Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Mimi nina ofisi ya PlayStation so kipindi cha likizo hichi, kama kuna MTU anaP3 imekamilika, aje aweke kwenye ofisi tukubaliane kwa wiki nampa buku kumi. Pia kwa upande wa mchango wangu juu ya hii biashara inalipa ukipata maeneo mazuri, ila kwa Swazi bei ni chini, ila kwa maeneo ya kishua kwa mechi inafika jero au buku, mtaji ni mkubwa kwa maama uwe na PS, TV, angalau 2 n na kuendelea
Vipi ni games gani zinazochezeka sana?
 
Nataka kuanzisha biashara ya video game kiosk. Naomba muongozo wa vifaa na game zipi pendwa.
 
Nataka kuanzisha biashara ya video game kiosk. Naomba muongozo wa vifaa na game zipi pendwa.
 
Watakuja wataalamu ila ushauri wangu,andaa business plan kwa utulivu sababu hio ndo itakua msingi wako.
 
Unataka kununua nini Consele yani playstation 2,3,& 4 au PC za gaming tuanzie apa.
 
Muda wa kufungua uweangalua kuanzia saa tisa kama ni uswahilini. Angalia usije ukakutana na mama wa mtaani wakikufungia kibwebwe mpaka kwa mwenyekiti wa mtaa,ofisi ya kata, watoto hawaendi shule wanashindia kwenye ps.
 
Wanapenda games za mpira, Magari, GTA, na baadhi ya mission.

Na ps3 Ina make sense zaidi Zama hizi.
 
Unataka kuanzisha maeneo gan mjini Dar, Arusha au kijijini huko Morogoro wap?
 
Game la mpira FIFA, Mortal combat, GTA, magemu ya magari kama need for speed, etc
 
Habari wadau,

Binafsi nimepata frame maeneo ya soweto shukrani centre, nina tv za chogo mbili (nilitaka kutafuta flat ila wakanishauri udokozi wa TV za flat upo juu sana kwenye frame za mbeya especially maeneo ya uswahili )na PS 2 mbili, kuna kijana nimempata pia asimamie..

Sasa nilipata vyote hivi standby nimeviweka ila sijajua pros and cons za hii biashara...naomba mwanga kwenye yafuatayo:

- Nianzie wapi kupata vibali rasmi wa biashara hii
- Faida na changamoto za biasghara
- Nipo location karibia na shule, natumai ni soko zuri ,je vipi kuhusu serikali za mtaa kwa walio jaribu hii biashara
- Mida mizuri ya biashara
- Ushauri wowote wa kunipa nikiwa nataraji anza hii biashara

Asanteni
 
Kama upo karbu na shule hutaruhusiwa kufungua mpaka sa8 yan mda wa masomo ukiisha. Haina process zozote wewe ni sawa na machinga tu.
 
Uwe na PS kama 4 hivi pamoja na biashara nyingine kwaajili ya front office kama kupiga passport...kuburn CD e.t.c ili uweze kufanya shughuli zako bila bugudhi
 
Biashara safi sana ata mimi binafsi nimekuw na wazo ilo tupeane ushauri na mawzo zaidi mpambanaji.
 
Jiandae, nasema tena jiandae, narudia tena kwa msisitizo jiandae kweli kweli maana zile pad za kuchezeshea utanunua kila leo maana zinakufa mapema mno na pad moja inauzwa kati ya elfu 10 mpaka 15.

Kila la kheri ni bishara ina vijisenti vya kununulia chumvi nyumbani endapo ukipata wateja wa kutosha, pia games zako ziwe latest mfano sasa hivi tuko PS4 na sio PS2 tena kama zamani.

Ila kumbuka kuwa wateja wako wakuu watakuwa ni wale watoto watukutu wasioipenda shule.

Kwa namna fulani ni biashara isiyopendwa na jamii kwa sababu ofisi yako huwa ndyo chimbo lao la kujifichia na huwafanya wawe wadokozi wa chenji nyumbani pale wakosapo pesa ya kuja kuchezea game!
 
muda wa kufungua uweangalua kuanzia saa tisa kama ni uswahilini,
angalia usije ukakutana na mama wa mtaani wakikufungia kibwebwe mpaka kwa mwenyekiti wa mtaa, ofisi ya kata, watoto hawaendi shule wanashindia kwenye ps.

Hii inatokea sana wakishaona kijana anapata pesa basi utasikia anafuga majonzi (chimbo)
 
Back
Top Bottom