Niliwahi kufikiria kuwekeza 2.6mil ( je itatosha)kwenye hii biashara wakuu... lakini sina uzoefu nayo wala taarifa sahihi inalipa vipi...ningependa siku moja nimpate mtu anayeifanya au aliyewahi kuifanya anipe muongozo... Asante
2.6 mil hii ni kwa kodi ,ps4 mbili ps3 moja, tv flat 3, viti na n.k
Sikia.
*Ps4 chukua moja ni 650k. Chukua iliyochipiwa ndo inafaa kwa biashara.
*ps3 chukua 2 kwa 320k kwa kila moja.
*ps2 chukua 2 kwa 130k kwa kila moja.
* tv chukua 2 za inch 32 kwajili ya ps3 na moja ya inch 42 kwaajili ya ps4. Nenda kwa wapemba mbweni utapata inch 32 kwa 300k na inch 42 kwa 450k za mtumba. Za mtumba zitadumu muda mrefu sana. Nasisitiza usinunue za dukani ni hasara.
*chukua inch 22 kwaajili ya ps2. Vilevile za mtumba.
* nunua gaming pc used kwa 350k. Tafuta hawa jamaa wanaitwa camara huwa wanazo. Chukua na monitor ya inch 22 au tv yenye hdmi au vga port. Hii itakusaidia kuweka games zenye kuharibu pad mf. Mortal kombat x au xl au 11. Pad za pc ni ngumu na gharama yake ni 8k pad moja k.koo.
*ps4 na ps3 weka games za mpira na mission ambazo haziharibu pad. Pc tia game za ngumi na zenye kuharibu pad.
BEI
*Ps3 na ps4 mpira ni 500 kwa dakika 10
Ps2 mpira mechi 2 500 na ni dakika 10
*games zingn za mission ni dakika 15 kwa 500 kwa ps3 na ps4 na dakika 30 kwa ps2.
LOCATION*
tafuta sehemu yenye watu wengi hasa vijana na yenye usalama. Fremu ni kati ya 50k hadi 70k. Usiogope itakulipa tu.
* dumisha usafi na kama unamweka mtu basi mlipe kwa siku elf 5 mpaka elf 7 kwa siku kutegemea na mahesabu anayokuletea.
* fanya mwenyewe kama mwezi hivi ndo umpe kijana. Na uwe muda mwingi unapiga jicho maana wakizoea huwa wana tabia ya udokozi.
* biashara ikikubali weka cctv camera ni kama 450k kila kitu. Itasaidia usalama na pia kum monitor kijana.
*VIFAA VINGINE
*stabilizor ni muhimu sana kwaajili ya kulinda vifaa vyako.
*pads ni za kuchunga hasa za ps4 maana ndo kikwazo kikubwa cha biashara hii.
*kibali toka serikali za mtaa ni 20k tu na hakuna kenge atakaye kusumbua
●muda wa kufungua ni saa 3 asubuhi hadi saa 5 usiku. Ila siku za shule hakikisha madogo hawaingii chini ya saa 7 mchana.
● kwenye ps4 jaribu kuweka hata kijisofa itaongeza hadhi.
****** FAIDA ********
* ukifikia hayo juu jiandae kula kuanzia 20k hadi 30k kwa siku za kawaida na 40k kwa siku za weekend.
KUNA WATU WANAPENDA KUONGEA VITU WASIVYO VIJUA. KAMA HUJUI KITU NI BORA KUKAA KIMYA