Hongera kwa uthubutu,biashara ya mbao ni nzuri sana na ina faida nzuri endapo utaisimamia na kuikubali na kuvumilia.
Mambo ya kuzingatia.
1. Unatakiwa uwe na usajiri(registration) wa kufanya biashara ya mbao hii utaipata ofisi ya misitu ya manispaa uliko japo kua ni shida sana kupata usajiri (naskia imekua deligated to ofisi za misitu za wilaya) usajiri huu ndio utakao kuwezesha kutambulika na serikali km ume ruhusiwa kununua na kuuza mbao pia usajiri ndio utautumia kukata kibari cha kusafirishia mzigo (T.P)
2. Kwa upande wa mtaji inategemea na malengo yako kama.
i} Nataka kununua miti kuchana na kusafirisha mbao mwenyewe au unataka kununua mbao tu kisha una safirisha
ii} Unataka utoe magari mangapi ya mbao kwa wiki/mwezi
iii} usafiri utakao utumia kusafirishia mzigo ni fuso au semi? maana bei ya fuso iko chini zaid ya semi lakini semi inabeba mzigo mkubwa kuanzia pieces 1000-1500 kulingana na size ya mbao.na fuso inabeba pieces 300-400 kulingana na size ya mbao.
*Mbao zina tofautiana kiwango cha bei kulingana na aina ya mti ila kwa iringa(sina uzoefu nako) miti mingi ni pine.kwa ufupi ni kwamba mtaji usiwe chini ya 4 kwa kuanziA.
3. Mbao inauzwa kwa futi au mita,bei ina tofautiana kulingana na size e.g 1x10 ina bei yake,1x8 ina bei yake, 2x6 ina bei yake, 2x4 ina bei yake.kwa hiyo una takiwa uwe makini na vipimo wakati wa kuchana, kununua, na kuuza epuka sana kuchaniwa mbao ambazo ni under size mfano mbao ya 1x10 wakati wa kupima ikawa 1x9 hiyo tayari ni hasara kwa sababu ukienda kuuza bei itapungua.
Eneo hili la vipimbo ndipo panapo umiza I mean hasara na faida ya mbao ipo kwenye vipimo kwa hiyo unapo peleka mzigo sokoni uwe mjanja na makini sna kwenye vipimo ukienda kichwa kichwa unaibiwa bila kujua.
4. Soko la mbao upatikanaji wake ni mgumu kidogo hasa kwa wageni wa hii biashara kwa sababu biashara hii ni ya kimtandao zaidi na mara nyingi wanunuzi wa mbao wana agiza mzigo kwa order hivyo ni juhudi zako binafsi kutafuta wateja na kuuza mbao zako kwa bei ya ushindani, kwa dar mbao zinauzwa tegeta na biguruni.
5. Epuka kununua /kuchana mbao za mti pori kama hauna kibari maalumu hii ni hatari sana kwa mtaji wako na maisha yako serikali iko macho sana japo kua wajanja/wazoefu wanajua wanafanyaje kusafirisha mzigo wa mbao za asili ila ukidakwa ukashindwa kuwatuliza wahusika unataifishiwa mzigo wako na jela juu. Pia zingatia muda wa kusafirishwa mbao ni kuanzia saa 12 asubuhi mpaka 12 jioni zaidi ya hapo ni kujitaftia matatizo.
6. Mbao zina lipiwa ushuru kila mbao ni shilingi 100.
7. Gharama za mbao ni
Hela ya kununulia mti (kama utachana mwenyewe)
Kumlipa fundi wa kuchana mbao,(kama utachana mwenyewe)
Wabebaji na ushuru na kulipia gari
Changamoto kubwa ya biashra ya mbao ni pamoja na
1. Kucheleweshwa kupata hela yako kwa wakati hapa nina maana kwamba unaweza kupeleka mbao sokoni ila unae muuzia asiwe na hela cash aka kuahidi kukulipa hela yako siku fulani but na asikupe hiyo siku husika (kutapeliwa kuna anzia hapa)
2. Mafundi wa mbao kukosa uaminifu na pia wanaweza wasikuchanie mbao kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali kama una hasira unaweza kukorofishana na watu wengi sna cha msingi ni uvumilivu tu.
Naamini nime eleza mengi muhimu ambavyo ni msaada tosha kwa kuanzia biashara.
kila la heri.
Chinga One.