Muuzaji Mkuu
JF-Expert Member
- Jun 18, 2022
- 893
- 2,001
Natumaini ni wazima wa afya watumiaji wote wa jf.
Leo nitaandika kila kitu nachojua kuhusu biashara ya mbao laini zinazotokana na mti aina ya pine.
Nitazungumzia kuanzia manunuzi ya miti kutoka kwa mkulima hadi namna mbao inamfikia mtumiaji wa mwisho.
Kabla sijaendelea ningependa kuweka vigezo muhimu ambavyo andiko langu litazingatia ili nieleweke vizuri.
Andiko langu litazingatia vigezo vifuatavyo:
•Aina za mbao
Mbao laini za miti aina ya pines.
•Vipimo vya mbao
Mbao fupi Yaani mbao za ft 12.
•Eneo nitakalozingatia
Mkoa wa njombe hasa eneo nilipo.
•Wafanyabiashara Binafsi
Watu binafsi wanaotaka kufanya hii biashara.
Baada ya kuona vigezo ambayo andiko langu litazingatia,sasa twende kwenye kiini cha andiko moja kwa moja.
Kwanza kabisa kabla hujaanza hii biashara ya mbao laini za miti aina ya pines lazima ujue na kuelewa mnyororo mzima wa thamani na makundi muhimu yanayohusika mpaka mbao zinamfikia mtumiaji wa mwisho.
Ni muhimu kuelewa huu mnyoror wa thamani na makundi muhimu yanayohusika kukamilisha mchakato mzima ili ujue wapi utajipachika kulingana na malengo yako pamoja na mtaji wako.
Hapa chini nimekuwekea makundi muhimu yanayounda mnyororo mzima wa thamani wa mbao laini za mti aina ya pines.
1.Wakulima wa miti aina ya pines wa mkoa wa njombe.
2.Wafanyabiashara wa Mbao wa mkoa Njombe.
3.Wafanyabiashara wa Mbao wa mikoa mingine kama Dar es salaam.
Hapa chini nitachambua kundi moja baada ya jingine lakini nitajikita zaidi kwenye kundi namba 2 & 3 kwasababu ndo lengo kuu la hili andiko.
1.Wakulima wa miti aina ya pines
Hili ndo kundi linalotuanzishia mnyororo wetu wa thamani wa hii biashara ya mbao kwa kupanda miti,kuihudumia hadi inakomaa tayari kwa kuvunwa.
Nilitamani kulichambua hili kundi kiundani kuanzia:
•Namna ya kupata ardhi bora na bei rafiki kwaajili ya kupanda miti hii aina ya pines mkoa wa njombe.
•Namna ya kuchagua mbegu bora za kuwatikia hmiche ya miti ya pines.
•Namna ya kuandaa viliba,vitalu na kuwatika miche ya miti ya pines.
•Namna ya kuipanda miche iliyo tayari shambani kwa ustadi wa hali ya juu.
•Namna ya kuihudumia miti yako kwa ubobevu mpaka inakomaa tayari kwa kuvunwa.
Pia nilitamani nizungumze fursa zinazotokeza kutoka na hili kundi mfano:
•Maduka ya mbegu bora za miti,viliba na vitu vyote vinavyohusika kwenye kupanda na kuhudumia miti.
•Kuanzisha bustani za miche ya miti ya pines
•Kuuza mbolea ya samadi kwaajili ya kuwatikia miche na kupandia miti.
•Vibarua vidogo vidogo kwa vijana wasio wavivu kama kuchimba mashimo ya kupandia,kupiga benderesi mashamba ya miti nk.
Lakini sitazungumzia haya leo kwasababu lengo letu leo ni kuwa wafanyabiashara wa mbao na sio wakulima wa miti ya mbao.
2.Wafanyabiashara wa mbao mkoa wa Njombe.
Hili ndo kundi linalofuata baada ya wakulima.
