Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

UZURI WA NGOMA UINGIE UICHEZE MWENYEWE

Biashara hii inayo faida sana pia ziko changamoto zake.. nilishawishika nikaamua kufungua nikamuweka mtu ila ilikuja kurudisha mtaji wangu (gharama za kununua vifaa pamoja na kodi) baada ya miezi 13.
 
Kupata 30K au 40K kwa siku inawezekana ila HAINA HUALISIA ... Tokea nianze hiyo biashara sijawahi kuletewa 40K kwa siku .... wastani ni 15K mpaka 25K kwa siku.
Ungekuwa unaifanya wewe bila kumuajiri mtu ingefika walau kiasi gani kwa siku? Au jamaa alikuwa pesa yote anayoipata alikuwa anakupa yote bila kukata cha juu?
 
Biashara moja ya kiboss sana.
Tafuta ps3 tatu na ps4 moja na ps2 moja. Then tv 4 za inch 32 kwaajili ya ps3 nanps4 na tv moja inch 22 flat kwaajili ya ps2.
Chukua kibali ambacho ni 20k kwa miaka miwili. Anza kula faida ya 20k j3 hadi j5 then 30k to 40k alhamisi na ijumaa. 50k jmos na jpili.
 
Ungekuwa unaifanya wewe bila kumuajiri mtu ingefika walau kiasi gani kwa siku? Au jamaa alikuwa pesa yote anayoipata alikuwa anakupa yote bila kukata cha juu?
Mahesabu yanajulikana ukikaa mwenyewe ni bora zaidi!!
Huwa kwa siku inafanya kazi masaa sita
TV ziko 3 .. bei ya kuchezesha kwa dakika 15 ni mia tano ... kwa hiyo ndani ya lisaa limoja utapata 6000 kwa Tv zote tatu ... ukiwa na magame mazuri ( kila baada ya miezi mitatu ubadili magame) kijiwe hakitakauka wateja
 
Biashara moja ya kiboss sana.
Tafuta ps3 tatu na ps4 moja na ps2 moja. Then tv 4 za inch 32 kwaajili ya ps3 nanps4 na tv moja inch 22 flat kwaajili ya ps2.
Chukua kibali ambacho ni 20k kwq miaka miwili. Anza kula faida ya 20k j3 hadi j5 then 30k to 40k alhamisi na ijumaa. 50k jmos na jpili.
Haina uhalisia buddah!! Kumbuka WATEJA WAKO WENGI NI WATU WASIO NA KAZI ... kupata 20 kwa SIKU SI MCHEZO ... naongelea uzoefu ... hahahha eti 50k hahahahhahaha haya fungua uanze
 
Kibali cha bodi ya game gharama zake ziko vipi?
Mwaka wa pili huu KODI INAYO NIHUSU NI KODI YA FRAME TUUU ... naongelea uhalisia!! Frame inafunguliwa saa tisa inafungwa saa 2 au saa 3 usiku ... hiyo bodi ya game hata siijui ..sina kibali chochote ... WALIKUJA SERIKALI ZA MTAA NIKAWAPA 20K WAKAONDOKA NA BIASHARA INAENDELEA MIAKA MIWILI SASA ... utasumbuliwa na baadhi ya wazazi lakini haina maana usikilize maneno yao..kuwa mwepesi kuwasikiliza ila puuzia ..maana ni wajibu wao kulinda watoto wao!!

KIUHALISIA HAMNA BODI YA GAME AU TRA WATAOPITA KUANZIA SAA TISA AU SAA KUMI ....
 
Back
Top Bottom