The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Kwa sasa nafanya coordination ya upandaji miti kwa wadau 410, wengine wamo humu na wengine wako nje ya jf. Msimu huu pekee tumeotesha miche milioni tatu na ushee, tumeotesha/nimesimamia kuotesha pines na mlingoti katika wilaya za Mufindi, Kilolo,Njombe na Madaba. Bei ya chini bila kupita kwa dalali ni Tsh 70,000/ kwa eka katika maeneo yasiyo na miundo mbinu. Na maeneo yenye miundombinu bei inafika Tsh 120,000/ kwa eka. Miche na manpower naweza kukusaidia kama tunavyosaidiana ktk group letu.
Shukrani kwa mrejesho wa haraka mkuu, naomba usinichoke kwa maswali mengi. Unweza kutuwekea vigezo vinavyomfanya mtu kupokelewa kwenye hiyo group unayo coordinate? Na kama inawezekana inaendeshwaje? Natanguliza shukrani za dhati Malila