Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

kuna sera/sheria imeanzishwa hivi karibuni kutaka wenye mashamba ya miti wawe wanaomba vibali kabla ya kuvuna miti yao. Jaribu kuitafuta uisome.

Sawa mkuu
 
Kuna sera/sheria imeanzishwa hivi karibuni kutaka wenye mashamba ya miti wawe wanaomba vibali kabla ya kuvuna miti yao. Jaribu kuitafuta uisome.
***
Miti yangu mwenyewe unipangie kuvuna,kwa hasira sipandi./
Kwa binafsi sinaufahamu wa kuwa kila ninapokata natakiwa kuotesha mpya maana ndio zao langu LA Kilimo.
 
Upo hapa hapa Mafinga watu washavuta hela za carbon credit
 
Mimi Nina heka 1 huko mafinga mtili naenda kupanda mwezi January
 
Kuna upcoming tree investors meeting/training in the southerh highland regions of Tanzania (Iringa). You will be exposed to a lit of things guys
 
Niliisikia kutoka kwa jamaa mmoja ila baadaye nikagundua ni tapeli. Kama ni kweli tujuze zaidi.
 
Wazo zuri. Nilipita maeneo ya Sumbawanga hasa Wilaya ya Kalambo,nako kuna mashamba haya japo kwa uchache! Issue kubwa hapa uwe na eneo. Huwezi kukodi kwa vile ni zao la kudumu na la muda mrefu.
 
Nilijaribu zoezi hili nimeishia kupanda hekari 18 tu za pines. Lakin natarajia kupanda zaid nikipata maeneo zaidi maana hilo ndilo tatizo kubwa zaidi.
 
Sijasikia mtu anayepanda mitiki hasa hasa maeneo ya morogoro. Au hamjasikia fursa upande huu?
 
Nimeshakupa mwaliko kupitia mail yako pamoja na wengine walioko kwenye ukurasa huu. Karibuni tufanye mambo.
Mkuu nebu basi tuwekee hapa ukokotozi wa heka 10 kwa mfano, ukianzia na
-Gharama za kununua shamba,
-Gharama za serikali ya kijiji,
-Gharama za miche
-Gharama za kupanda
-Gharama za kuweka mipaka/ikuza/kinga moto
-Gharama zingine

Msaada basi tujazie hapo utusaidie tujipime kaka
 
Kwa kule niliko mimi ni kama ifauatavyo.

A) shamba bei ni, 80k, 90k na 100k, kwa hiyo hapa uchague wewe bei unayo mudu, mfano tuchukue 90k kwa eka.
90k x 10 sawa na 0.9M
B) Gharama za kijiji zitakuwa 9000/ x 10 sawa na 90k
C) 10 x 600 x 100/ sawa na 0.6M
D) Upandaji ni 50k x 10 sawa na 0.5M
E) Usafirishaji wa miche 0.15M
F) Chakula 0.1M
G) kuweka fire break kila mwaka 0.2M
I) Vifaa vya kazi 0.15M

Hata kama gharama zitapishana kidogo na maeneo mengine, lakini ziko katika range hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…