Ni kweli najishughulisha sana na hii project, kwenye hii project kumeingia vibaka, tena wengine wanapata hata nafasi za wazi za kupiga wasiojua. Hata mimi nimeshapigwa, kwa hiyo najua. Sasa hivi usikubali kununua shamba la familia bila kupata document ya kikao cha familia husika. Ukisikia shamba la miti linauzwa inabidi uchunguze sana, unaweza kuta muuzaji analiuza sababu lina mgogoro ambao wewe hutauona mapema, shamba la hivyo inabidi utafute ushahidi wa kutosha, au lilikosewa kuoteshwa,au uvunaji wake utakuwa pasua kichwa nk. Ukisikia hili shamba linauzwa na muuzaji anashida sana, fungua macho.
Mashamba yanayouzwa na vijiji achana nayo, yanasumbua sana. Usikwepe kulipa ushuru wa kijiji, kisha chukua pay slip, kila kitu kifanyike ofisini mchana kweupe, na malipo kama ni hela nyingi, pitishia benki.
Naweza kuwasaidia kupata mashamba ya kuotesha miti kwa bei nzuri sababu nafahamu yalipo na mimi nipo hapo, naweza kuwasaidia kupata mashamba yenye miti tayari ( Mufindi/Kilolo/Njombe) katika maeneo nilikootesha mimi, sababu wauzaji wa mashamba ktk vijiji niliko walau naweza kupata taarifa sahihi.
karibuni.