Biashara ya mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo n.k)

Biashara ya mifugo (ng'ombe, mbuzi, kondoo n.k)

mkuu salama kabisa mambo yamebana sana kwa sasa,
hela za laana mimi huwa sizitaki kabisa ndio maana tunajaribu kumuelewesha ndugu yetu hapa kuhusu hizi biashara za kitapeli, huko kongwa, mpwapwa vijijini kuna wahuni huwa wanapeleka mafuta ya taa kubadili na mahindi daaa yani lita moja inabadilishwa kwa debe la mahindi. Wenye matractor nao huwa wanayapeleka huko kipindi cha kilimo then hekari moja inalimwa kwa gunia kadhaa za mahindi au maharage na wanakijiji hawana 30,000 ya kulimia hk 1 so inawabidi tu wakubali... itatuchukua muda sana kuja kuibadili tz yetu kwa mitindo ya namna hii

Mkuu suluhisho ni wao wakulima kuwa katika vikundi na kuwekeana mikakati ya uuzaji wa mazao, na kingine wawe na shughuli zingine Mbadala kama Ufugaji wa kuku, Nyuki, Vikundi vya kuweka na Kukopa,
 
Muhunze wilayani Kishapu kuna mnada wa ng'ombe pale very easy we kama unalo soko la kuuza hao ng'ombe zako, nenda zako pale kanunue kama bado hazijafikia idadi utakayo. kuna minada kibao ya ng.ombe mfano Sanga, Maswa n.k isipokuwa kipindi malisho mengi na bei iko juu, lakini kipindi cha ukame bei ubwete.

Maelezo mengine kama wanafanyaje nini na nini niPM, hakuna mbinu chafu, hamna wa kukusumbua, hamna kibali wala nini.

hakuna usanii kwenye biashara hio.ng'ombe wananuliwa minadani hasa kanda ya ziwa.
Unaweza mnunua ngombe kwa shs 200,000,kisha unamnenepesha,chakula ni mashumu ya pamba na pumba za pamba .vyakula hivi unavipata toka kwenye oilmill zilizotapakaa mwanza,shinyanga,geita,simiyu.
Ng'ombe ananenepa kwa mda wa miezi mitatu .
Ukimfikisha pugu utamuuza hadi 700,000.
Gharama ya kumlisha ng'ombe mmoja kwa mda huo haizidi laki moja.
Usafiri hadi pugu ,kuna mafuso au semi yakipeleka mizigo kanda ya ziwa au kongo yanarudi tupu .waweza kodi fuso kwa gharama haizidi laki nne,kama unang'ombe chini ya 20.
Kama una ng'ombe zaidi ya hapo unachukua semi trail au pulling ,nayo gharama haizidi laki sita.
Biashara haina cha leseni ni kibali tu na sidhani hata kama wanalipa kodi hawa jamaa.
Wakati mwingine wacomoro wanakufuata hadi sehemu unayolishia ng'ombe mnafanya biashara na yeye anapakia ng'ombe na kusepa.
Inalipa ,nimeshuhudia vijana wadogo wanazungusha mamia ya mamilioni kwenye biznes hii.ukimuona anaendesha baiskeli unamuona wakawaida wakati he is worth even 500 millions.
 
Maada endelevu kama hizi ndio zilinifanya nijiunge JF, watu wanatumia vichwa kufikiri na sio kufugia nywele. Nakiona kizazi cha wajasiria mali kinakuja kwa kasi. Mwenye data za mazao yatokanayo na mifugo zaidi ya nyama atumwagie tafadhali. Viwanda vya ngozi, kwato au utafiti wowote uliofanywa karibuni kwa hii sekta. Ninachojua Tanzania ni nchi ya tatu (3) barani afrika kwa wingi wa mifugo. Niko tayari kusahihishwa iwapo naipotosha jamii.
 
mkuu mimi ningekushauri ufanye jambomoja.

