Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Kwa wale wote wanaohitaji kufanya manunuzi ya mbao kwa jumla na rejareja waniulize,au kufahamu ni mbao ya aina gani itakuwa bora kwa kazi utakayoifanyia .piga 0656 993 992

Njoo ujibu kwanza hayo kabla hatujakubandika mengine.

Nimekubandikia hapo post yake uisome ukiwa umetulia, hajasema atajibu hapa. Amekuweke namba ya simu ili umpigie umuulize maswali yako hapa. Unataka mwenzako alale na njaa kutoa consultation bure?
 
Wanajamii na mimi nimeguswa sana na hii thread. Naomba kuuliza mkoa wa Iringa maeneo ya Ifunda Pine trees inaweza kustawi?
 
Hongera sana! Nashukuru kwa hii post, japo ni ya siku za nyuma kidogo, imenifungua macho kwa kiasi kikubwa. Mwanzoni mwa hii thread mliongelea maeneo ambapo ardhi inapatikana na Malila akaongezea pale, naona hiyo ilikuwa 2012....je kwa sasa unaweza kunisaidia ushauri wa maeneo napoweza kupata ardhi kubwa kwa ajili ya upandaji wa miti, (na mitiki ikiwemo) kwa bei nafuu kidogo?

Shukrani
 
Njooni handeni tupande mitiki tuwe mabilionea kama ifuatavyo, mitiki inakuwa tiyari kuvunywabaada ya miaka 10hadi 20 kwa sasa bei ya cubic mita moja ni 400$ namti wa miaka 10 un acubic mita 5!!!!!kwenye eka mija unaoand miche mia 5!!!!!!!!!
Habari, vipi upatikanaji wa ardhi huko? Naongelea ekari 50 au zaidi kwa pamoja bei zake je? Shukrani
 
Hongera sana!nashukuru kwa hii post,japo ni ya siku za nyuma kidogo,imenifungua macho kwa kiasi kikubwa.Mwanzoni mwa hii thread mliongelea maeneo ambapo ardhi inapatikana na Malila akaongezea pale,naona hiyo ilikuwa 2012....je kwa sasa unaweza kunisaidia ushauri wa maeneo napoweza kupata ardhi kubwa kwa ajili ya upandaji wa miti,(na mitiki ikiwemo) kwa bei nafuu kidogo?...shukrani
Ardhi nzuri kwa kilimo cha Mitiki inapatikana Kisarawe kama Km 50 kutoka Buguruni.Bei inaanzia laki nane kwa eka moja.
 
Ndugu hujatuambia namna ya kupata mashamba kwa sisi wageni katika maeneo hayo, kwa sasa nipo Nyanda za Juu Kusini nimekuja kwa ajili ya hili swala.
 
Ahsanteni wadau kwa elimu mnayoitoa ktk jukwaa hili.

Mkuu Malila nimeku PM. Naomba tuwasiliane.
 
Nashukuru sana mkuu kwa maelezo yako,vp kwa huo mzigo mkubwa wa semi trailer kwa utalaamu wako ukisafirisha kuuza dodoma utakuwa na faida nzuri?,na vp kuhusu garama za usafiri hadi dodoma?

Mkuu milioni 5 vipi inaweza tosha kufanya hii biashara?
 
mkuu milioni 5 vipi inaweza tosha kufanya hii biashara?

Atleast milioni 12 kwa anayeanza. Kuna kodi ya tra takribani 200,000, leseni ya biashara halmashauri takribani 150,000. ada ya maliasili takribani 260,000. kodi ya pango la eneo la biashara(kama si eneo lako), mshahara wa muuzaji, mlinzi na mtu ambaye atakua anafuta mzigo (kama hufanyi we mwenyewe) lori moja ambalo si semitela linachukua takribani pisi 1200, gharama za kukodi lori takribani milioni tatu (inategemea unazitoa wapi na unapeleka wapi) ukichukua mzigo wa milioni 7 faida ni milion 3.5 - 4.

Kila la heri
 
Kiukweli mwanza Mbao znalipa sana Mkuu fanyia huko DSM cna uhakika kma zitatoka haraka sana
 
Jiandae faini kwa kutembea nje ya muda wa serikali kwa mujibu wa sheria
Jiandae faini kuzidisha uzito (mizani) kama mbichi
Jiandae ghalama ya ziada km gari imeharibika au umetoa mzigo porini.
 
Read by the way, the line nimesema nimesikia sio kwamba nimethibitisha.
 
Huuu ni uongo na ukiendelea kuchekewa utaharibu jukwaa letu

Funguka mkuu hueleweki au mgeni jukwaani?.watu tunajifunza kitu hapa kama unasema amesema uongo ukweli wako ni upi sasa? Ferre tunahitaji mengi kutoka kwako mkuu.
 
Back
Top Bottom