Lakini kabla sijaendelea ningependa kukwambia kuwa hili kundi pia limegawanyika katika makundi mawili ambayo ni:
a) Wafanyabiashara wa mbao mbichi
b)Wafanyabiashara wa mbao kavu
Ebu tuaze kuliangali kundi moja baada ya jingine ili uone wapi unaweza kujipachika kama unataka kufanya hii biashara kwa njombe.
a)Wafanyabiashara wa mbao mbichi.
Hawa ni wafanyabiashara wanaonunua miti kwa wakulima,kisha wanachana mbao na kuziuza zikiwa mbichi kwa wafanyabishara wa mbao kavu (maarufu kama wamiliki wa yadi za mbao)
Kuanza kufanya biashara katika kundi hili hakuhitaji mtaji mkubwa sana lakini kunahitaji umakini mkubwa sana kwasababu ukikosea kidogo kwenye gharama za unendeshaji unapata hasara.
Hapa chini nitakuwea kila kitu unachotakiwa kukijua kama unataka kufanya biashara katika kundi hili.
Vitu unavyotakiwa kuvijua ni kama vifuatavyo:
•Mtaji wa kununua miti na namna ya kuinunua miti.
•Vibali muhimu vya serikali
•Gharama za uendeshaji
•Bei ya kuuzia mbao mbichi inayotembea sokoni
Hapa chini nakuchambulia kipengele kimoja baada ya kingine.
•Mtaji wa kununua miti na namna ya kuinunua.
Ili kuanza hii biashara jambo la msingi kabisa lazima uwe na mtaji wa kununua miti.
Sio lazima ununue msitu mzima ila angalau uwe na pesa ya kununua miti ambayo ukichana na kuuza mbao zako na wewe unabaki na faida kidogo.
Mfano,ukiwa na millioni 5+ unaweza kununua miti ya kutosha kuchana na wewe kukuachia chochote kitu.
Baada ya kuwa na pesa yako tayari ya kununua miti unaweza kuwatafuta madalali wa miti au wewe mwenyewe ukaanza msako kwa wakulima mpaka unapata miti ya kununua.
Jambo la msingi la kuzingatia hapa kabla ya kununua miti:
*Hakikisha miti ina umri wa kuanzia miaka 10+,hii itakusaidia kupata miti iliyokomaa vizuri.
*Hakikisha miti ina ujazo unaelewaka sio kishamba kizima miti ipo kama milunda (nguzo nyembamba)
*Hakikisha unajadiliana bei na mkulima kwa kuzingatia hivi vigezo:
-Eneo miti ilipo kwasababu kama ipo bondeni sana gharama za kutoa mbao huko zitakuwa kubwa
-Ujazo na idadi ya miti katika shamba,usikubali tu kukadiliwa ingia shamba hesabu mti mmoja mmoja.
*Hakikisha mnapeana mkataba wa mauziano ya miti kati ya wewe na mkulima.
•Vibali muhimu vya serikali
-Barua ya serikali ya mtaa inayothibitisha ununuzi wa msitu wa miti
-Kibali cha kuvuna misitu wa miti ya mbao kibishara kutoka kwa afisa misitu wilaya
NB:Hivi vibali sio muhimu sana kwasababu mara nyingi miti inaunwa vijijini huko ndani ndani hao maafisa mda wa kuja huko hawana.
•Gharama za uendeshaji
Hapa chini nitakuandikia gharama zote ambazo unatakiwa kujipanga nazo ili uweze kufanikisha kuchana mbao zako hadi kuuza.
*Kudondosha miti
Hapa utakodi mtu wa chainsaw akakudondoshee miti na kuikata vizuri ili iwe magogo.
Mfano hapa nilipo ni Tsh 12,000/= kwa mjari wa mafuta wa chainsaw.
*Mtu wa kupima miti
Huyu kazi yake ni kumsadia mtu wa chainsaw kupima miti katika urefu wa ft 12 ili kukata magogo ya kuchania mbao.
