Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Ukitaka ufanikiwe kibiashara uwe na passion nayo na uijue vizuri...

Mara nyingi ukiiga biashara kutoka ni ngumu sana... Good luck

Usisahau ukitaka playstation 3 nitafute nikuuzie na cd zake.. Maana umri umenitupa mikono, mishe za maisha nyingi sana nakosa muda wa kuicheza
Mkuu shingap nikutengee?
 
Mkuu kama wewe ni great thinker usifanye hii biashara, naichukia sana, inafanya watoto wawe wajinga sana, Huu utandawazi unawaathiri sana watoto, make wanatoroka shule na kwenda kucheza hizo game, usiangalie tu pesa, au uweke sheria kwamba masaa ya shule hakuna mtoto kusogea hapo,
Mtoto kama hana akili hana akili,nenda kwny shule za international watoto wanacheza michezo kibao, computer games,playstation, tatzo watoto wenu uswahilini wana ulimbukeni navyo, na sio wanaotooka shule ndo wanaenda game, wapo wanaoenda mabondeni kucheza kamali,wapo wanaoenda kwenye mabanda ya picha, pooltable, na kuna ambao wenye akili mbovu km wewe wanaosema huo mchezo ni kamali.
 
Uko arusha pande zipi? Mi mwenyewe ndio kazi yangu hio, mi npo Dar.
 
Good

Katika ukuaji wangu sikua mpenzi wa michezo ya kutoa hela but now ninapotafutia riziki nimeona kuna fursa kama hii.
Tatizo ukiacha TV Siuji kingine kinachohitajika Katika kucheza game.

Msaada wa vitu muhimu na approximated prices zake?

Shukrani.
 
Mkuu. Hope sijachelewa kukujibu hapa. Mimi binafsi nafanya hii biashara na ki ukweli inalipa kama uko makini na unajua kuhusiana na games za watoto. Binafsi nilianza na mtaji wa TZS 2 milion. Mimi ninachezesha Play Station 3 na Xbox One. NIna Play Station 3 tatu na X box 1. MAuzo kwa siku ni kati ya TZS 25,000 mpaka 35,000 (weekend ndio kunakuwa na hela zaidi). Play Stations zangu nimezi 'chip' kule kariakoo..zina games ndani, games latest na nilipata hii service kariakoo. Biashara hii inategemea na maeneo ila all in all, inalipa sana ukichukulia watoto wanapenda video games na wengi wao hawawezi ku afford kununua. Changamoto pia zipo ila ndio part ya biashara. Ukitaka maelezo zaidi nitakupatia..all the best mkuu, karibu kwenye ujasiliamali
Oyi...Nahitaji namba yako mkuu, Kuna mdogo wangu anataka kufanya iyo biashara...
 
Kwanza wanavyuo wengi wana pc. So games wanatembea nazo kwenye mabeg daily ni wazo zuri ila hamishia mtaani, mwanachuo hawez kutoa hela kcheza game wkt anaweza kuliweka kwenye pc yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nina ofisi ya PlayStation so kipindi cha likizo hichi, kama kuna MTU anaP3 imekamilika, aje aweke kwenye ofisi tukubaliane kwa wiki nampa buku kumi. Pia kwa upande wa mchango wangu juu ya hii biashara inalipa ukipata maeneo mazuri, ila kwa Swazi bei ni chini, ila kwa maeneo ya kishua kwa mechi inafika jero au buku, mtaji ni mkubwa kwa maama uwe na PS, TV, angalau 2 n na kuendelea.
 
Mimi nina ofisi ya PlayStation so kipindi cha likizo hichi, kama kuna MTU anaP3 imekamilika,aje aweke kwenye ofisi tukubaliane kwa wiki nampa buku kumi.Pia kwa upande wa mchango wangu juu ya hii biashara inalipa ukipata maeneo mazuri,ila kwa Swazi bei ni chini,ila kwa maeneo ya kishua kwa mechi inafika jero au buku, mtaji ni mkubwa kwa maama uwe na PS,TV, angalau 2 n na kuendelea
Na kuhusu swala lakodi likoje mkuu?
 
Ok, mkuu vipi kwa experience yako ni ganes gani inabidi uwe nazo ili kuweza kukidhi mahitaji ya wengi?
 
Back
Top Bottom