Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Habarini watu wa Mungu, mimi ninavutiwa kufanya biashara ya kuuza mbao Nairobi, mtaji kwangu suo tatizo sana, msaada ninaohitaji kwenu ni process za kupata kibali, kama kuna mtu anafaham utaratibu mzima wa kibali au taratibu nyingine zinazohusiana anisaidie tafadhali.
Asanteni sana

Hiyo biashara siijui na sina msaada kwako katika hili. Zaidi ya kukuambia uende mali asili eneo ulipo watakupa process zote, soko umeshalipata lakini.They are good listerner now days.
 
Mimi pia napenda kufahamu kuhusu hii biashara wakuu. Then kwako mkuu kwanin umechagua Nairobi na si local market la hapa kwetu?
 
Wakuu naombeni kujiunga na hili kundi, nipo katika process ya kupanda miti Iringa, nimeipenda hii thread maana kuna doubter alishaanza kunipotosha akili, katika pita pita zangu nikaona hii kitu hapa jamii forum,nashukuru kuwa approved kama member mpya, wenzetu wakenya wanakuja kununua maeneo Iringa sie tumelala tu duh!

Mimi harabari ya miti sijaanza kuwaza leo ila hatimaye sasa nimepata mwongozo mzuri zaidi kutimiza ndoto yangu, mitiki nina shamba njia ya Tanga nikaotesha miche kupitia bwana shamba lakini kutokana na sababu zisizozuilika nika abandon hiyo project ila shamba bado lipo, sasa nguvu yangu nahamishia Njombe nimevutiwa sana na mwanzilishi wa hii thread, mbarikiwe wote katika harakati za ujasiriamali.
 
Uko pm kunabiashara gan.wahun nyie tuu au ndo mwshoo utaper
 
Mimi nigependa kuwahamasisha wanJF kupanda miti ya mbao hasa mbao nyeupe (pines and cypress). Miti hii inasitawi sana sehemu za nyanda za juu kusini.

Mimi nilianza kupanda miti hii kama miaka kumi iliyopita. Nimepanda miti mingi kila mwaka bila kukosa. Kwa sasa ninazo ekari nyingi za miti hii. Vile vile miaka ya karibuni nimepanda eucalyptus.

Wakati naanza kupanda miti mche mmoja nilikuwa nanunua kwa Shs 50 na kuupanda kwa Shs 20. Kwa vile napanda miti mingi (zaidi ya laki moja kwa mwaka) baadaye niliamua kuotesha miche mimi mwenyewe ili kupunguza gharama.

Gharama zaidi ya miche na upandaji ni barabara za moto kuzunguka msitu. Hata hivyo nilinunua ngómbe na kuwaweka kwenye shamba ili wale majani yanayozunguka msitu. Wamenisaidia sana.

Unaweza kupanda miti kidogo kidogo kila mwaka kutumia mshahara wako kama nilivyofanya mimi. Baada ya miaka kadhaa utakuwa na miti mingi na utaweza kuwa unauza miti au kupasua mbao kila mwaka.

Wakuu habari za majukumu. Mimi pia ningependa kupata shamba kuanzia ekari 20 hadi 50 haswa lililooteshwa miti tayari. Wasiwasi wangu ni kupigwa/kutapeliwa. Je ninaweza kufanyaje nipate shamba kiuhalali na kisheria? Ninaomba kama kuna mtu ana shamba tayari maeneo ya Njombe au Kilolo ambaye anaweza kunisaidia kupata shamba kihalali nitashukuru sana.
 
Eucalyptus sio miti mizuri kupanda sababu inakunywa maji Mengi sana na kuleta ukame eneo husika sikushaur upande tena Ila pines, grevillea, casuarina Montana ni bora zaidi.
 
Wakuu habari za majukumu. Mimi pia ningependa kupata shamba kuanzia ekari 20 hadi 50 haswa lililooteshwa miti tayari. Wasiwasi wangu ni kupigwa/kutapeliwa. Je ninaweza kufanyaje nipate shamba kiuhalali na kisheria? Ninaomba kama kuna mtu ana shamba tayari maeneo ya Njombe au Kilolo ambaye anaweza kunisaidia kupata shamba kihalali nitashukuru sana.

CC Malila
KVM
 
Eucalyptus sio miti mizuri kupanda sababu inakunywa maji Mengi sana na kuleta ukame eneo husika sikushaur upande tena Ila pines, grevillea, casuarina Montana ni bora zaidi

Upandaji wa Eucalyptus inategemea na eneo uliko. Kama upo sehemu ambayo haipati mvua ya kutosha basi hiyo miti inaweza kuleta ukame. Sehemu ninayopanda mimi inapata mvua nyingi zinazoletwa na milima.
 
CC Malila
KVM
Bahati mbaya kwa sasa hivi sipo maeneo kwa hiyo ni vigumu kukuelekeza. Naomba umpm Malila yeye mara nyingi huwa anakwenda maeneo hayo.