- umefika wakati tuwe tunafanyabiashara zenye tija, biashara zenye faida na biashara ambzao hazina usanii.

- biashara kama hizi zina usaniimwingi sana
1. Kununua mazao na kwenda kuyauzasehemu nyingine

2. Kununa kuku na kwenda kuziuzasehemu nyingine

3. Kununua ng'ombe na kwenda kuziuzasehemu nyingine

hizi biashara lazima uwe msanii wahali ya juu kuweza kuzifanya na si kwamba zinahitaji akili bali zinahitajiusanii.


mfano:


1. Kununua kuku na kuja kuziuza sehemunyingine- hapa hakuna ulicho ongeza zaidi ya kuwalilia wanao kuzia wakuzie beiya chini na wewe ukauze bei ya juu. Haujaongeza thamani yoyote ile kwenye hawakuku

2. Unanunua magunia ya mahindi kutokadodoma na kupeleka dar- hapa hakuna cha maana ulicho fanya ila usaniiutafanyika wakati wa kununua utumie ndoo kubwa iliyo fanyiwa modfication, nawewe wakati wa kuuza lazima uchanganye mahindi mazuri na mabaya ulio nunua kwabei ya chini. Bila kuchanganya haya mahindi huwezi pata faida
- hapa unakuwa hujaongezea hayamahindi thamani yoyute ile

3. Kwenye swala la ng'ombe nalolinahitaji usanii tu, ukawalilie wanao kuzia il wakupunguzie na wewe upatekafaida.

umefika wakati wa kufanya biashara zakuongeza thanani

1. Nunua ng'ombe chinja na supplynyama hapa unakuwa umeongeza thamani
-au fungua kiwanda cha kupaki kabisana kuuzia watu wa supermarket, hapa unakuwa umefanya biashara ya maana sana

2. Nunua mahindi saga na paki unga,hapa unakuwa umeyaongezea hayo mahindi thamani kubwa mno na utapata faida

3. Nunua kuku chinja, pack na uza-
hii ndo biashara ya kuad value, lakinihii ya kununua mchele kutoka morogoro na kuja kuuza dar inahitaji usanii wakuchanganya mchele wa morogoro na ule wa thailandla sivyo hakuna chachote kile utakacho faidi

ndo maana hii biashara haihitaji akilibali usanii wa kuibia wateja, na si endelevu

huo usanii si ndio akili yenyewe?
 
Heshima kwenu wazee wa Jukwaa hili Ikimpendeza MUNGU kuanzia Mwaka ujao nitaingia Rasmi kwenye ufugaji wa NOA na Wanyama wengine nakwakuwa mambo hayo yanahitaji MTAJI wakutosha ili kz niifanye kwa uhakika nimeona nifanye Biashara ya Mbuzi kuchukua Mikoani na kuleta DAR OMBI kwaanaejua ni MKOA upi naweza kupata MBUZI kwa Bei nzuri ikiwezekana na Bei ya kila mbuzi 1 Mpaka sasa naendelea na utafiti mdg wa SOKO la uhakika ukiacha pale VINGUNGUTI natanguliza Shukrani,,,!!!
 
Heshima kwenu wazee wa Jukwaa hili Ikimpendeza MUNGU kuanzia Mwaka ujao nitaingia Rasmi kwenye ufugaji wa NOA na Wanyama wengine nakwakuwa mambo hayo yanahitaji MTAJI wakutosha ili kz niifanye kwa uhakika nimeona nifanye Biashara ya Mbuzi kuchukua Mikoani na kuleta DAR OMBI kwaanaejua ni MKOA upi naweza kupata MBUZI kwa Bei nzuri ikiwezekana na Bei ya kila mbuzi 1 Mpaka sasa naendelea na utafiti mdg wa SOKO la uhakika ukiacha pale VINGUNGUTI natanguliza Shukrani,,,!!!

