Well said mkuu, hivi ule utaratibu wa hati za kimila uliishia wapi? nasikia ilikuwa 20,000 tu, au hauwahusu wanunuzi wa ardhi yaani mpaka uwe umerithi?Miaka 70! sipo tayari kwa hili. Ngoja niendelee kufanya utaratibu wa kumiliki ardhi kisheria maana hizi projects za muda mrefu ni lazima uwashirikishe watu wa ardhi kikamilifu kabla ya kuanza kupanda miti. Tuliangalie kwa umakini hili swala, watu wengi wamepoteza ardhi kwa kutofuata taratibu za umiliki
Asante KVM,
Nichangie kwa kuleta nyongeza za hapa na pale ili kujazia mjadala wetu. Maeneo ya kupanda miti yaliyosahaulika ni Kilolo, Mfindi,Mby vijijini, Makonde plateau.
Tumetaja sana pines, cyprus, teak,eucalyptus, tumesahau acrocarpus kwa ukanda wa baridi na Msederela kwa kanda za joto kiasi.
Hatujazungumzia mbegu, mbegu bora za Pines kwa sasa ni Tatizo sugu.Tangu mwaka jana kituo cha Iringa wameshindwa kuzalisha, kwa hiyo pines/cyprus zinaandaliwa kienyeji na vijana huko vijijini.Kwa sasa pines za uhakika zinapatikana Nairobi, ila bei imesimama.
Mwaka jana tulipata taabu sana ya tubes, ila mwaka huu walau zipo pale TFA Iringa, bei iko juu. Ukiwa na usafiri wako, ni bora kununua Dar ukasafirisha. Dar ni Tsh 5000/ kwa kilo na TFA Iringa ni 6500/ kwa kilo.
Ili kupunguza gharama za kitalu, watika miche mapema, miezi mitano kabla ya msimu wa kupanda haujafika.
Kama unataka ardhi kubwa,Makete usiende, ni kazi ngumu kupata eka 50 za pamoja zinazofikiwa na miundo mbinu. Utapanda milimani ambako utashindwa kuvuna. Na maeneo mazuri yaliyobaki bei iko juu. Ludewa/Wino/Lupembe/Mfindi kusini huko bei poa.Kilolo bei inaanza kupanda.
Kwa wale wanaonunua miti na ardhi, wawe waangalifu, vijijini unaweza kuta miti ni mtu mwingine na ardhi ni ya mtu mwingine.
Asante, tuendelee kukata issue.
Kiongozi unaonekana unafahamu mengi juu ya miti hapo aithee, NAOMBA KUJOIN naamini nitafamu mengi nitakapopata mawasiliano yako... Email yangu ni waggmwz@gmail.com
well said mkuu, hivi ule utaratibu wa hati za kimila uliishia wapi? nasikia ilikuwa 20,000 tu , au hauwahusu wanunuzi wa ardhi yaani mpaka uwe umerithi?
Mkuu mbao aina gani,na za wapi? Mninga, Mvule, Mtondoro, Mwarobaini, Mwembe, Mnazi, Mpodo, Treated au zipi? Funguka upewe data.
Mbao aina gani? Softwood au hardwood?
Mbao za Mwarobaini zinasoko?
Mninga ndo target
Zina soko ile mbaya, ile miguu minene ya vitanda vinavyouzwa mjini sasa hivi mingi ni miarobaini.
Kama unataka mninga na jamii yake inabidi ujipange vizuri, unaweza kuwaletea watu mzigo toka porini, sio kazi ya kuingia kichwa kichwa mkuu.
Mkuu hivi Mwarobaini unachukua miaka mingapi hadi kufikia kuvunwa kwa mbao?
Kama eneo lina maji maji unaweza kuvuna mbao baada ya miaka 8 na kuendelea, kama eneo lina udongo mgumu basi hesabu ni baada ya miaka kumi. Taabu ya mwarobaini ni kupata pingili ya urefu wa ubao unaotakiwa.
Nmekusoma mkuu bt bdo cjapata jibu la swali bei zkoje town?
Ni kweli mkuu kwa miaka hiyo bora kupanda mikaratusi tu nilifikiri ina shortcut kama miaka mitatu tu hivi