Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Ndugu zako kwanini usiwape hiyo idea
Hahahaha, aisee
Jamaa wanafanya colabo mpaka wampige mtu. Hakuna kitu hiki acheni kupoteza watu. Maana hapa watu wanafanya kama vile wanawauzia majini vile, yaaani wewe unachukua mzigo unauza kisha unaenda unachukua mwingine unauza,aaaa acheni hizo.

Hata machinga basi na wao wangekuwa mamilionea,maana matajiri pale wanawapa mzigo bureee ni wao tu kukimbizana na wateja na ngoma inakuwa ngumu.
 
Kwa hiyo hapa siku hz mtu akisupport mada inakuwa ni ushirika wa wizi siyo?
Pole sana mkuu unahsi kila mtu ana mradi wa kirikuu, bodaboda na spices?

Nimekudharau sana asee!
 
Tatizo hapa ni watu kuleta hoja pasipo supporting evidence. Ndio maana wadau wanashtuka. Inakua vizuri unaleta mada halafu unatoa ukokotozi wa Gharama zoote halafu unatuonyesha na process nzima nikimaanisha mzunguko wa pesa mpaka kupata hiyo Mil. 2 kama faida.

Mleta mada najaribu kukusoma kusudi lako la kuleta hii mada nikipambanua na majibu unayotoa nayaona hayana details kabisa. Sasa sijui ulikua unataka nini? Maana iko clear haujaja kuelimisha, kuamasisha sasa sijui umekuja tu kutujulisha kuwa wewe na bro mnapata 2M kila wiki kama ni hilo basi tumekusoma mkuu.
 
Kisima hiyo Chain saw unakuwa unaikodisha au unafanyaje mkuu? Au itakubidi ununue cubic meters za mbao uanze kupasua? Naomba ufafanuzi tafadhali.
 
Kisima hiyo Chain saw unakuwa unaikodisha au unafanyaje mkuu? Au itakubidi ununue cubic meters za mbao uanze kupasua? Naomba ufafanuzi tafadhali.
Mkuu tatizo watu wanasahau kuwa nchi yetu bado bikra katika nyanja nyingi sana, kila kitu ni fursa hapa kwetu the thing is to know how to explore em and extract money from within!

Tunayo mapori mengi sana nchi hii yenye miti ya thamani kupindukia. Kuna vijiji bado vina miti ya asili kama mivule, mininga, mikomba, mikangazi, mikarati, mipilipili, mitondoro, miseni etc yote ni kwajili ya matumizi ya fenicha mbalimbali majumbani mwetu.

Hapa mkoani morogoro miti ya miembe inazidi kutafunwa kila iitwapo leo shehena za magogo zinapakiwa kwenda uchina lakini Maghembe ameona nyani tu!

Mkuu nenda wilayani mathalani kilosa; utapewa muongozo wa kupata kibali cha kuvuna miti kutoka kijiji husika.
Then rudi dar kujua soko na dealers wa mbao ambao wanaweza kuja kuchukua huko kijijini.
Simple!
 

KWELI NCHI YETU BIKRA THANKS MKUU NIMEKUPATA SANA
 
Wakuu biashara ya mbao ninaifaham kiasi bt kwa maelezo ya mtoa uzi sidhani kama nayakubali kwa asilimia 100 labda aje kutoa evidence zaidi.

Kwa uelewa wangu mdogo semi treiler moja la mbao cost zake kila kitu mpaka mzigo ufike dar 23ml lazima zikutoke tu although usipopata majanga ya kibiashara lazima faida utapata tena kubwa tu.

Hiyo ml23 inatoka hapa
Mzigo
usafiri
vibari vyote vya mali asili
 
Asante mkuu japo umekuwa na maelezo ya jumla ninaomba kama unaweza kutusaidia breakdown ya process na cost zikoje. Kwa mfano cost za vibali, mafundi, kununua miti n.k

Natanguliza shukrani
 
Mu-sir nitaelezea kadri ya uzoefu wangu.

Ieleweke kuwa uvunaji wa mbao nnaoongelea hapa ni hard wood tofauti kabisa na mleta mada ambaye nadhani alikusudia biashara ya mbao za kupaulia (syprus).

Kwa hard wood kuna vibari vya kijiji na vibari vya huko maliasili kwa dealer anayesafirisha mzigo mkubwa kwenda dar n.k
Vibari vya kijiji vina limit usisafirishe mzigo nje ya wilaya na kawaida halmashauri inapendekeza ni vijiji gani vinaruhusiwa kuvuna maliasili na huambatana na upewaji list.

So ukitaka kuchakata mbao sharti uuone uongozi wa kijiji na utajadiliwa(sh300k) then utaruhusiwa kuchana mbao sehemu maalum na ikiwa miti ipo ndani ya shamba la mtu basi mtapatana kwa kila mti atleast sh5k.
Kipindi nafanya hii kazi nilikuwa na clients zangu kutoka dar ambao walikuwa wanachukulia mzigo huku porini. Sikuwahi kusafirisha.

Kawaida operata wa chainsaw hulipwa sh700-1000 piece
Chainsaw husqvarna 272 xp inauzwa sh1300k-1600k.
Inatumia petrol,2t&oil chafu.

Tank lake linachukua 0.75ltr na linaweza kuchana pieces5-8.
 
Mkuu kuna mtu namdai anataka kuuza shamba lake huko mafinga ni ekari 2. Kama sikosei lina miti miaka sita kwa maelezo yake. Je, unaweza kusaidia soko?
 
Mkuu mimi pia mpandajinwa miti Njombe naomba uni add kwenye group lenu la upandaji miti kwasasa nipo mbali na nchi ila nina muwakilishi wangu ambaye ananipandia na kunisaidia mashamba uko Njombe, natanguliza shukrani za dhati, msimu80@gmail.com
 
Mkuu mimi pia mpandajinwa miti Njombe naomba uni add kwenye group lenu la upandaji miti kwasasa nipo mbali na nchi ila nina muwakilishi wangu ambaye ananipandia na kunisaidia mashamba uko Njombe,natanguliza shukrani za dhati, msimu80@gmail.com
Nitakutumia mwaliko kupitia mail yako yao.
 
Mkuu kuna mtu namdai anataka kuuza shamba lake huko mafinga ni ekari 2,kama sikosei lina miti miaka sita kwa maelezo yake ,je unnaweza kusaidia soko!?
Naweza kukutafutia soko fasta, lakini hujasema ni kijiji gani mkuu.
 
Wakuu naomba connection ya mtu anayeuza miche mizuri ya mitiki kwa dar es salaam. Na naomba kujuzwa kama miche hii ikipandwa mkuranga itaota.
 
Nimepanda miti 100 wiki jana, kila mche nimenunua sh 300 bei ya jumla.
 
Miarobaini inatoa mbao nzuri sana. Sasa kama mnazi unachongwa mbao, itakuwa muarobaini. Waulize mafundi fenicha mjini Dar wakuambie miguu ya makochi na vitanda iliyobora kabisa wanachonga mti gani.
Mkuu Malila umepanda pia muarobaini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…