Maeneo ya mkoa wa manyara kuna wafugaji wengi kama uko serious nikutafute mkuu
 
Lushoto, Korogwe pia ila msimu mzuri wakulima wawe wameishauza mazao yao yameisha utapata bei nzuri. Mifugo ndio assets au akiba yao huuzwa waklwa hawana kitu kama wametoka kuvuna mazao utapata kwa shida na bei juu. Hadi mwaka jana bei ya juu ilikuwa elfu 40 ila upate mwenyeji pia.
 
Maeneo ya mkoa wa manyara kuna wafugaji wengi kama uko serious nikutafute mkuu

Niko serious MKUU wangu ndomana nataka kujua wapi Ntawapata kwa bei nzuri Unaweza kujua huko Bei zao zikoje? nachangamoto za huko natanguliza Shukran!
 
Asante MAMA JOE! Kwa uzoefu wako unadhani nikipindi gani DEC? au? Unaweza kuwa na mtu wa Uhakika ukanielekeza kwake nijaribu kuchek nae? Km hutajali
Barikiwa ndg!
 
Kwa mwezi wa 12 soko liko UCHAGGANI, egesha mbuzi "wanono" pale Njia panda himo, Uchira na pale YMCA - moshi
usijeleta visivyonona manake ndo wanahamisha hela DSM na mikoammingineyo kupeleka kwao UCHAGGANI
 
Matola unaweza kusaidia hapa?
Natanguliza shukranj
 
Last edited by a moderator:
Niko serious MKUU wangu ndomana nataka kujua wapi Ntawapata kwa bei nzuri Unaweza kujua huko Bei zao zikoje? nachangamoto za huko natanguliza Shukran!

Mkuu kwa sasa cjafika kwenye minada muda kidogo ila kuna rafiki zangu ni wamasai na pia ni wafugaji nitawatafuta alafu nitakupa info zaidi kipindi kizuri ni kwenye kiangazi bei inakua nzuri sana changamoto ni usafiri ukiwa na usafiri wa uhakika wa kuzunguka kwenye minada nta ku pm no zangu.
 
Kwa mwezi wa 12 soko liko UCHAGGANI, egesha mbuzi "wanono" pale Njia panda himo, Uchira na pale YMCA - moshi
usijeleta visivyonona manake ndo wanahamisha hela DSM na mikoammingineyo kupeleka kwao UCHAGGANI

Asante kwa Info Kiongozi nalifanyia kz!!
 
mbuzi wapo huku shinyanga kwenye minada, price ranges btn 40-60.. uliza bei hapo vingunguti, then ni-pm # yako. we cn do

Sawa mkuu nikishakamilisha utafiti wangu ntatupia Mawacliano yangu hapa hapa Jamvini
 
mkuu kwa sasa cjafika kwenye minada muda kidogo ila kuna rafiki zangu ni wamasai na pia ni wafugaji nitawatafuta alafu nitakupa info zaidi kipindi kizuri ni kwenye kiangazi bei inakua nzuri sana changamoto ni usafiri ukiwa na usafiri wa uhakika wa kuzunguka kwenye minada nta ku pm no zangu.

pamoja sana!
 
Yoyote mwenye kutaka order ya mbuzi anipigie tufanye biashara hapahapa Dar es salaam 0714064767
 
vip mi nataka kufanya hiyo biashara,je inalipa?wapi wanapitikana na wapi soko?nilisikia kuwa pugu soko linapatikana ni kweli? naomba kwa anaefahamu anidadavulie please!
 
Habari ndugu, marafiki na jamaa!!, naomben ushauri juu ya biashara hii ya ng'ombe, mbuzi au kondoo kuhusu soko na gharama za usafiri kutoka Ruvu(pwani) hadi sokoni!!, lakin si mbaya kama kuna mfanyabiashara hiyo akashirkiana nami!!!. huwa mm nanunua kwa wafugaji na kuuza kwenye masoko ya huku porini ambayo hayana bei!!.
 
Back
Top Bottom