Mfano hapa nilipo huyu analipwa tsh 8,000/= kwa siku.
*Kukusanya pile za magogo
Baada ya miti kudondoshwa na kukatwa katika vipimo vya magogo ya ft 12 lazima yakusanywe katika piles (vilundo) mbali mbali tayari kwa kuchanwa.
Mfano: Hapa wanakusanya tsh 200/= kwa pingili moja ya gogo.
*Bei ya kukodi mashine ya kuchania mbao (Amec)
Hapa utakodi mashine ya kuchania mbao ambayo inaitwa amec.
Bei za kukodi mashine zinajumisha na mafundi wa kuchana humo humo kwasababu mmiliki wa mashine ndo anawalipa mafundi wake.
Lakini bei ya kukodi mashine inalipwa kulingana na idadi na size ya mbao amec imechana.
mfano hapa nilipo bei zipo hivi:
1×8~800/=
1×10~1000/=
2×6~800/=
2×4~700/=
2×3~500/=
2×2~500/=
1×4~500/=
1×6~700/=
Ko baada ya amec kumaliza kuchana mtafunga hesabu kwa kuanglia size za kila ubao na idadi zake kisha mtazidisha na bei hizo juu kujua mkodishaji amec analipwa sh ngapi
Pia kumbuka hizo bei juu zinajumuisha na mafundi wa kuchana kabisa wao huwa wanajua wanalipanaje na boss wao ambae ni mmiliki wa mashine.
*Kusafirisha mashine ya kuchania (amec)
Kuipeleka mashine ya kuchana porini ni gharama zako.Tena hapa unatakiwa kuandaa gharama za wapakiaji,msafirishaji na washushaji kule porini.
Gharama sio kubwa sana maana mara nyingi guta ndo huwa zinatukima na kinachoangaliwaga ni umbali wa mashine inakoenda.
*Kusomba mbao
Baada ya mbao zako kumaliza kuchanwa lazima zitoke huko porini na mara nyingi zinakuwa bondeni ambako lazima watu wabebe mabegani kuzileta juu ambapo gari inaweza kupakia.
Hii igharama inachajiwa kulingana na size ya ubao na umbali wa kuzisomba.
Siwezi kuweka bei kwasababu zinategemea sana makubaliano yako wewe na vibarua wa kusomba.
*Wapakiaji na washushaji wa mbao kwenye gari inayotoa mbao zako porini.
Baada ya mbao kusombwa lazima zipakiwe ili ziende kuuzwa kwenye yadi za maboss wanaonunua mbao kavu.
Hapa kuna vibarua wa kupakia na kushusha lazima uandae hesabu yao.
Hii gharama nayo ni makubaliano mara nyingi kati yako wewe na vibarua wako.
*Ghari inayokusombea mbao zako kutoka porinu kupeleka yadi kuuzwa.
Hapa napo gharama huwa ni makubaliano katika yako wewe na dereva wa gari.
Mara nyingi inategemea umbali na ukubwa wa gari inayoenda kupakia.
Ghari zinazotumika hapa ni canter za tani tofauti tofauti.
Nb: Kwenye hizi gharama za uendeshaji kama una uhisano mzuri na maboss wanaonunua mbao zako mara nyingi huwa wanatoa hii pesa kisha mnakatana kwenye hesabu za mauziano ya mbao.Ndo namna vijana wengi wanaendesha hii biashara huku njombe.
•Bei ya kuuzia mbao mbichi yadi za maboss
Hapa hakikisha maboss wa yard za mbao hawakukamui sana kwenye bei zao za kununulia ili na wewe ubaki na kitu.
mfano hapa nilipo bei zinazotembea sahizi ni:
1×8~3500/=
2×6~3500/=
2×4~2500/=
2×3~1600/=
1×6~2000/=
1×4~500/=
2×2~500/=
1×10~8000/=