kuuza lita 2,000 kwa shilingi 30,000 wasio na matenki wanachanga 30,000 halafu gari inapita kwa waliochanga wanawekewa maji,
Niwakumbushe tu Hayati Rais Magufuli aliwahi kwenda Segerea kuzindua miradi akaelezwa kero ya maji, akatoa siku saba kero ya maji iwe imeisha,maji yakatoka hadi alivyokufa nayo maji yakakatika.
Hili lipo chini ya Dawasa Kinyerezi, sijui viunga vingine vya jiji la Dar es Salaam.