Ila tu kwa uzoefu wangu wengi wanaouza mashamba yenye miti huwa wamepanda eka chache kama moja, mbili hadi tano. Wanaouza zaidi ya eka 20 ni wapandaji wakubwa na wapo wachache. Ila kwa hali ya sasa unaweza kuwapata baada ya mianya mingi ya mapato kuzibwa. Malila
 
Bahati mbaya kwa sasa hivi sipo maeneo kwa hiyo ni vigumu kukuelekeza. Naomba umpm Malila yeye mara nyingi huwa anakwenda maeneo hayo

Ila tu kwa uzoefu wangu wengi wanaouza mashamba yenye miti huwa wamepanda eka chache kama moja, mbili hadi tano. Wanaouza zaidi ya eka 20 ni wapandaji wakubwa na wapo wachache. Ila kwa hali ya sasa unaweza kuwapata baada ya mianya mingi ya mapato kuzibwa. Malila
Malila Njoo basi utusaidie kuhusu kuuziwa shamba za miti please mkuu.
 
Je, ni miti ya aina gani inafaa kupandwa katika mkoa wa Geita?
 
Malila njoo basi utusaidie kuhusu kuuziwa shamba za miti plsssss mkuu

Ni kweli najishughulisha sana na hii project, kwenye hii project kumeingia vibaka, tena wengine wanapata hata nafasi za wazi za kupiga wasiojua. Hata mimi nimeshapigwa, kwa hiyo najua. Sasa hivi usikubali kununua shamba la familia bila kupata document ya kikao cha familia husika.

Ukisikia shamba la miti linauzwa inabidi uchunguze sana, unaweza kuta muuzaji analiuza sababu lina mgogoro ambao wewe hutauona mapema, shamba la hivyo inabidi utafute ushahidi wa kutosha, au lilikosewa kuoteshwa,au uvunaji wake utakuwa pasua kichwa nk. Ukisikia hili shamba linauzwa na muuzaji anashida sana, fungua macho.

Mashamba yanayouzwa na vijiji achana nayo, yanasumbua sana. Usikwepe kulipa ushuru wa kijiji, kisha chukua pay slip, kila kitu kifanyike ofisini mchana kweupe, na malipo kama ni hela nyingi, pitishia benki.

Naweza kuwasaidia kupata mashamba ya kuotesha miti kwa bei nzuri sababu nafahamu yalipo na mimi nipo hapo, naweza kuwasaidia kupata mashamba yenye miti tayari ( Mufindi/Kilolo/Njombe) katika maeneo nilikootesha mimi, sababu wauzaji wa mashamba ktk vijiji niliko walau naweza kupata taarifa sahihi.

karibuni.
 
Ni kweli najishughulisha sana na hii project, kwenye hii project kumeingia vibaka, tena wengine wanapata hata nafasi za wazi za kupiga wasiojua. Hata mimi nimeshapigwa, kwa hiyo najua. Sasa hivi usikubali kununua shamba la familia bila kupata document ya kikao cha familia husika. Ukisikia shamba la miti linauzwa inabidi uchunguze sana, unaweza kuta muuzaji analiuza sababu lina mgogoro ambao wewe hutauona mapema, shamba la hivyo inabidi utafute ushahidi wa kutosha, au lilikosewa kuoteshwa,au uvunaji wake utakuwa pasua kichwa nk. Ukisikia hili shamba linauzwa na muuzaji anashida sana, fungua macho.

Mashamba yanayouzwa na vijiji achana nayo, yanasumbua sana. Usikwepe kulipa ushuru wa kijiji, kisha chukua pay slip, kila kitu kifanyike ofisini mchana kweupe, na malipo kama ni hela nyingi, pitishia benki.

Naweza kuwasaidia kupata mashamba ya kuotesha miti kwa bei nzuri sababu nafahamu yalipo na mimi nipo hapo, naweza kuwasaidia kupata mashamba yenye miti tayari ( Mufindi/Kilolo/Njombe) katika maeneo nilikootesha mimi, sababu wauzaji wa mashamba ktk vijiji niliko walau naweza kupata taarifa sahihi.

karibuni.

Shukrani kwa kujitolea kutoa elimu ya bure mkuu, najua kama ukipata wafuasi huenda wengine wakawa wateja wako ukatuuzia miche. Kwa sasa heka moja isiyopandwa inaweza kwenda kwa kiasi gani? Na wewe unazalisha miti ya aina gani? Nikinunua miche kwako unaweza kufanikisha upatikanaji wa vijana wa kupanda japo kwa maelewano tofauti kati yao na mimi?

Shukrani.
 
Kwa sasa nafanya coordination ya upandaji miti kwa wadau 410, wengine wamo humu na wengine wako nje ya jf. Msimu huu pekee tumeotesha miche milioni tatu na ushee, tumeotesha/nimesimamia kuotesha pines na mlingoti katika wilaya za Mufindi, Kilolo,Njombe na Madaba. Bei ya chini bila kupita kwa dalali ni Tsh 70,000/ kwa eka katika maeneo yasiyo na miundo mbinu. Na maeneo yenye miundombinu bei inafika Tsh 120,000/ kwa eka. Miche na manpower naweza kukusaidia.
 
Back
Top Bottom